D
|
hana ya KUJITOLEA inaonekana ni mpya sana
kwa nchi mbali mbali za Kiafrika.Nikichulia mfano nchini Tanzania, vijana wengi
wenye sifa za kupata ajira wanakaa nyumbani kusubiri wajibiwe maombi waliyotuma
katika taasisi mbali mbali zinazotegemewa sana kwa kutoa ajira. Wakati huo huo
wanasahau kuwa ujuzi wao unaendelea kupungua siku hadi siku. Pia kuna vijana
wengine wasio na elimu ya kazi ila wana vipaji wapo vijiweni wakiendelea
kufifisha vipaji vyao.
Jielimishe Kwanza! imefuatilia kwa kina
dhana ya nzima ya KUJITOLEA na kuona kuwa kuna faida nyingi zinazoweza kupatikana kwa
kijana kuchukua hatua ya uthubutu kuanza KUJITOLEA.Faida hizo ni;
- Kupata uzoefu wa kazi unayofanya…hivyo kigezo cha uzoefu kazini haikitakuwa kikwazo cha wewe kupata kazi
- Utajifunza mbinu mpya za kazi
- Kujiongezea wigo wa kufahamiana na watu katika kazi unayofanya
- Ni njia mojawapo kukuunganisha na kazi nyingine
- Utaifurahia kazi unayofanya kwa sababu unaipenda
- Unajiongezea hali ya kuaminika kupata kazi
http://lindsayolson.com/5-reasons-you-should-volunteer-to-find-a-job/ |
Narudia tena FIKIRI! tena kwa mapana(Uwe
na taswira kubwa) ANZA kidogo kulingana na uwezo wako ukizingatia kiasi kidogo cha pesa
ulicho nacho.Tambua kuwa, mabadiliko makubwa huanzia na jitihada ndogo ya mtu
mmoja.
Chukulia mfano wa mtu kama Mahtma Gandhi alivyoweza kuleta mabadiliko
makubwa nchini India.Alituachia msemo huu maarufu duniani “Be the change
that you wish to see most in your world”-Mahatma Gandhi.-Uwe chanzo cha
mabadiliko utakayo kuyaona.
ANZA SASA! kwa kujiweka, kujitokeza sehemu zenye fursa ili
uonekane…TAMBUA kuwa FURSA HAIKUTAFUTI! JITOKEZE KUONA FURSA! Soma hii. http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/09/somo-kupitia-mimeatafuta-fursa-uonekane.html
Huna sababu ya kutembea na bahasha au
kushinda ukipezi kutafuta nafasi za kazi mtandaoni au magazetini.Tambua kuwa
kazi nyingi hutolewa kwa kufahamiana.
Najua mwanzo mgumu! Fahamu kuwa hakuna
kitu kinapatikana kiurahisi…ukiona kipo cha urahisi kina shaka! Ni lazima
utalipia gharama…Waingereza wanasema hivi “you
will pay the price nothing is for free”
Nikutie moyo zaidi kijana uliyekata tamaa
ya kupata ajira kupitia nukuu maarufu ya mwandishi na msemaji wa hadhara- Zig
Ziglar anasema(na si alisema, kwa sababu maneno yake yanaishi) “You will get all you want in
life if you help enough other people get what they
want”- Zig Ziglar.(Utapata ukitakacho maishani kwa
kuwasaidia wengine kikamilifu kupata wanachotaka).
Angalizo:
Angalizo:
- Usisahau kuwa Jielimishe Kwanza! inahitaji watu wa kujitolea "Volunteers" katika njanya ya Uandishi wa makala zenye mtazamo chanya na kuhamasisha utendaji bora wa kazi.
Tuwasiliane: 0716 075 826 jielimishekwanza@gmail.com
Imetayarishwa
na kutolewa na
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni