inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Ijumaa, 20 Februari 2015

MTAZAMO: NINI KIPIMO CHA MAFANIKIO YAKO?


In order to succeed, your desire for success should be greater than your fear of failure.-Bill Cosby
__________________________

www.e-marketingassociates.com
Picha na www.e-marketingassociates.com
Tunapozungumzia mafanikio ni ile hali ya kujihisi vizuri kutokana na kuishinda au kuzishinda changamoto zilizopo na zile zinazojiinua katika maisha; ukizingatia kuwa kuna mapitio kadha wa kadha yenye changamoto mbali mbali katika kuelekea kutimiza malengo tarajiwa. Kama ilivyo kawaida kuwa katika kuelekea mafanikio,changamoto nazo hazikosi kujitokeza.
Mafanikio ya kirahisi bila kulipa gharama kupitia changamoto yana mashaka! Wanawake waliambiwa utazaa kwa uchungu na mwishowe kufurahia mtoto aliyezaliwa na kusahau hali ya uchungu wao, vile vile kwa wanaume waliambiwa utakula kwa jasho mwishowe kusahau machungu ya kazi zao kipindi cha kusheherekea mafanikio; Maandiko Matakatifu yameainisha kuhusu hili.
Hakuna mtu asiyependa kutimiza malengo yake yaliyo sanjali na shauku ya mafanikio. William Henry "Bill" Cosby mchekeshaji na mwana harakati maarufu mwenye mafanikio makubwa duniani anaweka angalizo kuhusu jinsi ya kupata mafanikio kwa kuzingatia shauku ya mafanikio kwa kusema; “ili kufanikiwa, shauku ya mafanikio yako inapaswa kuwa kubwa kuliko hofu ya kushindwa.”
Ukifuatilia kwa makini mtazamo wa Cosby kuhusu mafanikio utabaini kuwa watu wengi hukinzana naye kwa kutanguliza hofu ya kushindwa kabla ya kukabiliana na hali halisi kuelekea mafanikio yenye msukumo wa ndani wa shauku ya mafanikio
Kipimo Cha Mafanikio
Watu wengi wanashindwa kuweka uwiano mzuri kati ya shauku ya mafanikio na hofu ya kushindwa…uhalisia uliopo ni kwamba, watu wengi hutawaliwa na hofu ya kushindwa ipelekeayo kuelemea shauku ya mafanikio! Sambamba na hali hii tujiulize maswali ya msingi kuhusu kipimo cha uwiano wa mafanikio; je, nini kipimo cha mafanikio ya mtu binafsi? …je, ni ule uwezo wa mtu kuzishinda changamoto? au ni ule uwezo wenye uthubutu wa kuishinda hofu ya kushindwa kwanza?
Kutoa majibu ya maswali hayo si jambo la haraka haraka; namaanisha si kuangalia kigezo kimoja na kujiaminisha au kujiridhisha kimtazamo.Mara nyingi katika mafunzo yangu nasisitiza kuwa; mtazamo ulionao kukuhusuukijilinganisha na ule wa watu wengine unakuwa uhalisia wako kama utaamini nakujichukulia.(Mfano: mtu aweza kujiaminisha kuwa mafanikio ya wengi kiuchumi si kwa njia halali; ni lazima ufanye wizi, ukiuke taratibu za kiutendaji, utumie uchawi au ufanye mauaji…huu unakuwa uhalisia wa maisha yake kwa sababu ni mtazamo wake uliohusisha kujiaminisha.
Mafanikio ya kweli, yenye kuzingatia shauku ya mafanikio kwanza kuliko hofu ya kushindwa hupimwa kwa kuzingatia uwezo wa kifedha/kipato halali (uhuru wa kipato) kukidhi mahitaji mbali mbali ya kibinadamu (human needs) sanjali na kutimiza hitaji la msingi la kisaikolojia (uhuru wa nafsi na fikra).
Kutimiza hali ya kisaikolojia sambamba na mafanikio inatazamwa kwa jicho lingine na mwanasaikolojia Maslow (1943, 1954) hasa katika kutimiza mahitaji ya kibinadamu kupitia hatua au ngazi ya juu namba 5, mtaalamu Maslow ameiita “self-actualization of human needs” … na ni nadra sana kufikia hatua hii kwa sababu ya vikwazo na kutotimiza mahitaji ya ngazi ya chini kama; hali ya kisaikolojia (1), usalama (2), uhusiano wa kijamii (3), na uwezo wa kujitambua na kujiamini(4).
Katika hali isiyo ya kawaida, watu wengi wamekuwa wakipima mafanikio yao au ya wengine kwa kipimo cha macho ya matamanio pekee hasa kwa kuangalia umiliki wa mali (material things) kama kumiliki magari, majumba ya kifahari na mengine mengi yanayovuta macho na hisia lakini kusahau hali ya kisaikolojia kama vile furaha, uhuru wa nafsi na fikra n.k. Pia wanaamini kuwa pesa pekee huleta furaha na uhuru wa fikra na ule wa nafsi.
Ndugu msomaji, ijulikane kuwa kupima mafanikio yako yaliyo ya dhati usiangalie kigezo kimoja tu, ni vyema kuzingatia mafanikio endelevu yajumuishayo kutimiza shauku au hitaji la moyo bila kutanguliza hofu kwanza na kubwa kuliko ni lile la kutimiza hitaji la kisaikolojia kama alivyoainisha Mwanasaikolojia Maslow- kutimiza mahitaji  ya ngazi ya chini ili kupelekea kupata mafanikio ya kweli yasiyo na mawaa.

Makala inayohusiana: The Truth About What It Means to Be Successful

Imetayarishwa na
Mwandishi wa Kitabu-Mtazamo Wako Ni Upi?
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza.

Jumanne, 10 Februari 2015

MTAZAMO: FANYA HIVI KUKOSOA WENGINE BILA KULETA UGOMVI…


“I like oppositions and criticism, the two make me behave better with perfection-Henry Kazula
____________________________________________________________
Picha:managing-employee-performance.com
Napenda kukukumbusha ndugu masomaji wa Blog hii kuhusu moja ya makala zetu iliyobeba kichwa Ujasiriamali: wanaokupinga, kukudharau, kukuwekea vikwazo na kukukejeli wanakujenga bila wewe na wao kujijua…kwa mantiki kuwa hatupaswi kuogopa kukoselewa kwa minajili kuwa tutakatishwa tamaa au kudharaulika kwa maamuzi, mawazo au ubunifu wetu.

Katika safu hii leo napenda tuangazie upande mwingine wa yule au wewe unayependa kukosoa wengine kwa namna isiyo na lengo la kuboresha ubora wa utendaji ila kuwakwaza na kuwakatisha tamaa wengine. Yawezekana unafanya ukosoaji huo kwa kujua unachofanya au kwa kutojua uzito wa maneno yako kwa mhusika. 
Kwa kuzingatia mtazamo wa kisaikolojia, Jielimishe Kwanza! Blog inakudadavulia kinaga ubaga njia za kipekee za kukosoa wengine bila ya kumkwaza mhusika, wakati huo huo uhusiano ukiimarika na mhusika kujihisi vizuri na kutafakari kwa kina maoni aliyopewa.
Tumefanikiwa kukuletea njia 5 za msingi kuzitumia ili kuwa na uwezo wa  kukosoa kwa tija (constructive criticism) bila kuwakwaza wengine na sisi kujiongezea heshima na uthamani katika maeneo ya kazi;
1.    ANZA KWA KUTUMIA LUGHA ILIYO CHANYA…
DaleCarnegie, mwandishi wa kitabu “How to win Friends & Influence People” anasisitiza mtazamo chanya hasa katika kukosoa wengine bila kuleta ugomvi ukizingatia kuwa watu wengi hawapendi kukosolewa na hujiona wakamilifu muda wote.
Chukulia mfano wa kimtazamo ufuatao: Ikiwa umegundua kosa la kiutendaji au ni mapungufu tu ya kiutendaji kutoka kwa mfanyakazi unaweza kumwambia; “ukiongeza jitihada kidogo katika utendaji kazi wako utakuwa bora zaidi na kuongeza sifa ya kampuni” …na si kumwambia; sifurahishwi kabisa na utendaji kazi wako, ukiendelea hivyo nitakufukuza kazi”....
Au, unaweza kuwakuta watu wakitupa taka taka katika eneo lisilo rasmi ilihali kuna bango linaloonyesha sehemu sahihi ya kuhifadhi taka taka na kuwaambia; tafadhali naona ni vyema kama mngehifadhi taka taka zenu katika chombo kilichoonyeshwa…badala ya kusema; ninyi vipi! hamuoni bango linaloonyesha sehemu sahihi ya kutupa uchafu wenu? 
 
2.    ZINGATIA LENGO KUU KWA KUJENGA HOJA
Ni vyema kufahamu na kuzingatia sababu kuu ya wewe kukosoa mawazo au utendaji kazi wa wengine.Kwa kuzingatia lengo kuu utaweza kujua kwa kina maeneo yenye uzito na uhitaji wa maboresho zaidi, hivyo kutoa maoni yako yenye kukosoa kwa lugha iliyo rafiki.
3.    FUATILIA KWA UKARIBU UTEKELEZAJI WA MAONI YAKO
Si jambo baya ukimuona mhusika moja kwa moja na kumueleza ushauri wako juu ya utendaji kazi au mawazo fulani.Pia ukimuuliza mara kwa mara juu ya utendeaji kazi au utekelezaji wa maoni yako.Mhusika atakuona una lengo zuri la kutaka afanikiwe katika utendaji kazi.
4.    TAFUTA MUDA MUAFAKA WA KUKOSOA/KUTOA MAONI YAKO
Inapendeza kutafuta muda na mahali sahihi kumueleza mtu kuhusu mapungufu yake ya kiutendaji au mawazo ya kibiashara na si kuropoka mbele za watu kuhusu mapungufu yake. Inakera sana na kukatisha tamaa mara tu mtu anapokukosoa mahali pasipo sahihi au muda usio sahihi, haijalishi ubora wa ushauri kutoka upande mwingine.

5.    SIMAMIA UKWELI, USIFANYE KISHABIKI!
Tunapotoa ukosoaji haimaanishi kufanya ushabiki ili upande unaokosolewa ushindwe kutimiza malengo yake na kukata tamaa, la hasha! Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa kunatokea maboresho chanya ya kiutendaji kutokana na ushauri au maoni yaliyotolewa.Ni vyema kuzingatia ukweli wa kila hoja ukizingatia lengo kuu la kuhamasisha utendaji na si kudhoofisha mawazo au utendaji kazi wa wengine.
Kuhusu kufanikiwa kuishi na watu vizuri na kuwahamasisha, Soma kitabu:
"How to Win Friends and Influence People" by Dale Carnegie.
Imetayarishwa na
Mwandishi wa Kitabu-Mtazamo Wako Ni Upi?
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza.