inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumatano, 2 Aprili 2014

MAZINGIRA: NI JUKUMU LA NANI KUTUNZA USAFI WA MAZINGIRA?

Nimekuwa nikitafakari kwa kipindi kirefu kwa kutazama mtazamo na uelewa wa jamii  kuhusu usafi wa mazingira na kinachofanyika baada ya uchafuzi wa mazingira kutokea, nikajiuliza swali hili “nani mwenye jukumu la kutunza usafi wa mazingira?” bila shaka ukiwa mdau wa usafi wa mazingira, utajiuliza swali hili.Ikiwa hufahamu umuhimu wa usafi wa mazingira, utajua ni nani anahusika kutunza usafi wa mazingira ukiendelea kusoma makala hii.
Ili kuweka bayana suala hili la usafi wa mazingira, ni vyema tukajulishana au kukumbushana maana halisi ya neno “mazingira” …kwa uelewa wa kawaida, mazingira ni mjumuisho wa mambo yote yanayomzunguka binadamu, ukijumuisha mimea, wanyama na viumbe visivyo hai.Kwa lugha nyepesi, mazingira humtunza mwanadamu ukijumuisha mimea na wanyama.Hivyo, binadamu hupaswa kutunza na kuhifadhi mazingira  ili yamtunze, yatunze pia viumbe vingine vilivyo hali.
Binadamu anatajwa kuwa mstari wa mbele katika kutunza mazingira kwa sababu ana utashi wa kujua mema na mabaya.Pia ndiye wa kwanza kuanzisha shughuli mbali mbali za kibiashara na kiuchumi katika mazingira yanayomtunza.Ikiwa sanjali na shughuli hizo, mwanadamu ana jukumu la kuhakikisha mazingira anayoishi hayaathiriwi na shughuli zake kwa hali moja au nyingine.
Nimezungumza kwa mapana sana, sasa niguse wahusika moja kwa moja.Kutokana na mgawanyiko wa majukumu ya kila siku,tofauti za hali kiuchumi, na fursa ya kuwepo kwa teknolojia ya viwanda kumetokea matabaka katika jukumu letu sote la kutunza usafi wa mazingira.
Baadhi ya watu wamejitenga kabisa na jukumu hili muhimu kwa afya zao na za wengine kwa kusimamia maslahi pekee.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nisipothamini juhudi za watu wachache katika kuzingatia jukumu la ubinadamu la kutunza usafi wa mazingira.Mfano: vikundi vya kijamii, serikali kwa sehemu yake, Mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi.
Leo nitoe mfano wa shughuli zifanywazo na Shirika lisilo la Kiserikali “VoiceGiving” katika kusimamia usafi wa mazingira na kutoa elimu ya usafi wa mazingira jijini Dar es salaam-Tanzania. Shirika hili limenihamasisha sana kuhamasisha wengine kuhusu kuheshimu na kutunza mazingira yetu.
Picha na Voice Giving. Baadhi ya vijana wa Shirika la "Voice Giving" VG wakiwa kazini katika kituo cha basi jijini Dar es salaam.
Wanatumia njia shirikishi kuwahamasisha watu na kuwakumbusha jukumu lao la asili la kutunza usafi wa mazingira.Wameanza utekelezaji wa adhma yao kwa kuanza na mazingira ya vituo vya basi jijini Dar es salaam.Hutumia kauli mbiu kama “nipe fagio” na “taka  nomaa.”
Mwisho, najua kila mtu anapenda kuona mazingira yakiwa safi, najua binadamu ndiye anayetengeneza uchafu kutokana na shughuli zake za kila siku, pia hakuna mtu anayependa kukaa na uchafu, cha kushangaza zaidi watu huukimbia uchafu…ila kuna watu wachache sana huusika kusafisha mazingira.
Naomba tukumbushane wajibu wetu kupitia nukuu maarufu kutoka kwa mwanaharakati wa mazingira-Mahatma Gandhi aliposema “Be the change that you wish to see most in your world.” Kwa tafsili isiyo rasmi-“Uwe chanzo cha mabadiliko utakayo kuyaona” hivyo ukitaka kuona mazingira safi anza kuonyesha juhudi ya kuyaweka mazingira katika hali ya usafi, anzia nyumbani kwako.Chukia uchafu kwa vitendo, usisubiri mtu mwingine aje kuleta makabadiliko-wewe ni chanzo cha mabadiliko.
Imetayarishwa na kutolewa na Jielimishe Kwanza! 
Barua pepe: jielimishekwanza@gmail.com
+255 754 572 143