Napenda
kuanza kwa kuwapongeza wafanyakazi wote hasa kwa kuzingatia Mei mosi ilikuwa ni
siku ya kilele cha sherehe ya Wafanyakazi.
Photo:http://www.mentoringminds.com/socratic |
Nianze kwa kuuliza maswali; ni mara ngapi tumekuwa
tukiwafikiria na kuwatendea wengine visivyo(hasi) na baadaye tunagundua kuwa
haikuwa kama tulivyokuwa tunafikiria? Je,unajisikiaje katika hali hii ya kuujua
ukweli? Bila shaka, hakuna anayeweza kupinga ukweli huu kuwa binadamu tunaamini
sana hisia zetu na kujitengenezea
majibu mepesi kwa maswali magumu kuliko kuamini akili zetu.
Sina maana kuwa hatutumii akili zetu,ila mara
nyingine tunakuwa wavivu kidogo katika kutoa maamuzi sahihi, na hii ni kwa
sababu hisia zetu huchukua nafasi kubwa katika mazingira fulani…majibu yatokanayo na hisia
hayaumizi kichwa wala kuuchosha ubongo na ni ya haraka.
Mungu katupatia akili ili tufikiri kwa makini,
kupambanua na “kujua ukweli wa mambo” kama Mwl.J.K.Nyerere alivyoandika katika
kitabu cha TUJISAHIHISHE kuwa Kujielimisha Kwanza ni kujua ukweli wa mambo,
huwezi kujua ukweli wa mambo kwa kuendeshwa na hisia.
Nikuhakikishie ndugu msomaji kuwa, hakuna
kitu kibaya kama ukamfikiria ndugu au rafiki yako kimtazamo hasi na akatambua
jinsi unavyomchukulia tofauti na alivyo kiasili.Itakupa shida sana hapo baadaye
ukibaini ukweli wa mambo.Ikiwa unataka kujua ukweli wa mambo unapaswa pia
kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kutoa maamuzi hasi. Soma
Hatupaswi kukurupuka na kujiwekea majibu ya
kihisia…mfano: eti naona ndugu yangu
hanichangamkii tena, nafikiri ameona sina kipato. Pia kutoa suluhisho la
kupotelewa pesa kisha kumshuku mtu fulani kaiba na unaanza kumvamia kwa
maneno hata ngumi, baadaye kidogo unakumbuka kuwa kuna kitu ulinunua na
mahesabu yako sawa…utajisikiaje katika hali hii?
Kuna madhara
makubwa ya kutoa maamuzi hasi bila kuwa na utafiti wa kutosha.Nimejaribu
kugusia kidogo baadhi ya madhara hayo hasa kuvunjika kwa uhusiano kwa kirafiki,
hii inamwonyesha mwingine hali ya kutokuaminiana katika urafiki.
Ikiwa
utahitaji kujua madhara mengine ya Kisaikolojia ya kutoa maamuzi hasi bila ya
kufanya utafiti, tuwasiliane +255 754 572 143.
Imetayarishwa
na kutolewa na
Jielimishe
Kwanza!
ni kweli kabisa...hii imenitokea! Nashukuru sana Jielimishe Kwanza kwa elimu hii
JibuFuta