B
|
iashara hujumisha kuuza na kununua kwa lengo la kupata faida…kwa muuzaji
na pia mnunuzi anafaidika kwa kupata thamani (kwa lugha ya Kiingereza hujulikana kama “value”) ya huduma au
bidhaa aliyoilipia. Ifahamike kuwa mteja/mnunuzi huridhishwa na thamani-“value”
ya huduma au bidhaa, hivyo kutoa pesa yake kununua/kulipia gharama ya
bidhaa/huduma inayotoa/kuleta thamani kwake.
Hapa ndipo inapotumika kanuni rahisi ya Uchumi inayosema; watu hulipwa
kwa kuleta uthamani katika soko “people
get paid by bringing value to the market place”.Itambulike kuwa kuna njia
mbali mbali ambazo mtu anaweza kulipwa kwa kuleta uthamani katika soko.Mfano:
kupitia biashara na kuajiriwa.
Siku zote Wafanyabiashara wanaitumia sana kanuni hii ya “kulipwa kupitia uthamani na ubora wauletao
katika soko” kwa kujua au kutokujua hasa kwa kujilinganisha na wapinzani
wao wa biashara na kuboresha mapungufu au udhaifu wa wapinzani wao.
Ni vyema na ni wajibu kumjua mpinzani wako na kumfuatilia kwa ukaribu
sana na si kumchukia, kumfanyia mizengwe au kumpotezea. Kuthibitisha hilo
angalia mfano wa wapinzani hawa wa biashara jijini Dar es salaam nchini
Tanzania...
Kila mmoja anamtumia mwenzie kwa lengo zuri la kuleta uthamani wa
huduma aitoayo kwa mtumiaji/mteja.Mwisho wa yote ni kazi ya mtumiaji kuchagua.
Mtambue mpinzani wako, mfuatilie kwa umakini bila kuiga kila kitu
anachofanya…wewe boresha ubora wa huduma/bidhaa yako utafanikiwa.
Pia soma hii http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/08/biashara-ukitaka-kujenga-biashara-imara.html na
http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/06/biashara.html
Pia soma hii http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/08/biashara-ukitaka-kujenga-biashara-imara.html na
http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/06/biashara.html
Imetayarishwa
na kutolewa na
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni