inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Alhamisi, 28 Novemba 2013

AFYA: UNAJUA UNAKULA NINI KULINGANA NA KIPATO CHAKO?



T
unapozungumzia suala zima la afya bora ni hali ya kuwa vyema kimwili bila kuwa na ugonjwa au dalili ya ugonjwa.Watu wengi hujipongeza sana kwa kuamini kuwa afya ni unene…la hasha!
 Afya bora hujengwa/huboreshwa na makundi ya vyakula yenye virutubisho kama wanga,protini,vitamini, madini, mafuta, maji safi na salama.
Ukosefu wa lishe bora na ulaji mbaya umepelekea matizo mbali mbali kwa watoto na watu wakubwa.
Ukosefu wa kipato hupelekea kukosa lishe bora na wakati huo huo kuwa na kipato kikubwa hupelekea kuongezeka kwa uzito wa mwili uliyokithili sambamba na magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari,kansa na matatizo ya moyo.
Je, ulaji wako ni upi kwa kuzingatia mchoro ufuatao…A au B?


Jichunguze kwa makini, jiweke katika mfumo husika wa ulaji...A au B, Jiulize, hivi nilivyo kiafya ni sahihi kulingana na kanuni za ulaji bora? Ikiwa si sahihi, Jielimishe Kwanza kwa kuuliza wataalamu wa lishe,soma vitabu, makala na majarida muhimu kuhusu afya.
Ikiwa hujanielewa, usisite kuniandikia au kunipigia simu...nitakuelewesha. 
Nakutakia kila la heri katika zoezi hili muhimu la kuboresha afya yako na wengine.

Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!

Jumamosi, 23 Novemba 2013

AFYA: KUCHEMUA/KUPIGA CHAFYA, KUKOHOA KWA KUTHAMINI AFYA YA WENGINE

--> -->
K
atika kufuatilia kwa ukaribu tabia na mazoea ya watu mbalimbali jijini Dar es salaam kwa suala linalohusu afya, Jielimishe Kwanza! imegundua na kusikitishwa kuona watu wengi huchemua/hupiga chafya bila kutumia kitambaa safi ili kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya magonjwa yasambaayo kwa hewa kama mafua na kifua kikuu.
Naomba radhi kwa maneno makali nitakayoyatumia…ni kwa lengo zuri tu la kukumbushana na kuelimishana!
Wapo wanaotumia mikono yao kuzuia kusambaa kwa mate na makohozi au kushika pua kutoa kamasi na mara tu wakimaliza hutumia mkono kusalimiana na wengine…kwa kweli hii si nzuri kiafya.
Sambamba na kuchemua na kukohoa, wapo watu wengine hutema makohozi, mate hovyo bila kuzingatia kuwa kuna mtu/watu jirani yake.Kiuhalisia, tabia hii si nzuri kiafya na mazingira kwa ujumla.
Si lazima kwenda shule sana ndipo ijulikane kuwa kutumia kitambaa safi kufunika pua na mdomo ni muhimu kwa afya…utajisikiaje kuona mtu mwingine akikurushia mate/makohozi usoni kwa chafya? Ikiwa hatupendi kufanyiwa hivyo, tusiwafanyie wengine. Hili ni suala la uelewa tu, halihitaji kuwa na shahada.
Picha na news.discovery.com
Ikiwa una mazoea tajwa naomba uchukue hatua ya kubadika na kuwahamasisha wengine kubadilika.
Jali afya ya wengine kama unavyojijali, Punguza kuenea kwa magonjwa yanayoenezwa kwa hewa.

Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!

Jumanne, 19 Novemba 2013

BIASHARA: ELEWA KWANZA MTAZAMO WA WATEJA KABLA YA KULETA HUDUMA/BIDHAA KWENYE SOKO

-->

Makampuni mengi huwekeza fedha nyingi kwa utafiti wa masoko ya biashara zao lakini husahau suala muhimu sana la kujua kwanza mtazamo wa wateja.

Huu ni mtazamo mpya katika muundo wa biashara utakaokufanya ufanikiwe sana katika biashara yako:
 

Je, muundo wa biashara yako unawatazama wateja kwanza kabla ya kufikiria faida kutoka kwao?

Ukiihitaji ushauri kuhusu muundo wa biashara wenye mafanikio wasiliana na  
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!

Jumatatu, 11 Novemba 2013

VIJANA NA VIPAJI: Mkurugenzi mtendaji wa Jielimishe Kwanza! azindua “Evening Talk Program”



I
likuwa ni wakati mzuri kwa Jielimishe Kwanza! kupata fursa ya kushirikiana na Taasisi nyingine katika masuala mbali mbali ya kijamii.
 Asasi isiyo ya kiserikali ijulikanayo kwa jina “Human Talent Watch" (H.T.W) iliyopo Mbezi-Msuguli- jijini Dar es salaam imeanzisha program maalumu ya kuibua na kukuza vipaji kwa vijana ijulikanayo kwa jina la “Evening Talk Program” ikimaanisha “maongezi rasmi ya jioni “ kwa kuwashirikisha watu waliofanikiwa kwa kutumia vipaji ili kuwatia moyo na kuwapatia mbinu  vijana chipukizi katika vipaji husika.

Programu hiyo maalumu na yenye tija kwa vijana wenye vipaji nchini Tanzania ilizinduliwa Jumamosi , 9 Novemba 2013 na Mkurugenzi mtendaji wa Jielimishe Kwanza! ndugu Henry Kazula majira ya jioni.

Akiongea moja kwa moja na mwandishi wa Jielimishe Kwanza! mwenyekiti wa H.T.W ndugu Frank Mihayo alifanunua zaidi malengo ya “Evening Talk Program”, alisema;

…programu hii ni maalumu kwa kuwakutanisha vijana wenye umri kuanzia miaka 12-35 pamoja ili kujifunza/kupata mbinu mbali mbali zitakazowasaidia kutimiza ndoto zao. ”Evening Talk” ni chimbuko la la maarifa sahihi kwa vijana-“a source of perfect knowledge”.Pia ni fursa maalumu kwa vijana chipukizi wenye vipaji kukutanishwa na vijana mashuhuri waliofikia mafanikio ya ndoto zao katika nyanja mbali mbali-sanaa,uchumi,uongozi na biashara.

Ndugu Mihayo alikazia zaidi kuwa, watu waliofanikiwa kwa vipaji vyao watapata fursa ya kutoa mada zenye kuchochea hamasa ya mafanikio kwa vijana kupitia vipaji. Kwa vijana chipukizi watapata fursa ya kujijengea hali ya kujitambua,kujiamini,kujifunza mambo mapya kuhusiana na vipaji na kupata nafasi kuunganishwa na wadau mbali mbali.

Katika kutimiza azma ya mpango huu kuna changamoto zifuatazo;

  1.       Kukosa ukumbi wa kuendeshea programu hii
  2.       Ukosefu wa fedha za uendeshaji kama kalamu na madaftari ya kuhifadhia kumbukumbu
  3.      Fedha ya kuitangaza programu hii kwenye vyombo vingine vya habari ili vijana wengi wapate fursa ya kushiriki na kujifunza.
 ____________________________


MATUKIO KATIKA PICHA

Mkurugenzi mtendaji wa Jielimishe Kwanza! ndugu Henry Kazula akikata utepe kuashira kuzinduliwa kwa programu maalum kwa vijana ijulikanayo kama "Evening Talk".Kulia kwake ni Mwenyekiti wa H.T.W ndugu Frank Mihayo.


Mkurugenzi mtendaji wa Jielimishe Kwanza! ndugu Henry Kazula akiongea na vijana wenye



vipaji vya mpira,muziki na uigizaji.




Katika nyuso za furaha vijana wenye vipaji vya muziki,uigizaji na mpira wakiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Jielimishe Kwanza! ndugu Henry Kazula kwa pamoja na Mwenyekiti wa H.T.W ndugu Frank Mihayo.



Mwisho wa yote, mgeni rasmi alipewa fursa ya kuongea na vijana; alijaribu kuwashirikisha kwa kurejea moja ya makala zake kupitia Jielimishe Kwanza! ijulikanayo kwa kichwa

“Jinsi ya kupaza sauti ya mafanikio na jamii ikukubali" Soma hii  http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/05/jinsi-ya-kupaza-sauti-ya-mafanikio.html

Ikiwa umeguswa na program hii na unataka kuchangia kwa njia moja au nyingine usisitize kuwasiliana na Mwenyekiti wa H.T.W kwa namba +255 752 297 264 au muandikie kupitia barua pepe humantalentwatch@gmail.com

Imetayarishwa, Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!






Jumatano, 6 Novemba 2013

MTAZAMO: KISAIKOLOJIA, KUMWAMBIA MTOTO/MWANAFUNZI KUWA WEWE NI SIFURI, NI SAWA NA KUUA KIPAJI CHAKE…

Picha na ii4oc.com

N
ikiutazama mfumo wa elimu hasa kwa nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara, umelenga sana katika ufaulu wa masomo ya kitaaluma ili mwanafunzi aanze safari yake kujikomboa kimaisha bila kuangalia kipaji cha mwanafunzi husika, ikimaanisha kuwa taaluma kwanza, kipaji baadaye.

Imezoeleka kuwa ili mtu afanikiwe katika maisha yake ni lazima afaulu sana katika masomo yake awapo shuleni.Vipi kuhusu kutambua na kukuza kipaji cha mtoto/mwanafunzi bila kuangalia masomo ya kitaalamu? Ikiwa kuna ushahidi wa kutosha wa watu  maarufu waliotumia vipaji vyao kujiajiri pia kuajiri wengine, tunaweza kuliona hili kwa mtazamo mwingine chanya wa mabadiliko katika elimu.
Ukiangalia nchi nyingi zilizoendelea kiuchumi, hazijapuuza hata kidogo kipaji alichonacho mtoto/mwanafunzi…wanaangalia kwanza akipendacho mtoto kulingana na kipaji chake.Kuanzia hapo mtoto huanza kukuzwa kwa kujitambua na kunoa kipaji chake.
Masomo mengine ya utaalamu huchukuliwa kama ziada.Mtazamo huu ni mzuri kwa sababu mtoto/mwanafunzi akishindwa kufanikiwa katika masomo yake ya kawaida(masomo ya utaalamu), anajikita moja kwa moja katika kuonyesha kipaji chake kilichonolewa.
Nikitoa mfano halisi nchini Tanzania, wataalamu wa masula ya elimu wamekuwa na mtazamo kuwa ili mtoto afanikiwe maishani ni lazima apate matokeo kuanzia daraja la I hadi la III.Kuna kundi la wanafunzi wengine wa daraja IV na wale wa daraja 0…je vipi kuhusu hawa? Ni kweli hawawezi kufanikiwa maishani? Vipi kama kutakuwa na utaratibu wa kuchunguza na kutambua vipaji vyao ili vitumike kujiletea kipato? 
Katika siku za hivi karibuni, nchini Tanzania,Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ilitoa tamko la kubadili madaraja na viwango vingine vya ufaulu.Lililokereketa umma wa wananchi na wataalamu wengine wa masula ya elimu ni lile la kubadili jina tu la divisheni 0 kuwa divisheni V.
Nikirejea mtazamo wa kisaikolojia, mtoto/mwanafunzi akiambiwa kuwa wewe ni “sifuri” inamjenga kuwa katika dunia hii yeye hawezi kufanya lolote akijilinganisha na wengine.
Mtazamo wa Jielimishe Kwanza! kuhusu badiliko la divisheni sifuri kuwa divisheni V ni kwamba,  badiliko la jina halitabadilisha alama la kundi hilo bali ni kumpoza mwanafunzi kisaikolojia ili asijione kuwa hawezi kabisa.Hivyo basi anaweza kufanya kitu kingine nje ya mfumo rasmi wa elimu uliomtenga kitaaluma na si kipaji chake.
Imefika wakati muafaka wa kuhamasisha wadau wote wa elimu kulitazama suala la kipaji cha mtoto/mwanafunzi kuwa kipaumbele kabla ya masomo ya kitaaluma, pia ni vyema kumfundisha mtoto/mwanafunzi kwa kile alichonacho, anachokifahamu, anachoweza kufanya kwanza. Hii itamsaidia mtoto/mwanafunzi kuwa na wigo mpana wa kufanya kile moyo wake unapenda kwa ufanisi mkubwa.
_______________________________
“Sometimes we fight who we are, struggling against ourselves and our natures. But we must learn to accept who we are and appreciate who we become. We must love ourselves for what and who we are, and believe in our talents.” Harley King
________________________________________________________________________________
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!










Ijumaa, 1 Novemba 2013

ELIMU NA SAIKOLOJIA: MBADALA WA ADHABU YA VIBOKO KWA WANAFUNZI


M
akala hii  ni muendelezo wa makala ya Jumapili, 27 Octoba 2013 katika eneo la elimu kuhusu mtazamo wa Kisaikolojia kuhusu adhabu ya viboko mashuleni:


Picha www.brisbanetimes.com.au
Zifuatazo ni mbinu mbadala wa adhabu ya viboko zinazofuata taratibu za Wanasaikolojia, zinazoweza kutumiwa na mwalimu au mzazi bila kuleta madhara kwa mwanafunzi/mtoto wakati huo huo zikichochea tabia njema na ufaulu;


1.CHUNGUZA CHANZO CHA TABIA MBAYA YA MTOTO
Hupaswi kumwadhibu mtoto/mwanafunzi kwa viboko au adhabu nyingine ya kuutesa mwili wake kama amekiuka kanuni, au kuonyesha tabia mbaya.
Fuatilia kwa makini ukitafuta chanzo cha mabadiliko ya tabia yake,mpatie ushauri nasaha ukimfanya ajichunguze tabia yake, wakati huo huo ukimuelekeza madhara ya tabia yake mbaya.
Kubaliana naye kubadilika kwa kupanga naye mikakati iliyo na faida kwa mtoto/mwanafunzi(mfano-mkakati utakao chochea kujisomea na kuepuka tabia mbaya.

2. KEMEA TABIA MBAYA
Onyo litolewalo kwa mdomo ni adhabu yenye kugusa hisia ya ndani kwa mtoto/mwanafunzi kuliko adhabu ya viboko.Kemea kuonyesha kutoridhishwa na tabia mbaya au ufunjivu wa kanuni na maadili.
Zingatia: Mbinu hii ni nzuri na ina matokeo mazuri kama tu haitatumika mara kwa mara.Mtoto/mwanafunzi huweza kuchukulia kama mazoea na kutoa tafsiri kuwa mwalimu/mzazi ana hasira/mkali wakati wote ikitumika mara kwa mara.

3. TAFAKARI KWA PAMOJA NA MTOTO/MWANAFUNZI KUHUSU TABIA MBAYA
Tenga muda wa kukaa na mtoto/mwanafunzi kujadili madhara ya tabia mbaya au kukiuka kanuni mlizokubaliana.

4. TUMIA ZAWADI KUCHOCHEA TABIA NJEMA
Pongezi kwa mtoto/mwanafunzi huchochea kuendelea kwa tabia njema.Inaweza kuwa ya kitu cha kushikika au maneno ya pongezi.
Pia, mpongeze mtoto/mwanafunzi anapoonyesha kuwa na tabia njema.
 
Angalizo:Unapaswa kuwa makini sana katika kutoa zawadi kwa mtoto/mwanafunzi.Anaweza kuigiza tabia njema ili akufurahishe ilihali amaanishi kutoka moyoni. Ni vizuri kutompa mtoto/mwanafunzi zawadi mara kwa mara kila anapokufurahisha/anapoonyesha tabia njema.Kufanya hivyo hupoteza maana halisi ya zawadi, mwisho mtoto/mwanafunzi huchukulia zawadi kama mazoea au kitu cha lazima akiwa ameonyesha tabia njema.
 Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!