inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumapili, 1 Mei 2016

MAZINGIRA: KAMPENI YA KIJAMII NA MAZINGIRA ”Save Life. Save Water ecology” –“Okoa Maisha.Okoa Ikolojia- Maji” YAZINDULIWA DAR ES SALAAM


Founder & Executive Director:
Jielimishe Kwanza Co.Ltd,
+255 754 572 143
_________________________________________________________________________________ 


Kampeni ”Save Life. Save Water ecology” –“Okoa Maisha.Okoa Ikolojia- Maji” ni ya kwanza na ya kipekee kuzinduliwa nchini Tanzania chini ya udhamini wa kampuni “Jielimishe Kwanza” na “Jielimishe Kwanza Blog” katika miradi yao endelevu: “Environmental Activists in Tanzania”, “Enviro-Forum” na “Social & Environmental Entrepreneurship in Tanzania (SEE-Tanzania).

Mr.Henry Kazula, akifafanua kuhusu "Save Life.Save Water ecology"campaign-Tanzania. Picha:Blogs za Mikoa).

Pia, kampeni hi iliweza kushirikisha kwa ukaribu Dawati la Vijana-UNESCO UNESCO-Youth Desk-Tanzania” na mashirikishika mengine yasiyo ya Kiserikali yajihusishayo na Utunzaji na Usimamizi wa Mazingira kama Comprehensive Environmental Management Organization (CEMO), “Young Lawyers Foundation” na Jane Goodall’s Roots&Shoots”

”Save Life. Save Water ecology” -“Okoa Maisha.Okoa Ikolojia Maji” imekuja mahsusi kutokana na kuwepo kwa athari za mabadiliko ya tabianchi (mfano: mafuriko) pia uvamizi wa maeneo yaliyo kando kando ya vyanzo vya maji kwa shughuli za kibinadamu ambazo huathiri/huchafua ikolojia-Maji na kuhatarisha maisha ya viumbe walio majini pia kuyafanya maji yasiwe salama kwa matumizi ya Kibinadamu.

Kampeni hii endelevu nchini Tanzania imelenga kutoa hamasa kwa jamii kupitia warsha za vyuo vikuu kama “Sauti ya Vijana”, Radio na Televisheni katika  kuleta mwamko chanya wa kuhifadhi vyanzo vya maji na kuutaadharisha umma kuhusu madhara na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi kwa kuishi maeneo hatarishi-hasa mabondeni, katika fukwe za Bahari, Maziwa na Mito.Kauli mbiu yake ikiwa; “Usiishi mabondeni,katika Fukwe za Bahari,Maziwa na Mito”-Stay out of Valleys,Ocean,Lake and River shorelines”. Pia, imelenga kushirikiana na jamii  katika kuhifadhi na kutunza vyanzo vya maji kwa kupanda miti, kusafisha fukwe za bahari,maziwa na mito.

Hivyo, kupitia Sheria ya mazingira(2004) inayosimamiwa na Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Sheria ya Ardhi Sura 113, kampeni hii imedhamilia kwa dhati kutoa hamasa, ufahamu, ufafanuzi na taadhari kwa umma kujiepusha kuishi katika “maeneo ya mazingira nyeti” kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Mazingira(2004),sura 191(kif.51) na maeneo hatarishi katika Sheria ya Ardhi sura 113(6 na 7).Pia kutoa ufafanuzi juu ya umbali halisi wa kufanya shughuli za kibinadamu kutoka kwenye kingo za bahari, maziwa na mito kwa kuzingatia EMA,2004 51(1)na (2) ili kuhifadhi vyanzo vya maji kwa maslahi ya kuokoa maisha  ya binadamu kutokana mafuriko, kuokoa rasilimali fedha, na kujali maslahi ya utunzaji Mazingira kwa maendeleo endelevu (Sustainable development).

Shughuli nzima ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es salaam tarehe 29-30 Aprili 2016 iliwajumuisha washiriki ambao ni Wanaharakati wa Mazingira na Maafisa Mazingira kutoka Miji mikubwa- Dar es salaam,Mbeya,Arusha, Mwanza na Tanga; ambayo Kampeni hii imelenga kuendelea na uhamasishaji; lengo kubwa likiwa ni kufikisha ujumbe huu mahsusi kwa watanzania wote kwa maslahi ya Kijamii,Kimazingira na Kiuchumi hatimaye Taifa letu liweze kuyafikia malengo endelevu kwa kuchangia juhudi za Umoja wa Mataifa za Malengo 17 ya Maendeleo endelevu(17 SDGs ,2030).

Wanaharakati  wa Mazingira na washirikiri wa Uzinduzi wa Kampeni-"Save Life.Save Water ecology"  kutoka "Jielimishe Kwanza", Mashirika yasiyo ya kiserikali na Maafisa wa Mazingira kutoka Serikalini (Picha: Blogs za Mikoa)
_____________________________________________________

Washiriki walijumuika kujifunza na kubadilishana mawazo juu ya Sheria ya Mazingira 2004-utekelezaji na changamoto zake.Pia kutoa mapendekezo yatakayowasilishwa katika Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa Mazingira(NEMC).

Kampeni hii iliweza kutoa na kuboresha ufahamu na ushirikiri wa jamii katika kutekeleza malengo ya Maendeleo endelevu yaliyo sanjari na uhifadhi wa vyanzo maji na kuokoa maisha ya watu na viumbe waishio majini.Mmbadala wa ujarisimali jamii na ule wa Mazingira (Social & Environmental Entrepreneurship) kama “Ecotourism” ulipewa kipaumbele katika kupambana na uhifadhi wa vyanzo vya maji wakati huo huo jamii husika ikiboresha uchumi na maisha.

Siku ya pili ya shughuli ya uzinduzi wa kampeni hii; washiriki, kwa kuonyesha nia ya dhati ya kujifunza na kujionea uhalisia wa shughuli za binadamu katika uchafuzi wa mito na bahari, waliweza kutembelea Mto Mbezi. Ilionekana kuwa shughuli za uchimbaji mchanga, ujenzi kando kando ya mto kuchangia kubomoka kwa kingo za mto, utupaji wa taka ngumu(mto kutumika kama dampo) na utiririshwaji wa maji taka kutoka nyumba zilizo jirani ya mto.

Hatimaye washiriki walipatiwa vyeti vya ushiriki na kuwa mabalozi wa Kampeni hii katika mikoa mingine: Mbeya, Arusha, Mwanza na Tanga.

Ratiba ijayo:
Arusha-Agosti 2016
Mwanza-Octoba 2016
Tanga-December 2016.


Matukio katika picha: Mto Mbezi, Dar es salaam







Imetolewa na 
Jielimishe Kwanza Blog


"Kampeni hii ni endelevu, inahitaji msaada wa kifedha na ushiriki wa mashirika mengine zaidi.Unakaribishwa sana kuchangia au kujiunga nasi"


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni