K
|
ujifunza kwa kweli na kwenye tija ni
kupitia MAKOSA yaliyofanyika awali, hii ni kwa sababu, hayo ndiyo yametufikisha
hapa tulipo.
Nikiwa katika mapumziko, sehemu tulivu
yenye upepo mwanana pembezoni mwa Mlima mrefu Afrika, uliopo nchini
Tanzania-Mlima Kilimanjaro (http://www.tanzaniaparks.com/kili.html), nafakari
kuhusu mwaka 2013 na kupanga mikakati kuelekea mwaka 2014…naamua kuperuzi
katika maktaba yangu ndani ya “laptop” nakutana na kijitabu kiitwacho
“Tujisahihishe” cha Mwl.J.K.Nyerere (1962) chenye kurasa 8.
Nikashawishika na
jina la kijitabu hicho, hivyo nikataka kujua kulikoni ndani yake…Mwanzoni
ilibaki kidogo niachane nacho, kwa sababu kilikuwa kikielezea makosa ndani ya
T.A.N.U, najua hata wewe unaweza kusema nani anasoma vitabu vya T.A.N.U hadi
leo?
Nikakumbuka msemo huu; ya kale ni dhahabu, ikanijia shauku ya
kutaka kuyajua makosa hayo…yawezekana yamekufikisha/yametufikisha hapa
tulipo.Nikaanza kusoma kwa makini na kufumbuka macho kujionea makosa ya mwaka 1962
ambayo Watanzania tunaendelea kuyafanya kwa kujua, kwa mazoea au kutojua…
“Nitanukuu moja ya makosa yaliyoainishwa
na Mwalimu, Jielimishe Kwanza! inaliona kosa hili kubeba makosa mengine
tunayoyafanya kila siku;
Kosa
jingine ni kutojielimisha.Kanuni yetu ni moja inasema: “Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu
wote na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote”. Kwa ufafanuzi zaidi,
anasema; Kujielimisha siyo maana yake
kwenda shuleni. Kujielimisha ni kutafuta
ukweli wa mambo. Kwenda shule hutusaidia.Lakini japo hatuwezi kwenda shule
twaweza kujifunza”.
Watu wengi hukoma kujielimisha mara tu
wakihitimu masomo yao na kufikiri kuwa wanajua kila kitu.Mwl.J.K.Nyerere katika
kitabu hicho anawaainisha:
“watu walio hatari sana ni wale ambao
wanafikiri kuwa wanajua kila kitu wala hawana haja kujifunza zaidi.
Nabainisha haya kwa kukuhamasisha ndugu
msomaji kukaa chini na kutafakari makosa uliyoyafanya mwaka 2013 ili usiyarudie
mwaka 2014.
Ikiwa unajiona hukufanya kosa au makosa,
tambua kuwa hakuna mkamilifu katika dunia hii…Maandiko Matakatifu
yamebainisha.Nilihamasika sana na mwisho wa kitabu cha Mwalimu, aliweka wazi,
nanukuu; sitaki Mtu ye yote afikiri kuwa
mimi niliyeandika maneno hayo sinayo makosa.Hivyo si kweli.Hii na kwangu
kadhalika, najifunza sana kupitia makosa ninayofanya.
Naomba nisiwe msimuliaji sana wa maneno
ya Mwalimu, hamasika kujisomea mwenyewe kijitabu hicho ili ujue makosa mengine
ili yasijirudie kwako.
Tena na tena, naomba utumie wakati huu
mzuri wa mapumziko kujichunguza mapungufu yako yaliyopelekea kufanya makosa
uyajuayo.Jielimishe! Jipange upya kwa kujiwekea mikakati ukijifunza kwa makosa.
Nakutakia mapumziko mema na kukutakia
heri na fanaka ya Krismasi na Mwaka mpya 2014.
Imetayarishwa na
Henry Kazula,
Mkurugenzi mtendaji.
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni