inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumapili, 18 Mei 2014

AJIRA NA KAZI: MUZIKI UNAPOHAMASISHA KUJIAJILI


-->
M
ara nyingi hupendelea kusoma magazeti ya ndani na nje ya Tanzania.Pia nasoma vitabu tofauti tofauti vyenye kuchochea mtazamo a chanya.

Mazoea haya huniwezesha “kujua ukweli wa mambo” unaoendelea katika jamii na maisha kwa ujumla, pia kuandika makala mbali mbali ndani ya Jielimishe Kwanza!… hii ikiwa ni dhana kubwa ya Jielimishe Kwanza! 

Hii haina madhara yoyote katika masuala yangu ya shule...najua! wenzangu na mimi wanaosomea shahada ya Uzamili-"Master's" hujikita zaidi kwenye kusoma mambo yanayoendana na masomo ya darasani tu! Nashauri, Wakati mwingine ni vizuri kusoma mambo yahusuyo jamii moja kwa moja na maisha kwa ujumla wake.


Leo, Jumapili, Mei, 18 2014  saa 24:0 AM nimekutana na gazeti la Tanzania liitwalo Mwananchi lenye kauli mbiu "Fikiri Tofauti" ...hakika kuna makala napenda nikushirikishe kuhusu suala zima la msomi wa Chuo kikuu kupenda/kutegemea/kutarajia kuajiriwa.


Mwandishi, Herieth Makwetta, wa gazeti hilo Kanihamasisha! Kukuhamasisha! kubadili mtazamo, hasa alipoandika makala kutokana na mahojiano ya msanii wa Hip Hop kutoka Kundi la Weusi, Nickson Simon almaarufu kama "Nikki wa II" mwenye shahada ya Uzamili katika maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDMS).

Ama kwa hakika, "Nikki wa II" ni mfano wa kuigwa kwa vijana wasomi wenye shahada nchini Tanzania. Ukiwa msomi wa Sekondari au chuo kikuu nakushauri sikiliza kwa makini wimbo wake mpya ujulikanao kwa jina la   “Sitaki Kazi” utakubaliana nami.

Naomba ufanyie kazi sehemu ya mashairi ndani ya wimbo wake, anasema; 
"Sitafuti kazi ila nataka nitafutwe na watu wanaotafuta kazi"
 Pia, anasisitiza kutokuwa mtumwa wa kazi sanjali na moja ya makala zetu kama; athari za kufanya kazi katika mazingira ya utumwa wa kisasa na  kufanya kazi unayoipenda.


Naomba nisiendelee kuandika zaidi, ili uweze kupata muda wa kusoma kwa haraka na kutafakari yaliyomo ndani ya wimbo huo.Nakutakia utendaji kazi mwema, najua tena siku ya Jumatatu!
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!



Jumapili, 4 Mei 2014

MTAZAMO: USITOE MAAMUZI HASI BILA KUFANYA UTAFITI WA KUTOSHA…

-->
 
Napenda kuanza kwa kuwapongeza wafanyakazi wote hasa kwa kuzingatia Mei mosi ilikuwa ni siku ya kilele cha sherehe ya Wafanyakazi.

Photo:http://www.mentoringminds.com/socratic
Nianze kwa kuuliza maswali; ni mara ngapi tumekuwa tukiwafikiria na kuwatendea wengine visivyo(hasi) na baadaye tunagundua kuwa haikuwa kama tulivyokuwa tunafikiria? Je,unajisikiaje katika hali hii ya kuujua ukweli? Bila shaka, hakuna anayeweza kupinga ukweli huu kuwa binadamu tunaamini sana hisia zetu na kujitengenezea majibu mepesi kwa maswali magumu kuliko kuamini akili zetu.
Sina maana kuwa hatutumii akili zetu,ila mara nyingine tunakuwa wavivu kidogo katika kutoa maamuzi sahihi, na hii ni kwa sababu hisia zetu huchukua nafasi kubwa katika mazingira fulani…majibu yatokanayo na hisia hayaumizi kichwa wala kuuchosha ubongo na ni ya haraka.
Mungu katupatia akili ili tufikiri kwa makini, kupambanua na “kujua ukweli wa mambo” kama Mwl.J.K.Nyerere alivyoandika katika kitabu cha TUJISAHIHISHE kuwa Kujielimisha Kwanza ni kujua ukweli wa mambo, huwezi kujua ukweli wa mambo kwa kuendeshwa na hisia.
Nikuhakikishie ndugu msomaji kuwa, hakuna kitu kibaya kama ukamfikiria ndugu au rafiki yako kimtazamo hasi na akatambua jinsi unavyomchukulia tofauti na alivyo kiasili.Itakupa shida sana hapo baadaye ukibaini ukweli wa mambo.Ikiwa unataka kujua ukweli wa mambo unapaswa pia kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kutoa maamuzi hasi. Soma
Hatupaswi kukurupuka na kujiwekea majibu ya kihisia…mfano: eti naona ndugu yangu hanichangamkii tena, nafikiri ameona sina kipato. Pia kutoa suluhisho la kupotelewa  pesa kisha kumshuku mtu fulani kaiba na unaanza kumvamia kwa maneno hata ngumi, baadaye kidogo unakumbuka kuwa kuna kitu ulinunua na mahesabu yako sawa…utajisikiaje katika hali hii?
Kuna madhara makubwa ya kutoa maamuzi hasi bila kuwa na utafiti wa kutosha.Nimejaribu kugusia kidogo baadhi ya madhara hayo hasa kuvunjika kwa uhusiano kwa kirafiki, hii inamwonyesha mwingine hali ya kutokuaminiana katika urafiki.
Ikiwa utahitaji kujua madhara mengine ya Kisaikolojia ya kutoa maamuzi hasi bila ya kufanya utafiti, tuwasiliane +255 754 572 143.
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!