inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumamosi, 25 Oktoba 2014

MTAZAMO: Wengine wamekosa kabisa…


Kuna wakati tunajiona na kujichukulia kama hatuna bahati, haki wala uwezo wa kumiliki vitu vya thamani, kusoma hadi ngazi za juu za elimu tuitakayo au kuwa na uhuru wa kipato kutuwezesha kutatua matatizo mengine ndani ya maisha yetu.Hii ni kwa sababu tunawaona wengine wakituzidi kimaisha kwa kumiliki vitu vya thamani na kusonga mbele kiuchumi ilihali hatujui wamepitia njia zipi kuvipata. Msemo ufuatao katika lugha ya Kiingereza unakazia...


Mwisho wa siku tunabaki kunung’unika, kulaumu wengine kwa wajibu wetu na hata kufikia hatua ya kumkufuru Mungu… “eti ana upendeleo” La hasha!
Tunasahau kuwa kwa vile au kile tulicho nacho, tukionacho kidogo kwa mtazamo wetu wa kibinadamu kuna wengine wamekosa kabisa na wanatamani wawe kama sisi. Je, ndugu msomaji unalitambua hilo? Pia una tambua kuwa kuna watu wengine hawajui walale wapi? na hawajui wale nini?... Haya ni maswali machache tu yanayoweza kututofautisha na wengine, na mwishowe kujiona tuna nafuu kuliko hao wengine.
Pia, ijulikane kuwa kuna watu ambao wanaombea kesho ifike salama, na wengine wanaomshukuru Mungu kwa uhakika wa pumzi tu! waipatayo kila siku ipitayo… kwa kifupi hawana uhakika wa maisha. Wengine ni wagonjwa wamelala vitandani kwa muda mrefu sasa…wanashauku kubwa ya kutembea na kufanya kazi tena.
Ndugu msomaji, kwa umakini kabisa naomba jichunguze, jilinganishe na wasio nacho na wenye shida utaona kuwa una nafuu kubwa kuliko hao wengine!
Ni sahihi kusema kuwa mwanadamu hatosheki na haridhiki kwa kile alicho nacho kwa wakati husika.Siku zote tunajitahidi kujiongeza, ndiyo maana matajiri hawachoki kutafuta pesa na mali…kila kukicha wanasaka pesa na kujilimbikizia mali, wakati huo huo watu wengine wakiwa hawaijui kesho yao.
Hali hii hukinzana kidogo na mtazamo wa mtaalam, mwanasaikolojia Maslow (1943, 1954) katika Maslow’s Hierarchy of needs” anasema; mwanadamu ana mahitaji yaliyoainishwa kwa ngazi 5 muhimu. Mwanadamu huamasika kufikia hitaji fulani…likitimia huitaji tena kufikia hitaji lingine, lingine na lingine. Inafikia wakati uhitaji wa mwanadamu “human needs” hufikia kikomo cha kujitosheleza kiasi cha kuweza kutoa msaada kwa wengine wasio nacho, hatua au ngazi hiyo ya juu namba 5, mtaalamu Maslow ameiita “self-actualization of human needs” … na ni nadra sana kufikia hatua hii kwa sababu ya vikwazo na kutotimiza mahitaji ya ngazi ya chini kama; hali ya kisaikolojia(1), usalama (2), uhusiano wa kijamii (3), na uwezo wa kujitambua na kujiamini(4).
Ngazi zote tano (5) ameziainisha kwa umbo la “pyramid”-umbo la nyumba za kihistoria za Wamisri, ukianzia ngazi ya chini (1) kwenda ngazi juu ya ukomo (5).
Katika hali isiyo ya kawaida, watu wanaoonekana wamefika kikomo cha uhitaji, wanaonekana kutoridhika na hali hiyo kiasi kwamba huendelea kuwanyonya kiuchumi wasio nacho.Nisiingie sana kiundani hapa kuwahusu hao waliofika hali ya kikomo cha uhitaji kama wanavyojiona. Sitaki kukuhamisha kwenye mada kuu…wengine wamekosa kabisa! Ila tuache kunung’unika, tulizike kwa kidogo tulicho nacho! ili kiwe chumvi ya hamasa katika kuelekea mafanikio makubwa tutakayo kuwa nayo.
Waswahili wanasema ridhika na kidogo ulicho nacho, usitafute makuu usiyoyaweza kwa wakati husika! Kinyume na hapo utaingia tamaa bure ya kuiba, kudhurumu wengine, kukiuka maadili ya kazi na hata kufikia hatua ya kuua wengine kwa kutamani pesa na mali.Sina maana tubweteke, kukaa na kusubiri miujiza au kuacha kukaza buti kujinasua kihalali katika hali ngumu ya maisha…La!
Huu ni mtazamo tu wa Jielimishe Kwanza! …unaweza kukusaidia, usikate tamaa.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza! Social Enterprise.

Jumatano, 22 Oktoba 2014

BIASHARA: HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUJENGA THAMANI YA UBORA KATIKA SOKO

-->

Ikiwa wewe ni mfuatiliaji wa makala zetu kuhusu biashara utaona kuwa tunasisitiza sana kuhusu kuboresha thamani ya ubora wa bidhaa ili kuliteka soko na pia kumshinda mpinzani wako katika kugombea soko.Soma zaidi




Sanjari na mtazamo thabiti wa kiuchumi kuwa; watu hulipwa kwa kupeleka thamani ya ubora kwenye soko ni dhahiri kabisa kuwa mtu hawezi kupata kipato halali pasipo kuleta thamani ya ubora katika soko.Katika lugha ya kiuchumi, soko ni watu.Hivyo, hakuna kipato halali kinachoweza kupatikana katika biashara yako kama huleti thamani ya ubora kwa watu; kutoa suluhisho la maumivu ya watu kwa maisha yao ya kila siku.
Kama ilivyo ada, wajasiriamali na wafanyabiashara hupaswa kutoa suluhisho la matatizo ya watu.Kuna kanuni (10) za msingi zinazopaswa kufuatwa kufikia kuleta suluhisho la matatizo pia kufikia lengo kuu na kujipatia kipato endelevu.Kanuni hizo ni;
1.    CHUNGUZA KWA MAKINI HUDUMA/BIDHAA ILIYOPO KABLA YA KULETA YAKO
2.    BORESHA MAPUNGUFU YA WENGINE, UPATE SEHEMU YA KUSIMAMIA
3. JIDHATITI KWA KUJITOFAUTISHA NA WAFANYABIASHARA WALIOPO UKIBORESHA UBORA ZAIDI
4.    HAKIKISHA HUTOI SIRI YA KUFANIKIWA KWAKO KATIKA SOKO
5.    JITENGENEZEE UPEKEE WA THAMANI YA UBORA KATIKA SOKO
6.    TENGENEZA WIGO WA SOKO LAKO NA USIMAMIE MSIMAMO WAKO
7.    WAKATI WOTE ANZA KUFIKIRIA KUHUSU WATEJA WAKO; WANAHITAJI NINI KWA WAKATI HUSIKA? NA SI UTAPATA NINI KWANZA KWA WAKATI HUSIKA:
8.    TENGENEZA MAHUSIANO MEMA NA WATEJA WAKO…ZINGATIA UHITAJI WAO
9.    FANYIA KAZI MAONI YA WATEJA WAKO KATIKA KUBORESHA UTHAMANI WA BIDHAA
10. HATA SIKU MOJA USISHUSHE BEI ZAIDI YA MPINZANI WAKO ILI UWAVUTE WATEJA KWAKO.
Tunakutakia kila la heri katika biashara yako.Ikiwa utahitaji ufafanuzi wa mbinu hizi (10), usisite kuwasiliana nasi:+255 754 572 143
             Imetolewa na

                                 Jielimishe Kwanza! SE

Jumanne, 21 Oktoba 2014

MTAZAMO: HIVI UNAJUAJE KAMA KILA KITU UNACHOAMBIWA NA KUTAZAMA NI KWELI?


Picha:http://lifeinzd.com/why-telling-the-truth-sucks-and-why-its-awesome-a-case-study/
Umewahi kujiuliza kama mambo uyaonayo na kuyasikia ni kweli? Kila siku tunaona na kusikia wengine wakitueleza masula mbali mbali kutuhusu au kuwahusu wao na kukurupuka katika kuyafanyia kazi bila kufanya utafiti wa kina.Soma hii pia. 
Lakini, ni mara ngapi tumejiuliza kama masuala hayo ni kweli kabla ya kuchukua hatua za makusudi za utekelezaji? Pia, ni nini hutuaminisha kuwa mambo hayo ni kweli? Au unajuaje kama makala hii ninayokuandikia uisome sasa ni kweli?
Kupitia maswali hayo ya msingi ni vyema nikakushirikisha mtazamo wenye msaada wa karibu kutoka kwa Wabuddha;
“Believe nothing. No matter where you read it, or who said it, even if I have said it, unless it agrees with your own reason and your own common sense.” …kwa tafsiri isiyo rasmi inamaanisha kuwa- “Usiamini chochote. Bila kujali umesoma mahali au kupitia mtu fulani na hata kama nimesema, isipokuwa tu kinaendana/kinashabihiana na upeo wako wa kufikiri na akili yako ya kawaida katika kutoa maamuzi". Msisitizo umewekwa kwenye upeo wa kufikiri na uwezo wa kawaida katika kutoa maaamuzi.
Je, unafanyaje kuboresha au kunoa upeo wako wa kufikiri na uwezo wako katika kutoa maamuzi sahihi kwa wakati husika? Kupitia makala zetu kuhusu mtazamo utaona kuwa tunasisitiza kuhusu Kujielimisha Kwanza! hii ikiwa ni njia pekee ya kujua ukweli wa mambo kama Mwl.J.K.Nyerere alivyoanisha katika kijitabu chake cha TUJISAHIHISHE.Kuelekea kujua ukweli wa mambo tunaboresha na kunoa upeo wetu wa kufikiri na ufahamu katika kutoa maamuzi sahihi na yenye tija.
Sioni haja ya kuficha au kuzunguka sana, la msingi ni kusoma mambo mengi kupitia vitabu,majarida yenye tija na kusikiliza hotuba mbali mbali sambamba na kulinganisha mawazo ya watu tofauti, changanya na uwezo wako wa kupambanua mambo kuhusu uhalisia wa jambo fulani katika maisha, mwisho kuweza kutofautisha mchele na pumba.
Pia jifunze jinsi ya kuunganisha matukio tofauti tofauti ili kukufikisha katika jambo au suala unalotaka kujua undani wake.Kupitia njia hizi unaweza kuwa mpelelezi wa kuijua kweli iliyo suluhisho la kututoa njia panda, na mwisho wa yote unaweza kutumia uzoefu huu kutatua matatizo mbali mbali ndani ya jamii.
Usikubali kudanganywa!... kwa maana anayekudanganya hukuchukulia wewe kama mtu usiyeweza kutumia upeo wake vizuri katika kupambanua mambo.Hivyo usije naswa katika mtego wa kudanganywa...tumia njia tajwa kufuatilia na kuujua ukweli wa mambo.
Kuna faida kem kem za kujijengea tabia ya kupeleleza na kujua ukweli kuhusu jambo au mambo fulani, kuanisha chache;
1.KUEPUKA MIGOGORO ISIYO YA LAZIMA
2.KUTATUA MATATIZO KIRAHISI BILA UPENDELEO WA UPANDE FULANI
3.KUJIONGEZEA WIGO WA KUFAHAMU MAMBO MENGI YENYE TIJA KWA MAISHA YETU
4.HUTUPELEKEA KUWA NA MTAZAMO CHANYA WA MAISHA NA KUWAJUA WENGINE KIUNDANI BILA KULETA UGOMVI
5.KUWA NA UHURU WA NAFSI ISIYO NA MAWAA
6.KUWA NA FURAHA ILIYO MUHIMU KWA AFYA
7.KUEPUKA MSONGO WA MAWAZO USABABISHWAO NA KUTOFAHAMU UNDANI WA JAMBO FULANI
8.KUONDOKANA NA ADUI WA MAENDELEO- UJINGA
9. KUJITOA KATIKA UELEWA WA NJIA PANDA.

Jielimishe Kwanza! Jifunze na utafute kuijua kweli itakuweka huru!
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza! SE