inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Alhamisi, 13 Machi 2014

KAZI NA AJIRA: NAMNA YA KUACHA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAZURI NA SALAMA

-->Na Emmanuel C. Zongwe, kwa msaada wa mitandao. Mwandishi pia ni msomi wa masuala ya Kazi, Ajira na Rasilimali WatuTop of Form.Bottom of Form
+255 717 058 045

E-mail:ezongwe@yahoo.com
 


K
atika masuala ya kazi na ajira, jambo la muajiriwa kuacha kazi ofisi moja na kuhamia ofisi nyingine au kujiajiri ni la kawaida sana. Hii inatokana na mtu kuwa na matamanio ya kuwa na kazi nzuri zaidi, kazi inayolipa zaidi au anataka kuwa bosi wake mwenyewe (kujiajiri). Pamoja na kwamba jambo hili ni la kawaida katika mazingira ya kazi,tatizo lipo kwenye namna unavyoondoka katika ajira yako hiyo. 

Picha na woman.thenest.com
Je, unaondoka ukiacha mazingira salama au unaacha chuki na hasira kwa wengine? Watu wengi hujikuta wakiwa hawana mahusiano mazuri na waajiri wao wa zamani au hata wafanyakazi wenzao wa zamani. Wataalamu wa mambo ya Kazi, Ajira na Rasilimali Watu wanashauri kuwa jambo hili si zuri hasa kama mtu anahitaji kuwa na mtandao mpana wa wanataaluma tofauti    tofauti.
Kwa kuzingatia ushauri huo, hapa nakuletea njia sahihi 6 za wewe kuacha kazi uliyonayo sasa huku ukiacha mazingira salama na yenye kuweka hali ya kutengeneza mahusiano mazuri baadae.

1. Toa taarifa kwa wafanyakazi wenzako - siku uliyotoa taarifa rasmi kwa muajiri wako au siku chache baada, kutana na wafanyakazi wenzako, angalau watatu au wanne, ambao umekuwa ukishirikiana nao vizuri. Hao ni washauri wako wazoefu, ni marafiki wako katika masuala ya kitaaluma, ni watu unaopaswa kuendelea kuwa nao karibu. Waeleze kuwa unaacha kazi hapo, hakikisha pia unawaeleza namna misaada yao kwako ilivyokuwa ya thamani na kama ikiwezekana waeleze kuwa uko tayari kusaidiana nao hata kwa kipindi ambacho hutokuwa nao tena ofisini.

2. Onesha thamani ya ofisi hiyo - kwasababu kazi yako ya sasa na ufanisi uliouonesha hapo ndio chanzo cha wewe kupata ajira nyingine, basi onesha thamani ya ofisi hiyo. Hii ni muhimu hasa kama unahamia ofisi pinzani (competitor). Fanya mawasiliano na muajiri wako wa sasa, mueleze mategemeo yako kwenye ajira yako mpya, pia eleza namna unavyo thamini msaada wake kipindi chote ulichofanya naye kazi.

3. Tafuta mbadala wako - mkufunzi mmoja wa masuala ya Mawasiliano Sehemu ya Kazi, Jodi Glickman, ambaye ni Rais wa kampuni ya Communication Training anasema, "huwa nawahimiza watu wanaoacha kazi watafute watu watakaoziba nafasi zao kabla ya kuondoka". Kama muajiri atakuwa tayari, angalia mtandao wako na chagua angalau watu watatu ambao unahakika kati yao atapatikana mtu sahihi. Mpe muajiri wako mahali pa kuanzia kuziba pengo lako kwa kumpatia orodha ya watu    sahihi      kwa nafasi    hiyo.

4. Ondoka bila kuacha kasoro - hata kama unaona uwezo wako wa kutambua mambo unaweza kuwasaidia wafanyakazi unaowaacha pale, usijaribu kueleza mambo yatakayoacha kasoro pale. Mfano; usijaribu kusema mambo mabaya yamhusuyo muajiri, hata kama ndio yanayokufanya kuacha kazi hapo kwani kufanya hivyo kutaadhiri maendeleo ya taaluma yako. Badala yake eleza mambo chanya na uoneshe thamani ya viongozi wako wa kazi (supervisors).

5. Toa ujumbe wa shukrani
- fanya jitihada za kutuma ujumbe wa shukrani kwa waliokuwa viongozi wako wa kazi ambao kiukweli ndio waliokuwezesha kupata ujuzi mpya na uzoefu wa kazi (experience). Katika ujumbe huo eleza mambo mawili matatu ambayo hakika yalikusaidia sana. Ujumbe huu ni vizuri ukautuma      wiki chache baada ya kuondoka.

6. Fanya mrejeo - hapa namaanisha 'follow up'. Tengeneza namna ya kuendelea kupata habari zozote kumhusu muajiri wako wa zamani au kampuni uliyokuwa ukifanyia kazi. Fanya mawasiliano ya mara kwa mara na wafanyakazi wenzako wa zamani. Panga kukutana nao kwenye chakula cha mchana au wakati wa jioni, baada ya muda wa kazi na jadili nao mambo kadha wa kadha yahusuyo maisha.

Mwisho, hakika hizi njia zitakusaidia sana kuimarisha ukaribu na muajiri wako wa zamani. Ni dhahiri kuwa utapata ushirikiano kwani waajiri wazuri (smart employers) wanaelewa faida za kuwa na mawasiliano mazuri na wafanyakazi wao wa zamani.
Ni muhimu sana kwani hujui kesho na kesho kutwa utamkuta nani utakapokuwa unatafuta ajira nyingine mpya.
Imetolewa na
                                                     Jielimishe Kwanza!Social Entreprises


Jumapili, 9 Machi 2014

BIASHARA: NJIA PEKEE ZA KUPAMBANA NA KUMSHINDA MSHINDANI WAKO KATIKA BIASHARA…(SEHEMU 2)




Huu ni muendelezo wa makala iliyotolewa siku a Alhamisi, 20 Februari 2014, Soma.
Picha na blog.bounzd.com
Kwa kuzingatia maombi ya wasomaji wetu, tumeonelea ni vyema tukamalizia njia nyingine 3 zilizobaki za kupambana na kumshinda mshindani katika biashara,  ikiwa wengi wamejaribu kuzitumia njia mbili zilizotolewa katika makala iliyopita kwa mafanikio ya kuboresha ushindani wa biashara zao.
Nasi bila hiyana leo tunamalizia njia hizo kama ifuatavyo;
 3.Ongeza thamani ya ubora 
Wafanyabishara wengi hufikiri kuwa wakishusha bei zaidi ya mpinzani watalishinda soko, 
La hasha! Ikiwa mfanyabiashara kafikia hatua hii ujue kasahau kuwa, wateja hununua thamani ya kitu kwa lugha ya Kiingereza “value” ikiwa na maana ya kumridhisha mteja na si gharama ya kitu.Chukulia mfano wa bidhaa na huduma za Kampuni ya Apple zilivyo na thamani ya ubora  inayoendana na gharama.
Ingekuwa wateja wanaangalia gharama, hakika watu wachache sana wangeweza kumudu.Ila kwa kuzingatia thamani ya ubora, watu wanajitahidi kumiliki bidhaa na huduma za Kampuni ya Apple.
Hivyo,ongeza thamani ya ubora ikiwa sanjari na ongezeko la bei zaidi ya mpinzani wako…Hakika utalishinda soko!

4.Thamini kila mteja
Usijaribu hata siku moja kumbeza mteja wa aina yeyote ile, huwezi kujua leo kanunua kitu cha sh.1000 kesho atanunua kitu cha sh.10,000 nakuendela.Pia ujue kuwa wateja wako wanachukua sehemu kubwa ya matangazo, tena wanakufanyia matangazo bure! kwa njia ya mdomo…ni kwa sababu umewauzia thamani ya ubora wa huduma na bidhaa. 
Hii ni njia nzuri ya kucheza na saikolojia ya wateja wako, wakati huo huo ukiendelea kumshinda mpinzani wako katika soko.

5.Weka motisha kwa mteja
Njia hii ni nzuri ikiwa unaifuata njia namba 4.Njia hizi mbili zinaendana sana.Bila kujali aina ya mteja, hakikisha unajua kwanza motisha zitolewazo na mpinzani/wapinzani wako.
Mifano tunayo mingi, hebu jaribu kuchunguza makampuni ya simu jinsi yanavyocheza na akili za wateja kwa kuweka vijimotisha kila kukicha.Lengo lao kubwa ni kuhakikisha unabaki kwenye kampuni ya simu husika.Hata kama makampuni yote yanatoa motisha, usihofu!…mteja ndiye mwenye chaguo, atahakikisha anapata motisha kutoka kila kampuni kulingana na huduma itolewayo kwa wakati husika.Nawe hutakuwa na kitu cha kupoteza.

Mwisho, ndugu msomaji na mfanyabiashara nikutakie kila la heri katika kuboresha na kuimarisha biashara yako, usije kulogwa kumchukia mpinzani wako, huyu anakusaidia sana kuboresha biashara yako na kuifanya isibaki kama ilivyo kwa miaka nenda rudi.Hivyo mjue undani wake, Soma na boresha thamani ya ubora.
Kwa ushauri na maelekezo ya biashara, usisite kuwasiliana nasi,
+255 754 572 143

Imetayarishwa na kutolewa na 
Jielimishe Kwanza!

Jumanne, 4 Machi 2014

KAZI NA AJIRA: KUFANYA KAZI KWA BIDII PEKEE HAITOSHI…FANYA KWA MOYO!




“And the only way to do great work is to love what you do”-Steve Job
Njia pekee ya kufanya kazi kwa ufanisi ni kupenda kile unachofanya-Steve Job



 
Utendaji kazi na wenye tija ya mafanikio huanzia ndani ya moyo.Mtu anaweza kufanya kazi kwa bidii ila ndani ya moyo wake anasononeka na kuwaeleza wengine kuwa anapata ujira usiokidhi mahitaji yake.Hapa tunasema mtu huyu hana moyo wa kazi…
Picha:www.telegraph.co.uk
Watu wengi hufanya kazi wasizozipenda ilimradi tu wapate kipato kwa wakati husika, pia kwa sababu wamekosa kazi.Naomba nikuhakikishie ndugu msomaji, hakuna kitu kibaya kama kufanya kazi usiyoipenda! Ukifanya kazi usiyoipenda, hata kama unafanya kwa bidii vipi utajiona ni mtumwa tu.
Nikimnukuu Mama Theresa anasema; usitarajie mambo makubwa, tenda mambo madogo kwa moyo- kwa lugha ya kiingereza: “Don't look for big things, just do small things with great love.”Ukitenda mambo madogo kwa moyo ni rahisi sana kukupeleka kwenye mambo makubwa.Anasisitiza tena kuwa; Kufanya kazi pasipo upendo ni utumwa. “Work without love is slavery.”
Hapa nitatengeneza swali, moyo upi tena ikiwa natafuta kipato cha kukidhi mahitaji? Naweza kuliweka hili sawa kuwa, hupaswi kufanya kazi fulani usiyoipenda kwa minajili kuwa  ina kipato kikubwa…kama nilivyosema awali, utakuwa mtumwa wa kipato! Ndiyo maana kila siku wafanyakazi wanalalamika kuwa kipato hakitoshi, hii ni kwasababu wamejikita sana kwenye kuangalia maslahi pekee bila kuonyesha moyo wa kazi, pia hawalinganishi na ubora wa kazi wauletao kwenye soko.Kama alivyosema Jim Rohn kuwa, “watu hulipwa kutokana na uthamani wauletao kwenye soko.”Thamani kubwa zaidi kwenye soko, ujira mkubwa zaidi.Je, utawezaje kuleta uthamani kwenye soko kama huipendi kazi yako?
Ubora wa kazi hauwezi kupatikana kama watu wakitoa udenda kwanza kwenye kipato kabla ya kuonyesha moyo wa kujitoa na kuipenda kazi.Kwa lugha rahisi kabisa, onyesha moyo na nia ya kazi uifanyayo bila kutoa macho makubwa kwenye ujira.
Nimeshuhudia baadhi ya wafanyakazi wanaofanya kwa moyo- mh! Kama ukiwaona ndugu msomaji, unaweza kufikiri wanalipwa ujira mkubwa sana, lakini nilipopata fursa ya kuwahoji, wakanieleza kuwa wanafanya hivyo kwa sababu wanaipenda kazi, yaani wanajiona huru kufanya kazi.
Unaweza usinielewe kwa haraka haraka, fanya jaribio la kuipenda kazi kwanza, onyesha ubora, usinung’unike kama wengi wafanyavyo…utastaajabu kuona kipato kikiongezeka kwa njia nyingine.Utakuwa huru sana kwa sababu unajua sababu ya kufanya hivyo.
Ikiwa hujajua kazi uipendayo; jitathimini, isikilize sauti ya ndani ya moyo wako, chukua hatua ya kubadilika…simaanishi uache kazi, ila tenga muda wa ziada kuifanya kazi unayoipenda.
Kuna wakati mwingine nitakufahamisha faida za kufanya kazi unayoipenda.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Kama unataka ushauri usisite kuwasiliana nasi, 
Barua pepe: jielimishekwanza@gmail.com 
Skype: JielimisheKwanza13
Facebook: Jielimishe Kwanza!
+255 754 572 143



Jumamosi, 22 Februari 2014

MTAZAMO: HOJA HUPINGWA KWA HOJA...


MwanaTYVA na
Mwanafunzi wa Azania Sekondari.

W
akati pakiwa na taarifa zinazosambaa kwa kasi kuhusu wajumbe wa Bunge maalum la Katiba kudai kuwa fedha wanayolipwa kwa siku ya kiasi cha shillingi laki tatu (300,000=/) haitoshi hivyo waongezewe posho.

Nilipata muda na kurejea kusoma kijitabu kidogo cha TUJISAHIHISHE kilichoandikwa na Raisi wa TANU Julius K.Nyerere ili nirejee makosa yaliyofanyika kipindi cha TANU hadi akaamua kuandika kitabu hicho.Ulikuwa ni wakati mzuri wa kugundua kuwa makosa mengi hayajasahihishwa na yanaendelea, na yametufikisha hapa tulipo.Soma hii pia ili kujisahihisha makosa yetu.
J.K.Nyerere anaandika anasema "Ukiondoa matatizo yanayowapata binadamu kwa sababu ya mambo kama mafuriko,nzige,kiangazi na kadhalika MATATIZO YAO MENGI HUTOKANA NA UNAFSI" jambo linalowafanya kuuliza hali yao ya baadae itakuwaje na hufanya hivyo si kwa maslahi ya jamii ya watu,bali kwa maslahi yao binafsi.
Hayo yameanza kujitokaza ikiwa ni siku chache tu tangu wajumbe wa bunge maalum la Katiba kuwasili huko bungeni kutimiza yale jamii iliyowateuwa na  kuwaamini kuwa wanaweza fanya kazi waliyotumwa na wananchi.
Hayati J.K.Nyerere hakuishia upande mmoja tu,bali aliangalia upande wa pili wa shillingi na kuandika akisema "Kosa jingine linalotokana na unafsi tunalifanya wakati wa kuchagua viongozi,mahala pengine viongozi ( na hata wawakilishi) wetu hawana budi watokane na WATU bila hila au ujanja wa aina yoyote".Nimenukuu kifungu hiki nikihusisha na uhalisia kuwa tayari kuna taarifa za ndani toka bunge hilo maalum la Katiba na pengine katika vyombo mbalimbali ya habari kuwa kuna wawakilishi hawajaenda kuiwakilisha jamii yao,bali ni kwa manufaa yao binafsi.
J.K. Nyerere anaendelea na kusema "lakini mara nyingi wawakilishwaji huchagua wawakilishi bila kufikiri kwa makini kuwa viongozi hao wanaweza, au hawawezi kazi wanayochaguliwa kufanya.Wawakilishwaji watafanya makosa makubwa saana kama watachagua viongozi wao ovyo tu. Kimsingi yote ni makosa na kosa la kwanza ni tofauti na kosa la pili japo yote hutokana na Unafsi.”Swali la kujiuliza ni kwamba"
Wakati pakiwa na muendelezo wa matukio kadhaa kama haya, tunajifunza nini? na twapaswa kujisahihisha wapi? Kama Mtanzania mwenye kulichukulia kwa uzito wa hali ya juu Bunge maalum la Katiba nikijua fika ndipo mahali pekee patakapojenga hatma ya Tanzania njema,bora na yenye matumaini kwa Watanzania wote leo kesho,kesho kutwa au hata baada ya miaka hamsini ijayo tena,Wawakilishi wangeweka tofauti zao za kimaslahi pembeni kwanza na kutafakari kukubaliana kutimiza kwa moyo wa dhati majukumu watakayofanya wakiwa Bungeni-Dodoma kwa hizo siku na pengine zaidi kadri ya ufanishikishaji wa Katiba hiyo mpya, tarajiwa ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Hata hivyo napenda kumalizia kwa kusema kadhaliwa matakwa na mapendekezo ya wachache pia hujulikana katika mijadala,majadiliano na mazungumzo.Bila wachache kusema waziwazi matakwa yao,mijadala na majadiliano hayana maana.Kwa kadri ya mapendekezo na matakwa yao hao wachache waje na hoja na kupewa nafasi ya kusikilizwa kisha wenye kupinga nao wapinge kwa hoja.
Hivyo ni matumaini yangu kuwa wachache waliokuja na hoja ya kutokutosha kwa posho wanayolipwa, hivyo kutaka kuongezewa… watakuwa na hoja kwanini waona hivyo? na wachache wanaosema inatosha na kwa maana hiyo hapana uhitaji wa kuongeza posho hizo watakuwa na hoja kwanini wao wanaona hivyo.Hoja hujibiwa kwa hoja.
Mungu ibariki Tanzania. 
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!


Alhamisi, 20 Februari 2014

BIASHARA: NJIA PEKEE ZA KUPAMBANA NA KUMSHINDA MSHINDANI WAKO KATIKA BIASHARA…


Ikiwa unafanya biashara tambua kuwa huwezi kukosa mshindani.Mshindani wako ni yule anayetoa huduma au bidhaa kama yako kwa wateja uliowalenga.Anaweza kuwa na mbinu mbali mbali zinazomfanya aweze kukaa kwenye soko.Hivyo unapaswa kumfahamu na kumchunguza.
Picha imetolewa blog.bounzd.com 
Ndugu msomaji na mfanyabiashara unayependa kujielimisha kujiimarisha, naomba itambulike kuwa katika eneo hili sijabagua aina ya biashara, ila nazungumzia biashara halali zenye kipato halali…ikiwa sasa kuna njia nyingi tu za kufanya biashara halali, mfano kupitia teknolojia ya habari na mawasiliano-mitandao ya jamii n.k. unaweza kuamua mwenyewe njia mahsusi itakayo kupatia mafanikio kwa urasahisi.

Katika  mtazamo wa biashara, inapaswa ujue kuwa, njia hizo zote huwezi kukosa mshindani.

Unajisikiaje au unajipangaje unapoona mfanyabiashara mwenzio anatoa huduma au kuuza bidhaa ile ile kwa mafanikio kiasi kwamba anakaribia kukushinda? Hili ni swali gumu kwa mfanyabiashara yeyote anayefanya biashara halali isiyo na mawaa.

Nikushirikishe mbinu (5) pekee za kibiashara zinazotumiwa na wafanyabiashara wakubwa ambazo hata wewe kama ni mfanyabiashara mdogo au mkubwa unaweza kuzitumia ikiwa tu umewahi kusoma alama za nyakati.
Kabla ya kuanza kutafuta na kutumia mbinu hizi, unapaswa kumjua mpinzani wako.Je wajua jinsi ya kumjua mpinzani wako? Soma hii.
Mbinu hizo ni; (leo nitaainisha 2)


1.Inunue kampuni inayoelekea kukutisha ili ubaki kileleni.
Hapa unaweza kuniuliza; inawezekanaje hapa ndugu mwandishi?  Inawezekana kabisa.Naomba nikupe mifano halisi: Mwaka 2012 Facebook iliweza kuinunua Instagram (ikiwa ni kampuni changa iliyotishia uwepo wa Facebook) kwa dola bilioni 1($1 bilioni) kama ilivyoripotiwa na   @CNNMoneyTech February 19, 2014: 6:54 PM ET.
Mwaka 2014, Facebook tena, imetangaza kuinunua kampuni pinzani-WhatsApp kwa dola bilioni 19. Hiyo ndiyo biashara kubwa zaidi ya ununuzi kuwahi kutekelezwa na Facebook hadi kufikia sasa. Najua umejionea mwenyewe jinsi WhatsApp inavyokuja kwa kasi ikiwa na watumiaji zaidi ya mil.450, na inajiongezea watumiaji wapya milioni 1 kila siku. 
 Pia, kwa kufanikisha hilo mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa mtandao huo upo njiani kuwaunganisha watu bilioni moja jambo litafanya Facebook kuwa na thamani kubwa, BBC Swahili imeripoti leo, 20 Februari, 2014 - Saa 04:27 GMT.

2.Ingia Ubia Na Mpinzani Wako
Hapo zamani nchini Tanzania, tukiwa na teknolojia hafifu tulitegemea sana kuhifadhi  na kutoa fedha zetu benki. Mapinduzi makubwa yametokea katika eneo hili la biashara mara tu matumizi ya simu za mkononi ikiwa sanjari na teknolojia ya kutuma na kupokea pesa pale ulipo…ikimaanisha si lazima uende benki kupanga foleni.
Mfano halisi wa jambo hili ni pale baadhi ya benki nchini Tanzania(sitaki kuzitaja, unazijua) zimepata mtikisiko mkubwa kutoka kwa mpinzani mpya aitwae teknolojia ya kutuma na kupokea fedha kupitia simu za viganjani. Huduma hii mpya imewavuta wateja wengi kiasi cha kutishia maisha ya Mkongwe wa biashara.
Nikuulize ndugu msomaji, benki wanaishije na mpinzani katika mazingira ya biashara? Bila shaka…utakuwa umejionea mwenyewe jinsi Makampuni yanavyojenga ubia na mfumo mpya wa kutuma, kuweka na kupokea fedha.
…Itaendelea.
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza! Social Interprises.

Jumamosi, 25 Januari 2014

MTAZAMO: MAMBO TUNAYOSOMA, KUSIKILIZA NA KUTAZAMA YANATUJENGA KITABIA



K
atika maisha yetu ya kila siku tunakutana na mambo mbali mbali, mambo hayo tunayoyaona,kusoma na kusikiliza yana mchango mkubwa katika kujenga tabia zetu kwa njia moja au nyingine.
Mambo yote hayo yanaweza kutujenga na kuonyesha tabia hasi au chanya mbele ya jamii kulingana na mazingira.
Nikimnukuu msanii wa muziki wa kufoka foka nchini Tanzania, Farid Kubanga almaalufu kama 
Fid Q katika wimbo wake wa Propaganda kuna mstari anaimba-“tunajenga tabia kisha tabia zinatujenga” …hii ni kweli kabisa, tabia tunazozijenga kutokana na mazoea mbali mbali kwa kujua au kutokujua, zinatujenga kitabia.
Ijulikane kuwa,tabia ikijijenga ni vigumu kuibadili, ukweli huu ni sawa alivyoimba msanii wa muziki wa mashairi ya kughani Mrisho Mpoto katika wimbo wake wa “Nikipata nauli” kuwa, tabia ni kama ngozi ya mwili hauwezi kuibadili…ni afadhali iwe njema, ikiwa mbaya ni hatari kwa mtu binafsi na Taifa kwa ujumla.
Ikiwa unasikiliza,kusoma au kutazama masuala yenye mtazamo hasi na yenye hali ya hofu ya kutothubutu, ni hakika kabisa kuwa utakuwa ni mtu wa mashaka katika maisha yako.
Pia kuna masuala yanayovuta hisia na faida yake ni kitambo kidogo, haya yote kwa namna moja au nyingine yanajenga tabia ya msomaji,mtazamaji au msikilizaji na hatimaye kupelekea kuonyesha tabia hizo kwa vitendo mbele ya jamii.
Kwa hakika, tabia zetu na matendo yetu ni mazao ya masuala mbali mbali tunayoyasoma,kuyasikia na kuyaona.Hii hutokea pale tu tunapoamua kujifunza na kuyaweka katika utekelezaji kwa mazoea na hatimaye kuwa tabia.Unaweza usiamini haya niyasemayo, kwa sababu yanatokea kwetu bila kujijua…hadi mtu mwingine mwenye kujua tabia za watu atueleze.
Nikitoa mfano mdogo tu wa tabia ya ukatili kwa binadamu wenzetu, hii hutokea kwa mtu kuwa na mazoea ya kusoma,kusikiliza,kutazama sinema/video za watu makatili.Utaniuliza inawezekanaje mazoea yakasababisha mtu kuwa katili kwa wengine? Hii hutokea kwa sababu ya kuchukulia matendo ya watu makatili tunaowaona,kuwasikiliza na kusoma taarifa zao kimazoea katika maisha ya kawaida.Filamu mbali mbali za kikatili huwaaminisha watu kuwa matendo yaonekanayo ni ya kawaida tu ilhali si kweli.
Mfano mwingine ni ule wenye kuchochea tabia njema na yenye maendeleo na kupelekea mtu kubadilika kitabia kutokana na kusoma vitabu vyenye kuonyesha mbinu za mafanikio pia kuangalia filamu zenye kuchochea maarifa na utendaji bora wa kazi, hivyo kuleta maendeleo kwa mtu husika na taifa kwa ujumla.Fuatilia historia ya mafanikio ya watu mashuhuri duniani utagundua ukweli wa jambo hili.
Kufikia hapa unaweza kujichunguza mwenyewe, unapendelea kusoma,kusikiliza,kutazama mambo gani? Je, yana tija ya kukukomboa kiuchumi au yanakufanya uwe msindikizaji ya mafanikio ya wengine? Au yanakupa hofu ya kuchukua hatua ya kuthubutu kuelekea katika safari ya mafanikio? Sambamba na hilo, je unatumia muda katika njia ya kuzalisha faida au hasara? Majibu unayo mwenyewe…Tumia muda huu kuchagua kusoma,kusikiliza au kutazama mambo yanayojenga tabia njema, amini usiamini hutakuwa vile ulivyo sasa.
Nakutakia kila la heri  katika kujiepusha na mambo yasiyojenga tabia njema na kukutisha na kukukatisha tama ya kusonga mbele kimaendeleo…soma,angalia,sikiliza mambo yenye kuchochea mtazamo chanya…utapata ujasiri wa kuleta mabadiliko yenye tija ya maendeleo binafsi na  nchi yako kwa ujumla.
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza! 

Kwa udhamini wa ………………………………..(bofya hapa kuwa mdhamini na ujitangaze zaidi).



Jumanne, 14 Januari 2014

MTAZAMO 2: HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUTUMIA MTAZAMO WA WENGINE KUKUHUSU WEWE NA KUJIONGEZEA UTHAMANI…

-->

It’s what we learn about ourselves from our response that really matters-Marissa Walter
________________________________________________________________________________________

N
dugu msomaji, najua unaambatana nami kuhusiana na makala iliyopita kuhusu unavyojiona, unavyowaona na vile wanavyokuona wengine.http://jielimishekwanza.blogspot.com/2014/01/mtazamo-unavyojiona-unavyowaona-na-vile.html
Kama nilivyoeleza katika makala hiyo kuwa, kuna utofauti wa kimtazamo kwa sisi tunavyojiona ukilinganisha na ule wa wengine.
Moja kwa moja nikulete kwenye jinsi unavyoweza kutumia mtazamo wa wengine kukuhusu wewe na kujiongezea uthamani katika utendaji kazi na maisha ya kila siku.
Zipo njia mbali mbali zitakazokufanya uweze kutumia mtazamo wa wengine kujiongezea uthamani, nitainisha njia tano (5) zinazobeba nyingine;
1.Jitambue uwezo wako wa asili kabla ya wengine hawajakueleza.Hii ni njia muhimu sana…inatengeneza sehemu ya kuanzia kupima mtazamo wako kiutendaji.(Hili huanza na shauku au hamasa iliyo sanjali na uwezo wako wa ndani).
2.Kuwa mwepesi kupokea mawazo kutoka kwa wengine kutokana na mitazamo yao kukuhusu(uwe makini kulinganisha mawazo yako na yao ukisimamia sifa zinazoendana na wewe).
3.Usichukulie kama unadharaulika kutokana na mitazamo ya wengine kuhusu uwezo wako wa ndani…chukulia changamoto wanazozileta kama njia ya kuboresha mapungufu uliyonayo katika utendaji wako.(Tambua kuwa kuna watu wengine wapo kukukatisha tamaa, hawakutakii mema…utawajua kwa kusikiliza mawazo yao ukilinganisha na uwezo wako na mawazo ya wengi kukuhusu wewe).
4.Watumie vizuri watu unaofanana nao mtazamo…hawa watakuimarisha zaidi.
5.Usishawishike kubadisha mtazamo wako kuhusu ulivyo na utendaji kila wakati…hii itakufanya usiwe na msimamo, mwisho wa siku hautakuwa na kitu cha kusimamia na kutambulisha uwezo wako wa asili.Mfano:Ukiwa na shauku ya kuwa mwana mageuzi,kiongozi halafu mtu mwingine akakueleza kuwa huna sifa/karba hiyo na una sifa nyingine tofauti ilihali wengi wanathamini uwezo wako.
Picha na
--> ferociousstrength.com

Lakini mwisho wa siku, cha muhimu zaidi ni vile unavyojiona mbele ya watu wengine.Maoni yao kukuhusu wewe yanaongezea na kujenga uwezo wako kwa njia moja au nyingine kama utayachukulia kwa mtazamo chanya.
Nakutakia kila la heri katika kutumia mtazamo wako na wa wengine katika kuboresha uthamani wako.
Imetayarishwa na kutolewa na 
Henry Kazula
Jielimishe Kwanza!

Ijumaa, 10 Januari 2014

MTAZAMO: UNAVYOJIONA, UNAVYOWAONA NA VILE WANAVYOKUONA WENGINE…

-->
-->
“Person perception refers to the different mental processes that we use to form impressions of other people.” Michal Zacharzewski

W
atu wengi kwa maeneo tofauti wamekuwa wakiamini sana vile wanavyojiona na kujichukulia hasa katika uwezo wa asili wa kupambanua mambo na utendaji. Kujiaminisha huko kunatokana na hisia zao za ndani zinazoendeshwa na dhamiri zao.
Picha na www.elements2lead.com
Mtazamo wa kisaikolojia unadhihirisha kuwa tunavyojiona kwa nje kwa kulinganisha na utendaji wetu wa kila siku ni tofauti na wengine wanavyotuona na kutuchukulia.
Pia tunavyowaona wengine na kujiaminisha kuwa ni uhalisia wao  unakuwa uhalisia wetu kuwahusu wao.Soma hii kujua zaidi kupitia http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/12/mtazamo-taswira-unayowajengea-watu.html
Mwanasaikolojia Kendra Cherry, kupitia http://psychology.about.com/od/socialpsychology/a/person perception.htm anaeleza kuwa kuna hali tatu za kimuonekano zinazopelekea kuwachukulia wengine; tabia ya mtu unayemtazama, mazingira ya tukio na tabia yako mwenyewe.
Tunaweza kujiona tuna kipaji au uwezo fulani na kulizika, lakini kwa upande mwingine bila kujijua tuna uwezo mwingine mkubwa uliojificha ambao hatuuoni ila wengine wanauona.
Tufanye nini sasa ili kujua mtazamo wa wengine kuhusu tulivyo na uhalisia wetu?
Fuatana nasi katika makala ijayo ili ujue upande wa pili unatuchukuliaje ili utumie fursa hiyo kutambua uwezo wako mwingine na kujiongezea uthamani mbele za watu.

Imetayarishwa na kutolewa
Jielimishe Kwanza!


Alhamisi, 2 Januari 2014

MAFUNZO NA AJIRA:FURSA ZA KUJITOLEA NA KUPATA FURSA YA AJIRA

Opportunity to your door, Get this opportunity,Learn to become a skilled Volunteer.Get exposed to employment opportunity.

Volunteers selected to join with Jielimishe Kwanza!
(
Social Enterprises) will get training fee discount of 50% to attend a training on Volunteerism and Professional soft skills for 1st week(full course) and 2nd week (hidden qualities required by employers from volunteers+connection to other working place). Other volunteers will be required to pay 100% of training fee.

Training fee will cover training materials+venue+refreshments.
Apply or Register Now!

Read http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/10/vijana-kujitolea-njia-kuelekea-kupata.html to get some tips on volunteering.

Jumapili, 22 Desemba 2013

MTAZAMO: KUELEKEA MWAKA 2014, TUJIELIMISHE! TUJIFUNZE! TUJIPANGE UPYA KUPITIA MAKOSA…



K
ujifunza kwa kweli na kwenye tija ni kupitia MAKOSA yaliyofanyika awali, hii ni kwa sababu, hayo ndiyo yametufikisha hapa tulipo.
Nikiwa katika mapumziko, sehemu tulivu yenye upepo mwanana pembezoni mwa Mlima mrefu Afrika, uliopo nchini Tanzania-Mlima Kilimanjaro (http://www.tanzaniaparks.com/kili.html), nafakari kuhusu mwaka 2013 na kupanga mikakati kuelekea mwaka 2014…naamua kuperuzi katika maktaba yangu ndani ya “laptop” nakutana na kijitabu kiitwacho “Tujisahihishe” cha Mwl.J.K.Nyerere (1962) chenye kurasa 8.
Nikashawishika na jina la kijitabu hicho, hivyo nikataka kujua kulikoni ndani yake…Mwanzoni ilibaki kidogo niachane nacho, kwa sababu kilikuwa kikielezea makosa ndani ya T.A.N.U, najua hata wewe unaweza kusema nani anasoma vitabu vya T.A.N.U hadi leo?
Nikakumbuka msemo huu; ya kale ni dhahabu, ikanijia shauku ya kutaka kuyajua makosa hayo…yawezekana yamekufikisha/yametufikisha hapa tulipo.Nikaanza kusoma kwa makini na kufumbuka macho kujionea makosa ya mwaka 1962 ambayo Watanzania tunaendelea kuyafanya kwa kujua, kwa mazoea au kutojua…
“Nitanukuu moja ya makosa yaliyoainishwa na Mwalimu, Jielimishe Kwanza! inaliona kosa hili kubeba makosa mengine tunayoyafanya kila siku;
Kosa jingine ni kutojielimisha.Kanuni yetu ni moja inasema: “Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu wote na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote”. Kwa ufafanuzi zaidi, anasema; Kujielimisha siyo maana yake kwenda shuleni. Kujielimisha ni kutafuta ukweli wa mambo. Kwenda shule hutusaidia.Lakini japo hatuwezi kwenda shule twaweza kujifunza”.
Watu wengi hukoma kujielimisha mara tu wakihitimu masomo yao na kufikiri kuwa wanajua kila kitu.Mwl.J.K.Nyerere katika kitabu hicho anawaainisha:
 “watu walio hatari sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu wala hawana haja kujifunza zaidi.
Nabainisha haya kwa kukuhamasisha ndugu msomaji kukaa chini na kutafakari makosa uliyoyafanya mwaka 2013 ili usiyarudie mwaka 2014.
Ikiwa unajiona hukufanya kosa au makosa, tambua kuwa hakuna mkamilifu katika dunia hii…Maandiko Matakatifu yamebainisha.Nilihamasika sana na mwisho wa kitabu cha Mwalimu, aliweka wazi, nanukuu; sitaki Mtu ye yote afikiri kuwa mimi niliyeandika maneno hayo sinayo makosa.Hivyo si kweli.Hii na kwangu kadhalika, najifunza sana kupitia makosa ninayofanya.
Naomba nisiwe msimuliaji sana wa maneno ya Mwalimu, hamasika kujisomea mwenyewe kijitabu hicho ili ujue makosa mengine ili yasijirudie kwako.
Tena na tena, naomba utumie wakati huu mzuri wa mapumziko kujichunguza mapungufu yako yaliyopelekea kufanya makosa uyajuayo.Jielimishe! Jipange upya kwa kujiwekea mikakati ukijifunza kwa makosa.
Nakutakia mapumziko mema na kukutakia heri na fanaka ya Krismasi na Mwaka mpya 2014.
Imetayarishwa na
Henry Kazula,
Mkurugenzi mtendaji.
Jielimishe Kwanza!