K
|
wa
miaka mingi tangu kuingia kwa Mashirika yasiyo ya Kiserikali ( Kwa lugha ya Kiingereza kama Non
Governmental Organizations-NGOs )katika nchi mbali mbali hususani Tanzania
yamekuwa yakitegemea fedha za kuendesha miradi ya kijamii kutoka kwa wafadhili.
Mashirika
hayo yasiyo ya Kiserikali yamekuwa yakishirikiana na Serikali bega kwa bega
katika kutatua changamoto mbali mbali za kijamii.
Mafungu
hayo ya fedha kutoka kwa wafadhili yamekuwa na masharti yaliyo sanjali na
kuhakikisha miradi inakuwa na tija kwa jamii kama ilivyokusudiwa.
Ingawaje
baadhi wadau wengine katika Mashirika hayo wamekuwa wakitumia ujanja ujanja
kujineemesha na fedha hizo za wafadhili.Hili limepelekea wafadhili wengi
kujing’atua kutoa misaada na kuyaacha Mashirika hayo yasiyo ya Kiserikali
solemba, yakiwa na kiu za kutimiza miradi mbali mbali.
Ujasiriamali jamii- “Social Enterpreneurship”…Njia
mbadala ya kuepuka utegemezi
na kuleta tija ya
moja kwa moja kwa jamii!
Picha na sagescholars.berkeley.edu |
Ujasiriamali jamii-
“Social Enterpreneurship”-
Tunatambua tatizo kwa pamoja, tunatumia kanuni na mbinu za kitaalamu mfano: kanuni za biashara kuleta badiliko kubwa katika jamii kama tulivyokusudia, lenye faida kwa jamii nzima na si kwa mtu mmoja...wakati huo huo Shirika letu la Kijamii likikua na likijiendesha lenyewe siku hadi siku!
_______________________________________________________________________________________________________________
_______________________________________________________________________________________________________________
Soma undani na umuhimu wa Ujasiriamali jamii -“Social Enterpreneurship” kupitia http://www.caseatduke.org/documents/dees_sedef.pdf
Imetolewa na
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni