inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumatano, 22 Oktoba 2014

BIASHARA: HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUJENGA THAMANI YA UBORA KATIKA SOKO

-->

Ikiwa wewe ni mfuatiliaji wa makala zetu kuhusu biashara utaona kuwa tunasisitiza sana kuhusu kuboresha thamani ya ubora wa bidhaa ili kuliteka soko na pia kumshinda mpinzani wako katika kugombea soko.Soma zaidi




Sanjari na mtazamo thabiti wa kiuchumi kuwa; watu hulipwa kwa kupeleka thamani ya ubora kwenye soko ni dhahiri kabisa kuwa mtu hawezi kupata kipato halali pasipo kuleta thamani ya ubora katika soko.Katika lugha ya kiuchumi, soko ni watu.Hivyo, hakuna kipato halali kinachoweza kupatikana katika biashara yako kama huleti thamani ya ubora kwa watu; kutoa suluhisho la maumivu ya watu kwa maisha yao ya kila siku.
Kama ilivyo ada, wajasiriamali na wafanyabiashara hupaswa kutoa suluhisho la matatizo ya watu.Kuna kanuni (10) za msingi zinazopaswa kufuatwa kufikia kuleta suluhisho la matatizo pia kufikia lengo kuu na kujipatia kipato endelevu.Kanuni hizo ni;
1.    CHUNGUZA KWA MAKINI HUDUMA/BIDHAA ILIYOPO KABLA YA KULETA YAKO
2.    BORESHA MAPUNGUFU YA WENGINE, UPATE SEHEMU YA KUSIMAMIA
3. JIDHATITI KWA KUJITOFAUTISHA NA WAFANYABIASHARA WALIOPO UKIBORESHA UBORA ZAIDI
4.    HAKIKISHA HUTOI SIRI YA KUFANIKIWA KWAKO KATIKA SOKO
5.    JITENGENEZEE UPEKEE WA THAMANI YA UBORA KATIKA SOKO
6.    TENGENEZA WIGO WA SOKO LAKO NA USIMAMIE MSIMAMO WAKO
7.    WAKATI WOTE ANZA KUFIKIRIA KUHUSU WATEJA WAKO; WANAHITAJI NINI KWA WAKATI HUSIKA? NA SI UTAPATA NINI KWANZA KWA WAKATI HUSIKA:
8.    TENGENEZA MAHUSIANO MEMA NA WATEJA WAKO…ZINGATIA UHITAJI WAO
9.    FANYIA KAZI MAONI YA WATEJA WAKO KATIKA KUBORESHA UTHAMANI WA BIDHAA
10. HATA SIKU MOJA USISHUSHE BEI ZAIDI YA MPINZANI WAKO ILI UWAVUTE WATEJA KWAKO.
Tunakutakia kila la heri katika biashara yako.Ikiwa utahitaji ufafanuzi wa mbinu hizi (10), usisite kuwasiliana nasi:+255 754 572 143
             Imetolewa na

                                 Jielimishe Kwanza! SE

Jumanne, 21 Oktoba 2014

MTAZAMO: HIVI UNAJUAJE KAMA KILA KITU UNACHOAMBIWA NA KUTAZAMA NI KWELI?


Picha:http://lifeinzd.com/why-telling-the-truth-sucks-and-why-its-awesome-a-case-study/
Umewahi kujiuliza kama mambo uyaonayo na kuyasikia ni kweli? Kila siku tunaona na kusikia wengine wakitueleza masula mbali mbali kutuhusu au kuwahusu wao na kukurupuka katika kuyafanyia kazi bila kufanya utafiti wa kina.Soma hii pia. 
Lakini, ni mara ngapi tumejiuliza kama masuala hayo ni kweli kabla ya kuchukua hatua za makusudi za utekelezaji? Pia, ni nini hutuaminisha kuwa mambo hayo ni kweli? Au unajuaje kama makala hii ninayokuandikia uisome sasa ni kweli?
Kupitia maswali hayo ya msingi ni vyema nikakushirikisha mtazamo wenye msaada wa karibu kutoka kwa Wabuddha;
“Believe nothing. No matter where you read it, or who said it, even if I have said it, unless it agrees with your own reason and your own common sense.” …kwa tafsiri isiyo rasmi inamaanisha kuwa- “Usiamini chochote. Bila kujali umesoma mahali au kupitia mtu fulani na hata kama nimesema, isipokuwa tu kinaendana/kinashabihiana na upeo wako wa kufikiri na akili yako ya kawaida katika kutoa maamuzi". Msisitizo umewekwa kwenye upeo wa kufikiri na uwezo wa kawaida katika kutoa maaamuzi.
Je, unafanyaje kuboresha au kunoa upeo wako wa kufikiri na uwezo wako katika kutoa maamuzi sahihi kwa wakati husika? Kupitia makala zetu kuhusu mtazamo utaona kuwa tunasisitiza kuhusu Kujielimisha Kwanza! hii ikiwa ni njia pekee ya kujua ukweli wa mambo kama Mwl.J.K.Nyerere alivyoanisha katika kijitabu chake cha TUJISAHIHISHE.Kuelekea kujua ukweli wa mambo tunaboresha na kunoa upeo wetu wa kufikiri na ufahamu katika kutoa maamuzi sahihi na yenye tija.
Sioni haja ya kuficha au kuzunguka sana, la msingi ni kusoma mambo mengi kupitia vitabu,majarida yenye tija na kusikiliza hotuba mbali mbali sambamba na kulinganisha mawazo ya watu tofauti, changanya na uwezo wako wa kupambanua mambo kuhusu uhalisia wa jambo fulani katika maisha, mwisho kuweza kutofautisha mchele na pumba.
Pia jifunze jinsi ya kuunganisha matukio tofauti tofauti ili kukufikisha katika jambo au suala unalotaka kujua undani wake.Kupitia njia hizi unaweza kuwa mpelelezi wa kuijua kweli iliyo suluhisho la kututoa njia panda, na mwisho wa yote unaweza kutumia uzoefu huu kutatua matatizo mbali mbali ndani ya jamii.
Usikubali kudanganywa!... kwa maana anayekudanganya hukuchukulia wewe kama mtu usiyeweza kutumia upeo wake vizuri katika kupambanua mambo.Hivyo usije naswa katika mtego wa kudanganywa...tumia njia tajwa kufuatilia na kuujua ukweli wa mambo.
Kuna faida kem kem za kujijengea tabia ya kupeleleza na kujua ukweli kuhusu jambo au mambo fulani, kuanisha chache;
1.KUEPUKA MIGOGORO ISIYO YA LAZIMA
2.KUTATUA MATATIZO KIRAHISI BILA UPENDELEO WA UPANDE FULANI
3.KUJIONGEZEA WIGO WA KUFAHAMU MAMBO MENGI YENYE TIJA KWA MAISHA YETU
4.HUTUPELEKEA KUWA NA MTAZAMO CHANYA WA MAISHA NA KUWAJUA WENGINE KIUNDANI BILA KULETA UGOMVI
5.KUWA NA UHURU WA NAFSI ISIYO NA MAWAA
6.KUWA NA FURAHA ILIYO MUHIMU KWA AFYA
7.KUEPUKA MSONGO WA MAWAZO USABABISHWAO NA KUTOFAHAMU UNDANI WA JAMBO FULANI
8.KUONDOKANA NA ADUI WA MAENDELEO- UJINGA
9. KUJITOA KATIKA UELEWA WA NJIA PANDA.

Jielimishe Kwanza! Jifunze na utafute kuijua kweli itakuweka huru!
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza! SE

Jumanne, 29 Julai 2014

MTAZAMO: TUKIBADILI MTAZAMO TUNAWEZA KULETA MABADILIKO…

Nakuletea makala hii fupi ikiwa ni sehemu tu ya yale yaliyojili siku ya wiki ya maadhimisho ya kuzaliwa shujaa wa Afrika-Nelson Mandela “Madiba” kuanzia Julai,12-18,2014 katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia-Tengeru,Arusha.

Kwa wiki nzima kulikuwepo na maonyesho ya ubunifu wa Kisayansi na elimu za hadhara zikijumuisha wataalam mbali mbali wa Sayansi na Teknolojia kutoka vyuo vya hapa nchini na nje ya nchi.

Nikiwa mwanachuo, nilitembea mabanda mbali mbali ya kibunifu.Nilivutika na ubunifu wa mtaalamu, mjasiriamali Bw. Justin Mungure wa Makumira, Arusha kwa ubunifu wake wa kuibadilisha TOYO ya magurudumu matatu maarufu kwa kubeba mizigo kuwa ya magurudumu manne muonekano kama ule wa gari.
Picha:Muonekano wa pikipiki aina ya TOYO ya magurudumu matatu.




Niliweza kumhoji mtaalamu, ilikuwaje kufikia ubunifu wake? Alijibu; “mara nyingi nimeona TOYO za magurudumu matatu zikianguka kwa kukosa nguvu ya mbele ya gurudumu moja…hivyo nikaamua kuiboresha zaidi kwa kuifanya iwe na magurudumu mawili sawa na nyuma…na sijabadilisha mfumo mwingine wa mashine…”




Picha:TOYO ya magurudumu manne-Ubunifu wa Justin Mungure.

Mungure anifanya kazi hiyo katika karakana yake iliyopo eneo la Makumira-Jijini Arusha.Hubadilisha TOYO ya magurudumu matatu kwa gharama ya takribani shilingi milioni moja na nusu za kitanzania(1,500,000/=) licha ya gharama ya kununua TOYO mpya.
Picha:Justin Mungure akiwa kwenye TOYO yake.

Nilihamasika sana na ubunifu wake ndiyo maana nimependa kukushirikisha ndugu msomaji kuwa tunaweza kubadili mtazamo wa kufikiri na kuamini katika masuala mengi katika maisha yetu ikiwemo jinsi ya muonekano wa vitu mbali mbali na hata yale yahusuyo Teknolojia kwa lengo la
--> kwa lengo la kuboresha ubora na ufanisi.Tunahamasishwa kuwa na mtazamo tofauti wa kufikiri na si kutegemea mtazamo wetu tuliouzoea kila siku na kutegemea matokeo tofauti katika maisha yetu ya kila siku.

Imetayarishwa na kutolewa na 
Jielimishe Kwanza! Social Enterprise. 

Jumatano, 25 Juni 2014

MAZINGIRA: CHANZO CHA MABADILIKO YA TABIANCHI...

Toleo jipya:
 



Na Henry Kazula,
Mtaalamu wa Sayansi ya Mazingira,
"Nelson Mandela African Institution of Science and Technology, Arusha-Tanzania"
Mwandishi, Msemaji wa hadhara na mhamasishaji wa mabadiliko
__________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________
Photo:http://www.eecuk.co.uk/energy-efficiency-climate-change-and-the-city-of-london/
Kutokana na taarifa ya jopo la wataalam wa mabadiliko ya tabianchi duniani-“Intergovernmental Panel on Climate Change (IPCC)” wanasema kuwa, mabadiliko ya hali hewa husemekana kuwa ni hali yoyote inayopelekea kubadilika kwa tabianchi na ya dunia kwa ujumla wake, hii ni kutokana na visababishi asilia ukijumisha shughuli  mbali mbali za binadamu.
Mabadiliko ya tabianchi na dunia kwa ujumla hujumisha viashiria kama kuongezeka kwa joto duniani (...husababisha kuyeyuka kwa barafu), kuongezeka kwa kina cha bahari (huatarisha kutoweka kwa visiwa mbali mbali duniani),ukame na mvua zisizokuwa na utaratibu,mafuriko.
Kuna madhara* mbali mbali yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi-hasa kwa binadamu ambaye ni mchangiaji wa mabadiliko hayo;
·      *Upungufu wa mvua na mafuriko husababisha tatizo la upatikanaji wa chakula-hivyo gharama za chakula kuongezeka
·      *Kuibuka kwa magonjwa -mfano kuongezeka kwa joto kumepekea kuenea kwa ugonjwa wa Malaria kwenye maeneo yaliyokuwa na baridi na hayakuwa na ugonjwa huo hapo awali
·      *Kuteteresha uchumi wa Nchi- hasa kutokeapo majanga yasababishwayo na mabadiliko ya hali ya hewa, mfano: mafuriko huaribu miundo mbinu ya nchi iliyo muhimu kwa kukuza uchumi, pia fedha za maendeleo hutumika katika majanga kusaidia wahanga
·      *Kupotea kwa viumbe kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa katika sehemu husika
* Nchi masikini na zinazoendelea zipo kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi.
Kwa kipindi kirefu kumekuwa na marumbano ya hapa na pale kuhusu chanzo cha mabadiliko ya tabianchi, binadamu amekuwa akinyooshewa kidole kuwa ni chanzo kikubwa cha mabadiliko hayo kutokana na shughuli mbali mbali za kijamii na kiuchumi.
Takwimu za kihistoria zinaeleza kuwa kwa kipindi cha miaka elfu kumi iliyopita hali ya hewa na tabianchi haikuwa na mabadiliko yoyote, ikimaanisha kuwa ilikuwa kawaida, ingawaje kuanzia hapo hali ya tabia/hewa imekuwa ikipitia mabadiliko ya hapa na pale.”Swali linakuja, nani amechangia mabadiliko hayo hadi sasa?” kama nilivyoeleza awali, kuna visababishi asilia na shughuli za binadamu.
Kuna kila sababu kuwa shughuli za binadamu zimechangia kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko hayo na haya tunayoyaona.Ondea mbali visababishi asilia ambavyo naweza kusema vilikuwepo tangu kuwepo kwa dunia.
Binadamu ameingilia kwa kiasi kikubwa mfumo wa hali ya hewa ujumuishao; anga la hewa, maji (bahari na vyanzo vyake),barafu,ardhi na eneo la viumbe uhai.
Ingawaje mfumo wa hali ya hewa huendeshwa pia na visababishi asilia kama vile mripuko wa volcano, kubadilika kwa miozi ya jua ifikiayo uso wa dunia, muingiliano wa bahari na anga la hewa, mikondo ya bahari iletayo baridi na joto nchi kavu na kubadilika kwa mizunguko ya dunia katika kulizunguka jua kutokana na kani mvutano iliyopo kati yake na mwezi na sayari nyingine.
Shughuli mbali mbali za binadamu zilizo sanjari na uvumbuzi na kukua kwa viwanda duniani kumepelekea kuongezeka kwa joto kama inavyoripotiwa na wataalamu wa masuala ya hali hewa duniani-IPCC.
Ongezeko la joto duniani la Sentigredi 2 kwa karne hii ya 21 limeifanya dunia kuwa katika vipindi hatarishi viambanavyo na majanga mbali mbali.Ongezeko hilo linalosemekana kusababishwa na ongezeko la takribani 400ppm la hewa ukaa-kabonidioxide gesi (CO2) inayokumbatia joto la dunia mara tu gesi hii ichukuapo joto kutoka kwenye mionzi ya jua hivyo kufanya joto kuzidi kubaki katika uso wa dunia.Inakadiriwa kuwa hewa hiyo itaongezeka kufikia 550ppm (mara mbili zaidi kabla ya mapinduzi ya viwanda) na kupelekea ongezeko la joto duniani la Sentigredi 3 kufikia 2050. Ongezeko hii ni la hatari kama juhudi za makusudi na za pamoja hazitachukuliwa kupunguza hewa ukaa.
Mtu aweza kuuliza, nini hupelekea kuongezeka kwa hewa ukaa? Jibu ni rahisi sana ndugu msomaji: shughuli za binadamu kama uzalishwaji wa nishati kupitia makaa ya mawe, uchomaji misitu, kubadilisha uoto wa asili kuwa makazi na viawanda, ukataji miti, shughuli za viwanda, vyombo vya usafiri kwa kuunguza mafuta n.k.Ukiangalia kwa makini utaona kuwa shughuli za kuinua uchumi zinachangia kwa kiasi kikubwa kwa mabadiliko ya tabia ya nchi.Hii ndiyo sababu mataifa makubwa yaliyojiimarisha kiuchumi yanakwepa kuchangia juhudi za kupunguza ongezeko la hewa ukaa duniani na kuhamasisha nchi masikini na zinazoendelea kuwa mstari wa mbele kupunguza ongezeko la hewa ukaa.
Ndugu msomaji, unaweza kufikiri kuwa uchafuzi wa hali ya hewa na mazingira katika sehemu nyingine duniani hauleti madhara kwa Taifa lako…madhara yapo, tena ni makubwa kwa sababu hewa ipo katika mzunguko na hubeba hewa mbaya kutoka eneo moja hadi lingine.Hivyo, hatuwezi kujitenga katika juhudi za kumbana na kupunguza hewa ukaa. 
Kila Taifa lina wajibu wa kupambana kudhibiti ongezeko la hewa ukaa kabla ya hali ya hatari haijatufikia...naweka msisitizo kwa mataifa makubwa yaliyojiimarisha kiuchumi kutokana na viwanda kuwa mstari wa mbele kupunguza ongezeko la hewa ukaa na si kutoa misaada kwa nchi masikini kupambana na tatizo wakati nchi hizo kubwa zikiendelea kufanya uchafuzi bila kuchukua hatua madhubuti za kupunguza tatizo.
Bila shaka ,kwa kiasi chake umeona ni jinsi gani binadamu anavyochangia mabadiliko ya tabianchi.
Tukutane wakati mwingine katika ukurasa huu ujue zaidi kuhusu “mbinu za pamoja kupunguza hewa ukaa na gesi nyingine zinazochafua anga”
"Mabadiliko huanza na mimi na wewe"
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza! 
Rejea:
Burroughs,W.J.(2007). Climate Change.A multidisciplinary Approach.2nd edition. United Kingdom:University Press,Cambridge.
IPCC,(2007).Climate Change 2007:Scientific Basis,Cambridge,UK:Cambridge University Press.


Jumapili, 18 Mei 2014

AJIRA NA KAZI: MUZIKI UNAPOHAMASISHA KUJIAJILI


-->
M
ara nyingi hupendelea kusoma magazeti ya ndani na nje ya Tanzania.Pia nasoma vitabu tofauti tofauti vyenye kuchochea mtazamo a chanya.

Mazoea haya huniwezesha “kujua ukweli wa mambo” unaoendelea katika jamii na maisha kwa ujumla, pia kuandika makala mbali mbali ndani ya Jielimishe Kwanza!… hii ikiwa ni dhana kubwa ya Jielimishe Kwanza! 

Hii haina madhara yoyote katika masuala yangu ya shule...najua! wenzangu na mimi wanaosomea shahada ya Uzamili-"Master's" hujikita zaidi kwenye kusoma mambo yanayoendana na masomo ya darasani tu! Nashauri, Wakati mwingine ni vizuri kusoma mambo yahusuyo jamii moja kwa moja na maisha kwa ujumla wake.


Leo, Jumapili, Mei, 18 2014  saa 24:0 AM nimekutana na gazeti la Tanzania liitwalo Mwananchi lenye kauli mbiu "Fikiri Tofauti" ...hakika kuna makala napenda nikushirikishe kuhusu suala zima la msomi wa Chuo kikuu kupenda/kutegemea/kutarajia kuajiriwa.


Mwandishi, Herieth Makwetta, wa gazeti hilo Kanihamasisha! Kukuhamasisha! kubadili mtazamo, hasa alipoandika makala kutokana na mahojiano ya msanii wa Hip Hop kutoka Kundi la Weusi, Nickson Simon almaarufu kama "Nikki wa II" mwenye shahada ya Uzamili katika maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDMS).

Ama kwa hakika, "Nikki wa II" ni mfano wa kuigwa kwa vijana wasomi wenye shahada nchini Tanzania. Ukiwa msomi wa Sekondari au chuo kikuu nakushauri sikiliza kwa makini wimbo wake mpya ujulikanao kwa jina la   “Sitaki Kazi” utakubaliana nami.

Naomba ufanyie kazi sehemu ya mashairi ndani ya wimbo wake, anasema; 
"Sitafuti kazi ila nataka nitafutwe na watu wanaotafuta kazi"
 Pia, anasisitiza kutokuwa mtumwa wa kazi sanjali na moja ya makala zetu kama; athari za kufanya kazi katika mazingira ya utumwa wa kisasa na  kufanya kazi unayoipenda.


Naomba nisiendelee kuandika zaidi, ili uweze kupata muda wa kusoma kwa haraka na kutafakari yaliyomo ndani ya wimbo huo.Nakutakia utendaji kazi mwema, najua tena siku ya Jumatatu!
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!



Jumapili, 4 Mei 2014

MTAZAMO: USITOE MAAMUZI HASI BILA KUFANYA UTAFITI WA KUTOSHA…

-->
 
Napenda kuanza kwa kuwapongeza wafanyakazi wote hasa kwa kuzingatia Mei mosi ilikuwa ni siku ya kilele cha sherehe ya Wafanyakazi.

Photo:http://www.mentoringminds.com/socratic
Nianze kwa kuuliza maswali; ni mara ngapi tumekuwa tukiwafikiria na kuwatendea wengine visivyo(hasi) na baadaye tunagundua kuwa haikuwa kama tulivyokuwa tunafikiria? Je,unajisikiaje katika hali hii ya kuujua ukweli? Bila shaka, hakuna anayeweza kupinga ukweli huu kuwa binadamu tunaamini sana hisia zetu na kujitengenezea majibu mepesi kwa maswali magumu kuliko kuamini akili zetu.
Sina maana kuwa hatutumii akili zetu,ila mara nyingine tunakuwa wavivu kidogo katika kutoa maamuzi sahihi, na hii ni kwa sababu hisia zetu huchukua nafasi kubwa katika mazingira fulani…majibu yatokanayo na hisia hayaumizi kichwa wala kuuchosha ubongo na ni ya haraka.
Mungu katupatia akili ili tufikiri kwa makini, kupambanua na “kujua ukweli wa mambo” kama Mwl.J.K.Nyerere alivyoandika katika kitabu cha TUJISAHIHISHE kuwa Kujielimisha Kwanza ni kujua ukweli wa mambo, huwezi kujua ukweli wa mambo kwa kuendeshwa na hisia.
Nikuhakikishie ndugu msomaji kuwa, hakuna kitu kibaya kama ukamfikiria ndugu au rafiki yako kimtazamo hasi na akatambua jinsi unavyomchukulia tofauti na alivyo kiasili.Itakupa shida sana hapo baadaye ukibaini ukweli wa mambo.Ikiwa unataka kujua ukweli wa mambo unapaswa pia kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kutoa maamuzi hasi. Soma
Hatupaswi kukurupuka na kujiwekea majibu ya kihisia…mfano: eti naona ndugu yangu hanichangamkii tena, nafikiri ameona sina kipato. Pia kutoa suluhisho la kupotelewa  pesa kisha kumshuku mtu fulani kaiba na unaanza kumvamia kwa maneno hata ngumi, baadaye kidogo unakumbuka kuwa kuna kitu ulinunua na mahesabu yako sawa…utajisikiaje katika hali hii?
Kuna madhara makubwa ya kutoa maamuzi hasi bila kuwa na utafiti wa kutosha.Nimejaribu kugusia kidogo baadhi ya madhara hayo hasa kuvunjika kwa uhusiano kwa kirafiki, hii inamwonyesha mwingine hali ya kutokuaminiana katika urafiki.
Ikiwa utahitaji kujua madhara mengine ya Kisaikolojia ya kutoa maamuzi hasi bila ya kufanya utafiti, tuwasiliane +255 754 572 143.
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!

Jumatano, 2 Aprili 2014

MAZINGIRA: NI JUKUMU LA NANI KUTUNZA USAFI WA MAZINGIRA?

Nimekuwa nikitafakari kwa kipindi kirefu kwa kutazama mtazamo na uelewa wa jamii  kuhusu usafi wa mazingira na kinachofanyika baada ya uchafuzi wa mazingira kutokea, nikajiuliza swali hili “nani mwenye jukumu la kutunza usafi wa mazingira?” bila shaka ukiwa mdau wa usafi wa mazingira, utajiuliza swali hili.Ikiwa hufahamu umuhimu wa usafi wa mazingira, utajua ni nani anahusika kutunza usafi wa mazingira ukiendelea kusoma makala hii.
Ili kuweka bayana suala hili la usafi wa mazingira, ni vyema tukajulishana au kukumbushana maana halisi ya neno “mazingira” …kwa uelewa wa kawaida, mazingira ni mjumuisho wa mambo yote yanayomzunguka binadamu, ukijumuisha mimea, wanyama na viumbe visivyo hai.Kwa lugha nyepesi, mazingira humtunza mwanadamu ukijumuisha mimea na wanyama.Hivyo, binadamu hupaswa kutunza na kuhifadhi mazingira  ili yamtunze, yatunze pia viumbe vingine vilivyo hali.
Binadamu anatajwa kuwa mstari wa mbele katika kutunza mazingira kwa sababu ana utashi wa kujua mema na mabaya.Pia ndiye wa kwanza kuanzisha shughuli mbali mbali za kibiashara na kiuchumi katika mazingira yanayomtunza.Ikiwa sanjali na shughuli hizo, mwanadamu ana jukumu la kuhakikisha mazingira anayoishi hayaathiriwi na shughuli zake kwa hali moja au nyingine.
Nimezungumza kwa mapana sana, sasa niguse wahusika moja kwa moja.Kutokana na mgawanyiko wa majukumu ya kila siku,tofauti za hali kiuchumi, na fursa ya kuwepo kwa teknolojia ya viwanda kumetokea matabaka katika jukumu letu sote la kutunza usafi wa mazingira.
Baadhi ya watu wamejitenga kabisa na jukumu hili muhimu kwa afya zao na za wengine kwa kusimamia maslahi pekee.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nisipothamini juhudi za watu wachache katika kuzingatia jukumu la ubinadamu la kutunza usafi wa mazingira.Mfano: vikundi vya kijamii, serikali kwa sehemu yake, Mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi.
Leo nitoe mfano wa shughuli zifanywazo na Shirika lisilo la Kiserikali “VoiceGiving” katika kusimamia usafi wa mazingira na kutoa elimu ya usafi wa mazingira jijini Dar es salaam-Tanzania. Shirika hili limenihamasisha sana kuhamasisha wengine kuhusu kuheshimu na kutunza mazingira yetu.
Picha na Voice Giving. Baadhi ya vijana wa Shirika la "Voice Giving" VG wakiwa kazini katika kituo cha basi jijini Dar es salaam.
Wanatumia njia shirikishi kuwahamasisha watu na kuwakumbusha jukumu lao la asili la kutunza usafi wa mazingira.Wameanza utekelezaji wa adhma yao kwa kuanza na mazingira ya vituo vya basi jijini Dar es salaam.Hutumia kauli mbiu kama “nipe fagio” na “taka  nomaa.”
Mwisho, najua kila mtu anapenda kuona mazingira yakiwa safi, najua binadamu ndiye anayetengeneza uchafu kutokana na shughuli zake za kila siku, pia hakuna mtu anayependa kukaa na uchafu, cha kushangaza zaidi watu huukimbia uchafu…ila kuna watu wachache sana huusika kusafisha mazingira.
Naomba tukumbushane wajibu wetu kupitia nukuu maarufu kutoka kwa mwanaharakati wa mazingira-Mahatma Gandhi aliposema “Be the change that you wish to see most in your world.” Kwa tafsili isiyo rasmi-“Uwe chanzo cha mabadiliko utakayo kuyaona” hivyo ukitaka kuona mazingira safi anza kuonyesha juhudi ya kuyaweka mazingira katika hali ya usafi, anzia nyumbani kwako.Chukia uchafu kwa vitendo, usisubiri mtu mwingine aje kuleta makabadiliko-wewe ni chanzo cha mabadiliko.
Imetayarishwa na kutolewa na Jielimishe Kwanza! 
Barua pepe: jielimishekwanza@gmail.com
+255 754 572 143