“The image you create about others and think it is real, becomes your
reality”-Henry Kazula.
M
|
ara nyingi tumekuwa tukiwafikiria na kuwasema wengine kinyume
na uhalisia wao.Kuna watu huwafikiria wengine mabaya tu, pia kujiaminisha kuwa
mafanikio ya wengine si ya halali au maisha wanayoishi wengine si halisi.
Yaani, tunawafikiria wenzetu mabaya! mabaya! tu.Huu ni mtazamo
hasi uliojijenga ndani ya nafsi za watu.
Kwa kipindi kirefu Jielimishe Kwanza! imefuatilia suala la
mtazamo wa watu kuhusu maisha na watu kwa ujumla.Imebainika kuwa ukiwasikiliza
watu 5 kuhusu ufikiri/mtazamo wao kwa watu fulani waliofanikiwa na hata wale
wasiofanikiwa utagundua kuwa ni mmoja tu atakayetoa maelezo yenye mtazamo
chanya.Kama huamini, fanya jaribio hili la kupima mtazamo wa watu.
Ikiwa taswira unazojingea kuhusu wengine ni hasi, huu utakuwa
ni uhalisia wako! na utajiaminisha, utakuwa ni mtu wa manung’uniko, masengenyo, kukata
tamaa ya maisha kwa kujiaminisha kuwa huwezi kufanikiwa kwa njia ya halali
inayohusisha juhudi zako binafsi.Madhala yake kwa Taifa ni makubwa, hususan
kuongezeka kwa wimbi la umasikini na utegemezi ndani ya jamii.
Pia utajikuta umeanza kujijengea mbinu zisizo sahihi
kupambana na uhalisia unaofikiria kuhusu hali na tabia ya maisha ya wengine.
Nikirudi kwenye mahusiano kwa wanandoa, kuna hatari kubwa
endapo mmoja wa wanandoa atakuwa na taswira hasi kuhusu mwenziwe.Mfano, mmoja
akimfikiria na kujenga taswira kuwa mwenziwe anatoka nje ya ndoa, itamjenga na itakuwa
ni uhalisia wake bila ya kuwa na utafiti wa kina.Hili hupelekea kuvunjika kwa
ndoa nyingi kwa sababu ya kukosa kuaminiana.
Nakuhamasisha ndugu msomaji, kubadili mtazamo kwa kujifunza
jinsi ya kuishi na watu na kufahamu njia halali za mafanikio yao…fuatilia
historia zao ili uwe na uthibitisho wa unachokiamini, kufikiria kabla ya kutoa
ushuhuda mbele ya wengine.
Soma hii http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/06/mtazamo.html ili uwe na mtazamo chanya.
Tukumbuke kuwa, Maaandiko Matakatifu yanatuasa kuwa si vizuri
kufikiria na kuwasemea wengine mabaya.
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni