Ikiwa unafanya biashara tambua kuwa huwezi kukosa
mshindani.Mshindani wako ni yule anayetoa huduma au bidhaa kama yako kwa wateja
uliowalenga.Anaweza kuwa na mbinu mbali mbali zinazomfanya aweze kukaa kwenye soko.Hivyo unapaswa kumfahamu na kumchunguza.
Picha imetolewa blog.bounzd.com |
Ndugu msomaji na mfanyabiashara unayependa
kujielimisha kujiimarisha, naomba itambulike kuwa katika eneo hili sijabagua
aina ya biashara, ila nazungumzia biashara halali zenye kipato halali…ikiwa
sasa kuna njia nyingi tu za kufanya biashara halali, mfano kupitia teknolojia
ya habari na mawasiliano-mitandao ya jamii n.k. unaweza kuamua mwenyewe njia mahsusi itakayo kupatia mafanikio kwa urasahisi.
Katika
mtazamo wa biashara, inapaswa ujue kuwa, njia hizo zote huwezi kukosa
mshindani.
Unajisikiaje au unajipangaje unapoona
mfanyabiashara mwenzio anatoa huduma au kuuza bidhaa ile ile kwa mafanikio
kiasi kwamba anakaribia kukushinda? Hili ni swali gumu kwa mfanyabiashara
yeyote anayefanya biashara halali isiyo na mawaa.
Nikushirikishe
mbinu (5) pekee za kibiashara zinazotumiwa na wafanyabiashara wakubwa ambazo
hata wewe kama ni mfanyabiashara mdogo au mkubwa unaweza kuzitumia ikiwa tu
umewahi kusoma alama za nyakati.
Kabla ya kuanza kutafuta na kutumia mbinu hizi,
unapaswa kumjua mpinzani wako.Je wajua jinsi ya kumjua mpinzani wako? Soma hii.
Mbinu hizo ni; (leo nitaainisha 2)
1.Inunue kampuni inayoelekea kukutisha ili
ubaki kileleni.
Hapa unaweza kuniuliza; inawezekanaje hapa
ndugu mwandishi? Inawezekana
kabisa.Naomba nikupe mifano halisi: Mwaka 2012 Facebook iliweza kuinunua Instagram
(ikiwa ni kampuni changa iliyotishia uwepo wa Facebook) kwa dola bilioni 1($1
bilioni) kama ilivyoripotiwa na February 19, 2014: 6:54 PM ET.
Mwaka 2014, Facebook tena, imetangaza
kuinunua kampuni pinzani-WhatsApp kwa dola bilioni 19. Hiyo ndiyo biashara
kubwa zaidi ya ununuzi kuwahi kutekelezwa na Facebook hadi kufikia sasa. Najua
umejionea mwenyewe jinsi WhatsApp inavyokuja kwa kasi ikiwa na watumiaji zaidi
ya mil.450, na inajiongezea watumiaji wapya milioni 1 kila siku.
Pia, kwa
kufanikisha hilo mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa mtandao
huo upo njiani kuwaunganisha watu bilioni moja jambo litafanya Facebook kuwa na
thamani kubwa, BBC Swahili imeripoti leo, 20 Februari, 2014 - Saa 04:27 GMT.
2.Ingia Ubia Na Mpinzani Wako
Hapo zamani nchini Tanzania, tukiwa na
teknolojia hafifu tulitegemea sana kuhifadhi
na kutoa fedha zetu benki. Mapinduzi makubwa yametokea katika eneo hili
la biashara mara tu matumizi ya simu za mkononi ikiwa sanjari na teknolojia ya
kutuma na kupokea pesa pale ulipo…ikimaanisha si lazima uende benki kupanga
foleni.
Mfano halisi wa jambo hili ni pale baadhi ya benki nchini
Tanzania(sitaki kuzitaja, unazijua) zimepata mtikisiko mkubwa kutoka kwa mpinzani
mpya aitwae teknolojia ya kutuma na kupokea fedha kupitia simu za viganjani.
Huduma hii mpya imewavuta wateja wengi kiasi cha kutishia maisha ya Mkongwe wa
biashara.
Nikuulize ndugu msomaji, benki wanaishije
na mpinzani katika mazingira ya biashara? Bila shaka…utakuwa umejionea mwenyewe
jinsi Makampuni yanavyojenga ubia na mfumo mpya wa kutuma, kuweka na kupokea
fedha.
…Itaendelea.
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza! Social Interprises.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni