“Person
perception refers to the different mental processes that we use to form
impressions of other people.” Michal Zacharzewski
W
|
atu wengi kwa maeneo tofauti wamekuwa wakiamini sana vile
wanavyojiona na kujichukulia hasa katika uwezo wa asili wa kupambanua mambo na
utendaji. Kujiaminisha huko kunatokana na hisia zao za ndani zinazoendeshwa na
dhamiri zao.
Picha na www.elements2lead.com |
Mtazamo wa kisaikolojia unadhihirisha kuwa tunavyojiona kwa nje kwa
kulinganisha na utendaji wetu wa kila siku ni tofauti na wengine wanavyotuona
na kutuchukulia.
Pia tunavyowaona wengine na
kujiaminisha kuwa ni uhalisia wao
unakuwa uhalisia wetu kuwahusu wao.Soma hii kujua zaidi kupitia http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/12/mtazamo-taswira-unayowajengea-watu.html
Mwanasaikolojia Kendra Cherry,
kupitia http://psychology.about.com/od/socialpsychology/a/person perception.htm
anaeleza kuwa kuna hali tatu za kimuonekano zinazopelekea kuwachukulia wengine;
tabia ya mtu unayemtazama, mazingira ya tukio na tabia yako mwenyewe.
Tunaweza kujiona tuna kipaji au uwezo fulani na kulizika,
lakini kwa upande mwingine bila kujijua tuna uwezo mwingine mkubwa uliojificha
ambao hatuuoni ila wengine wanauona.
Tufanye nini sasa ili kujua mtazamo wa wengine kuhusu tulivyo
na uhalisia wetu?
Fuatana nasi katika makala ijayo ili ujue upande wa pili unatuchukuliaje
ili utumie fursa hiyo kutambua uwezo wako mwingine na kujiongezea uthamani mbele
za watu.
Imetayarishwa na kutolewa
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni