inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumapili, 22 Desemba 2013

MTAZAMO: KUELEKEA MWAKA 2014, TUJIELIMISHE! TUJIFUNZE! TUJIPANGE UPYA KUPITIA MAKOSA…



K
ujifunza kwa kweli na kwenye tija ni kupitia MAKOSA yaliyofanyika awali, hii ni kwa sababu, hayo ndiyo yametufikisha hapa tulipo.
Nikiwa katika mapumziko, sehemu tulivu yenye upepo mwanana pembezoni mwa Mlima mrefu Afrika, uliopo nchini Tanzania-Mlima Kilimanjaro (http://www.tanzaniaparks.com/kili.html), nafakari kuhusu mwaka 2013 na kupanga mikakati kuelekea mwaka 2014…naamua kuperuzi katika maktaba yangu ndani ya “laptop” nakutana na kijitabu kiitwacho “Tujisahihishe” cha Mwl.J.K.Nyerere (1962) chenye kurasa 8.
Nikashawishika na jina la kijitabu hicho, hivyo nikataka kujua kulikoni ndani yake…Mwanzoni ilibaki kidogo niachane nacho, kwa sababu kilikuwa kikielezea makosa ndani ya T.A.N.U, najua hata wewe unaweza kusema nani anasoma vitabu vya T.A.N.U hadi leo?
Nikakumbuka msemo huu; ya kale ni dhahabu, ikanijia shauku ya kutaka kuyajua makosa hayo…yawezekana yamekufikisha/yametufikisha hapa tulipo.Nikaanza kusoma kwa makini na kufumbuka macho kujionea makosa ya mwaka 1962 ambayo Watanzania tunaendelea kuyafanya kwa kujua, kwa mazoea au kutojua…
“Nitanukuu moja ya makosa yaliyoainishwa na Mwalimu, Jielimishe Kwanza! inaliona kosa hili kubeba makosa mengine tunayoyafanya kila siku;
Kosa jingine ni kutojielimisha.Kanuni yetu ni moja inasema: “Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu wote na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote”. Kwa ufafanuzi zaidi, anasema; Kujielimisha siyo maana yake kwenda shuleni. Kujielimisha ni kutafuta ukweli wa mambo. Kwenda shule hutusaidia.Lakini japo hatuwezi kwenda shule twaweza kujifunza”.
Watu wengi hukoma kujielimisha mara tu wakihitimu masomo yao na kufikiri kuwa wanajua kila kitu.Mwl.J.K.Nyerere katika kitabu hicho anawaainisha:
 “watu walio hatari sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu wala hawana haja kujifunza zaidi.
Nabainisha haya kwa kukuhamasisha ndugu msomaji kukaa chini na kutafakari makosa uliyoyafanya mwaka 2013 ili usiyarudie mwaka 2014.
Ikiwa unajiona hukufanya kosa au makosa, tambua kuwa hakuna mkamilifu katika dunia hii…Maandiko Matakatifu yamebainisha.Nilihamasika sana na mwisho wa kitabu cha Mwalimu, aliweka wazi, nanukuu; sitaki Mtu ye yote afikiri kuwa mimi niliyeandika maneno hayo sinayo makosa.Hivyo si kweli.Hii na kwangu kadhalika, najifunza sana kupitia makosa ninayofanya.
Naomba nisiwe msimuliaji sana wa maneno ya Mwalimu, hamasika kujisomea mwenyewe kijitabu hicho ili ujue makosa mengine ili yasijirudie kwako.
Tena na tena, naomba utumie wakati huu mzuri wa mapumziko kujichunguza mapungufu yako yaliyopelekea kufanya makosa uyajuayo.Jielimishe! Jipange upya kwa kujiwekea mikakati ukijifunza kwa makosa.
Nakutakia mapumziko mema na kukutakia heri na fanaka ya Krismasi na Mwaka mpya 2014.
Imetayarishwa na
Henry Kazula,
Mkurugenzi mtendaji.
Jielimishe Kwanza!

Alhamisi, 19 Desemba 2013

MTAZAMO: TASWIRA UNAYOWAJENGEA WATU WENGINE INAKUWA UHALISIA WAKO…


“The image you create about others and think it is real, becomes your reality”-Henry Kazula.

M
ara nyingi tumekuwa tukiwafikiria na kuwasema wengine kinyume na uhalisia wao.Kuna watu huwafikiria wengine mabaya tu, pia kujiaminisha kuwa mafanikio ya wengine si ya halali au maisha wanayoishi wengine si halisi.
Yaani, tunawafikiria wenzetu mabaya! mabaya! tu.Huu ni mtazamo hasi uliojijenga ndani ya nafsi za watu.
Kwa kipindi kirefu Jielimishe Kwanza! imefuatilia suala la mtazamo wa watu kuhusu maisha na watu kwa ujumla.Imebainika kuwa ukiwasikiliza watu 5 kuhusu ufikiri/mtazamo wao kwa watu fulani waliofanikiwa na hata wale wasiofanikiwa utagundua kuwa ni mmoja tu atakayetoa maelezo yenye mtazamo chanya.Kama huamini, fanya jaribio hili la kupima mtazamo wa watu.
Ikiwa taswira unazojingea kuhusu wengine ni hasi, huu utakuwa ni uhalisia wako! na utajiaminisha, utakuwa ni mtu wa manung’uniko, masengenyo, kukata tamaa ya maisha kwa kujiaminisha kuwa huwezi kufanikiwa kwa njia ya halali inayohusisha juhudi zako binafsi.Madhala yake kwa Taifa ni makubwa, hususan kuongezeka kwa wimbi la umasikini na utegemezi ndani ya jamii.
Pia utajikuta umeanza kujijengea mbinu zisizo sahihi kupambana na uhalisia unaofikiria kuhusu hali na tabia ya maisha ya wengine.
Nikirudi kwenye mahusiano kwa wanandoa, kuna hatari kubwa endapo mmoja wa wanandoa atakuwa na taswira hasi kuhusu mwenziwe.Mfano, mmoja akimfikiria na kujenga taswira kuwa mwenziwe anatoka nje ya ndoa, itamjenga na itakuwa ni uhalisia wake bila ya kuwa na utafiti wa kina.Hili hupelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi kwa sababu ya kukosa kuaminiana.
Nakuhamasisha ndugu msomaji, kubadili mtazamo kwa kujifunza jinsi ya kuishi na watu na kufahamu njia halali za mafanikio yao…fuatilia historia zao ili uwe na uthibitisho wa unachokiamini, kufikiria kabla ya kutoa ushuhuda mbele ya wengine.
Tukumbuke kuwa, Maaandiko Matakatifu yanatuasa kuwa si vizuri kufikiria na kuwasemea wengine mabaya.
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!

Jumatano, 18 Desemba 2013

MTAZAMO: MAKOSA 10 YANAYOWEZA KUINYIMA AKILI YAKO UHURU WA KUFANYA KAZI YAKE BARABARA...

-->
T
 ukikumbushana moja ya makala zetu kuhusu viashiria vya kutekwa kwa uhuru wa fikra,mtazamo, uchumi wa mtu binafsi http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/12/mtazamo-hivi-ndivyo-uhuru-wako.html
Picha na stepontoliquid.wordpress.com
naomba nikulete kwenye makala ya  leo kuhusu makosa yanayoweza kuinyima akili uhuru wa kufanya kazi yake barabara-(mbele ya kila kosa kuna suluhisho);
1.   Kutojielimisha-kujielimisha ni njia ya kujua ukweli wa mambo
2.  Kupuuza usomaji wa makala na vitabu- ukweli wa mambo hufahamika kupitia kulinganisha mawazo ya watu tofauti tofauti…Unasoma mawazo yao kupitia vitabu au makala zao au kuongea nao.
3.   Kupuuza mawazo ya wengine-kuwa msikivu zaidi na si muongeaji zaidi bila kupuuza wazo la mwingine
4.   Kujifanya mjuaji wa yote-tambua kuwa siku zote tunajifunza vitu vipya, huwezi kujua kila kitu
5. Kuwa na majibu rahisi kwa maswali magumu(huu ni uvivu wa kufikiri)-tuepuke kubashiri kwa hisia na kutoa majibu rahisi ya matatizo/maswali magumu…tuiruhusu akili yetu itafakari kwa kujiuliza maswali ya msingi na kutoa majibu ya matatizo.
6. Kuchagua viongozi wasio na sifa…hawa hukunyima fursa ya kutoa mawazo yako na kukufanya uwe mtumwa wa fikra zao-tuwapime viongozi kwa uwezo wao wa kuongoza wenye kujua wameteuliwa kwa manufaa ya wananchi na si unafsi.Tuwaepuke viongozi wanaoamini zaidi mawazo yao binafsi kwa manufaa yao na kuyafanya ya wengi.
7.   Kutumia pombe na madawa ya kulevya kupindukia-punguza au acha matumizi ya pombe na madawa ya kulevya.
8. Kutopata muda wa kukaa mwenyewe na kutafakari maisha yako-jiwekee utaratibu wa kukaa mwenyewe na kutafakari kuhusu changamoto za maisha.
9. Kutegemea wengine wakuamulie kila kitu au wakuthibitishie maamuzi yako-jiamini, tambua kuwa wazo lako ni wewe unayejua hatma yake.Ujue kuwa katika dunia hii kuwa wakatisha tama wengi.Wakati mwingine ni vyema kufanya mambo yatokee…ukikosea, jifunze tena kwa kupitia makosa hayo.
10. Hofu ya kukosea-Wavumbuzi wengi duniani walifanya makosa mengi sana…wakajifunza kupitia makosa.(Ungana nasi kwenye makala ijayo yenye kichwa:TUJIELIMISHE! TUJIFUNZE! TUJIPANGE UPYA KUPITIA MAKOSA…
Mfano wa Thomas Edison katika kuvumbua taa ya umeme alifanya makosa 1,000.Edison alichulia makosa haya kama ni njia 1,000 za kutengeneza taa ya umeme.Jifunze kwa watu mashuhuri duniani waliofanya makosa kupitia http://www.uky.edu/~eushe2/Pajares/OnFailingG.html 
Ikiwa hujanielewa na unahitaji ufafanuzi zaidi, tafadhali usisite kuwasiliana nasi.
Imetayarishwa na kutolewa na,
Jielimishe Kwanza!  


Jumatatu, 16 Desemba 2013

MTAZAMO: HIVI NDIVYO UHURU WAKO UNAVYOWEZA KUTEKWA

-->
Jielimishe Kwanza wanapoamua kukuelimisha kuhusu uhuru hawamaanishi wa nchi au Taifa ila ni ule uhuru wa mtu binafsi.Hii inamaanisha kuwa uhuru wa Taifa kwa ujumla wake unaanzia na mtu mmoja.
Picha na www.freedomideas.com
Nikimnukuu Mkurugenzi wa Jielimishe Kwanza! Henry Kazula katika moja ya mafunzo yake aliwahi kusema; "Mtu mmoja hawezi kuleta mabadiliko yote katika dunia, lakini mabadiliko duniani huanzia na mtu mmoja".
Taifa linaweza kuwa huru lakini watu wake wanaweza wasiwe huru kimtazamo, kiakili, kiuchumi na kifikra.
Ndugu msomaji najua kwa haraka haraka unaweza usinielewe…soma makala hii ukiirudia tena.Naomba nikukumbushe moja ya makala zetu inayoelezea na kutoa suluhisho la jinsi ya kuepukana na utumwa wa kifikra http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/09/mtazamo-hivi-ndivyo-tunavyoweza.html
Pia nikulete moja kwa moja kwenye suala la jinsi uhuru wako unavyoweza kutekwa na mtu mwingine bila wewe kujua. Vifuatavyo ni baadhi ya viashiria vinavyozingatia mtazamo wa kisaikolojia;
  1.       Kupewa vitu au fedha bure
  2.     Kutumika kifedha na si fedha ikutumikie (working for money and not money working for you).
Ikiwa una kiashiria kingine, tuandikie kupitia barua pepe jielimishekwanza@gmail.com
Hamasika! Hamasisha Uhuru wa Kimtazamo, Kiakili, Kiuchumi na Kifikra. 
Usikubali mtu atawale Uhuru wako!
“I know but one freedom and that is the freedom of the mind.” ~Antoine de Saint-Exupery
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!

Jumatano, 4 Desemba 2013

AJIRA: ATHARI YA KUFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA YA UTUMWA WA KISASA KWA MFANYAKAZI"


N
ikirejea makala zangu mbili kuhusu kazi na ajira: jielimishekwanza.blogspot.com/2013/10/ajira-na-kazi-jiepushe-zuia-utumwa-wa.html na http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/10/kazi-na-ajira-hivi-ni-viashiria-vya.html nataka nikujuze kuhusu athari kwa mfanyakazi aliye katika mfumo wa kazi wenye chembe chembe za Utumwa wa Kisasa kama ijulikanavyo kwa lugha ya Kiingereza (Modern-day Slavery).
 
Kutokana na utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Jielimishe Kwanza! katika maeneo mbali mbali ya kazi, umebaini  athari zifuatazo, ambazo huwapata wafanyakazi katika mazingira ya kazi;

1.Kushuka kwa hamasa na shauku ya kufanya kazi.Hivyo, wafanyakazi wengi wanafanya kazi kwa mazoea tu, bora siku ziende.

2.Kudhoofika kwa ubunifu na mbinu za utendaji wa mfanyakazi binafsi…mfanyakazi anakuwa na mtu wa kufuata maelekezo tu!

3.Kuongezeka kwa manung’uniko ya chini chini na migomo baridi kazini.

4.Kufanya kazi kwa hofu ya kukosa ajira…hapa ndipo uhuru wa mfanyakazi unapotekwa. Soma makala inatakayofuata: “Hivi ndivyo uhuru wako unavyoweza kutekwa”.

5.Kukosa fursa ya kuchangia na kutoa maoni katika kuboresha maslahi ya mfanyakazi…maamuzi ya uongozi ni ya mwisho haijalishi mfanyakazi ana mchango gani kwenye kampuni, shirika au taasisi.

Ikiwa unakumbwa na athari mojawapo kati ya hizi, jichunguze kwa makini, je una mchango gani katika eneo la kazi? Nini kinahitajika kazini ili uweze kuheshimiwa na kupata haki yako kulingana na jitihada zako?...ukiwa huna jibu sahihi au upo njia panda usisite kuwasiliana na jopo la Jielimishe Kwanza! katika eneo husika, utapata ufumbuzi wa kuishi kwa ndoto yako na kufuata kile moyo unapenda kufanya.
Tunakutakia kila la heri katika kupambana na utumwa wa kisasa katika maeneo ya kazi.
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!