inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumanne, 24 Januari 2017

MTAZAMO: HAKI YA MWANAMKE KUMILIKI ARDHI- BARAZA LA WANAWAKE VIJIJINI (RWC) LATEKA HISIA ZA BARAZA KUU LA UMOJA WA AFRIKA (AUC)


Ikiwa ni siku chache kabla ya Mkutano mkuu Wa jinsia Wa Baraza kuu la Umoja wa Afrika (AUC) unaotarajiwa kuanza tarehe 22-25 Januari 2017 jijini Addis Ababa-Ethiopia, Shirika la “Action Aid Tanzania” kwa kushirikiana na Mtandao Wa Jinsia- “Tanzania Gender Networking Programme” (TGNP)-Mtandao wamekutana kwa pamoja kujadili mafanikio makubwa ya kuundwa kwa Baraza la Wanawake Vijijini-The Rural Women Council (RWC) lililoundwa mwaka 2012.


Moja ya mafanikio, na kubwa kuliko yote ni lile la Baraza la Wanawake Vijijini (RWC) kutambuliwa na  Baraza kuu la Umoja wa Afrika (AUC) hadi kufikia hatua ya kutoa mwaliko kwa Bi. Flora Mathias Mlowezi ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la hilo kwa Afrika Mashariki, pia ni mwanaharakati wa masuala ya Jinsia kutoka “TGNP’s Tigushe Knowledge Center in Mbeya rural district” ili kuwakilisha sauti za vilio vya wanawake wengi vijijini kuhusu Haki yao ya msingi kumiliki Ardhi nchini Tanzania na Afrika ya Mashariki kwa ujumla.

  
Picha: Bi. Flora Mathias Mlowezi: Mwenyekiti-Baraza Afrika ya Mashariki na
Mwanaharakati- “TGNP’s Tigushe Knowledge Center in Mbeya rural district" kutoka Tanzania.

Licha ya kutetea maslahi za wanawake wengi waliopo vijijini katika haki yao ya kumiliki Ardhi; Bi Flora anakuwa ni miongoni mwa wanawake shupavu walioweza kushiriki Kampeni maalumu ya kupanda mlima mrefu Afrika-Kilimanjaro kupitia kampeni “Kilimanjaro Initiative” iliyoasisiwa na 

Baraza la Wanawake Vijijini-The Rural Women Council (RWC) mnamo Octoba 2016 chini ya uangalizi wa TGNP-Mtandao wa Jinsia na Action Aid Tanzania jijini Arusha-Tanzania.


Kupitia mkutano mdogo wa wadau wa kutetea masuala ya haki ya mwanamke kumiliki Ardhi kutoka TGNP- Mtandao wa Jinsia na Action Aid Tanzania uliofanyika jijini Dar es salaam tarehe 21/01/2017, washiriki walilenga kumjengea uwezo na kumpa ujasiri Bi.Flora ili kuwa na uelewa wa kutosha katika kuwawakilisha wanawake wote wa vijijini nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla wake.


Picha: Wajumbe katika Mkutano mdogo wafuatilia jambo kutoka kwa Mwenyekiti wa kikao.
  
Suala la msingi linalomfanya Bi.Flora kwenda kuwakilisha sauti za wanawake wengine kuhusu haki ya kumiliki Ardhi, ni lile la kutoa ufafanuzi wa kina wa tamko la madai ya wanawake wote wa vijijini lililowasilishwa Octoba 2016 kwa Mwenyekiti wa AUC. Hivyo, itakuwa na wasaa mzuri kwa jitihada hizo za Wanawake waishio vijijini kuweza kusikilizwa katika masikio ya viongozi, watunga sera na wasimamiaji sera kutoka mataifa mbali mbali barani Afrika na jumuiya nyingine za Kimataifa.

 
Picha: Mwenyekiti wa kikao akiwasilisha Tamko la Madai lililotokana na Kilimanjaro Initiative ya Octoba 2016.

Dhana ya kutoa kipaumbele kwa wanawake waishio vijijini ilikuja kutokana na kuwepo kwa 70% ya wanawake wanaoishi vijijini ukilinganisha na mjini, pia idadi hiyo kubwa inawahusisha wanawake walio wengi wanaotegemea Ardhi kama rasilimali ya kuendesha maisha yao ya kila siku kama vile kilimo na ufugaji.

Imetolewa na Jielimishe Kwanza kwa niaba ya Action Aid Tanzania jijini Dar es salaam.