N
|
Kutokana na utafiti wa hivi karibuni
uliofanywa na Jielimishe Kwanza! katika maeneo mbali mbali ya kazi, umebaini athari zifuatazo, ambazo huwapata wafanyakazi
katika mazingira ya kazi;
1.Kushuka kwa hamasa na shauku ya
kufanya kazi.Hivyo, wafanyakazi wengi wanafanya kazi kwa mazoea tu, bora siku
ziende.
2.Kudhoofika kwa ubunifu na mbinu
za utendaji wa mfanyakazi binafsi…mfanyakazi anakuwa na mtu wa kufuata
maelekezo tu!
3.Kuongezeka kwa manung’uniko ya
chini chini na migomo baridi kazini.
4.Kufanya kazi kwa hofu ya kukosa
ajira…hapa ndipo uhuru wa mfanyakazi unapotekwa. Soma makala inatakayofuata: “Hivi
ndivyo uhuru wako unavyoweza kutekwa”.
5.Kukosa fursa ya kuchangia na
kutoa maoni katika kuboresha maslahi ya mfanyakazi…maamuzi ya uongozi ni ya
mwisho haijalishi mfanyakazi ana mchango gani kwenye kampuni, shirika au
taasisi.
Ikiwa unakumbwa na athari mojawapo
kati ya hizi, jichunguze kwa makini, je una mchango gani katika eneo la kazi?
Nini kinahitajika kazini ili uweze kuheshimiwa na kupata haki yako kulingana na
jitihada zako?...ukiwa huna jibu sahihi au upo njia panda usisite kuwasiliana
na jopo la Jielimishe Kwanza! katika eneo husika, utapata ufumbuzi wa kuishi
kwa ndoto yako na kufuata kile moyo unapenda kufanya.
Tunakutakia kila la heri katika
kupambana na utumwa wa kisasa katika maeneo ya kazi.
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni