Siku hii kuu kwa kina mama duniani huadhimishwa kila mwaka siku ya Jumapili ya pili ya mwezi Mei. Mwaka huu, itakuwa siku ya jumapili ya tarehe 12 Mei 2013.
Imechorwa na Henry Kazula |
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Tanzania imeshika nafasi ya 135 kati ya nchi 176 duniani zilizofanyiwa utafiti na ya 3 katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Hata hivyo, taarifa hiyo ilieleza kuwa wanawake wengi wanapoteza maisha wakiwa kwenye ujauzito na wakati wa kujifungua ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika na duniani kwa ujumla.
Taarifa hiyo ilijikita katika kuangalia jinsi akina mama na watoto chini ya miaka mitano walivyo katika hatari kubwa ya kupoteza maisha, afya ya uzazi, elimu kwa wanawake, kipato cha wanawake na hali yao kisiasa.
Habari zaidi: http://www.thecitizen.co.tz/News/-/1840392/1845698/-/exkklrz/-/index.html
___________________________
Kipekee
nashukuru kwa kupata taarifa hii muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu.Hii
imekuwa kama taa nyekundu iliyowashwa kuonyesha hatari.Hapa hatutakiwi
kununa wala kubisha au kupuuza tafiti zilizogharimu fedha na muda, hali
halisi kila mtu anaiona na kuweza kuthibitisha.
Taarifa
kama hizi zinapotolewa wengine hubisha kwa kuangalia eneo dogo tu hasa
huduma za afya mijini hasa majiji.Ukienda vijijini hali si nzuri, wewe
mwenyewe unaweza kuwa shahidi.
Hapa,
kila mwananchi anapaswa kuwajibika na si kunyooshea kidole kwa Serikali
pekee.Mashirika binafsi, watu binafsi tujitoe ili kuboresha hali ya
akina mama ambao ni walezi wakubwa katika familia zetu.
Mabadiliko yanaanza na mtu mmoja, mwishoni taifa lote kwa ujumla.
Hivyo basi, tuisheherekee siku hii, lakini tujue kuwa wakina mama nchini wana hali mbaya.
Itambulike
kuwa, madhara ya hali mbaya yao hayaishii kwao, bali ni jamii kwa
ujumla.Naomba tuzingatie ule usemi usemao "Ukimkomboa mwanamke,
umekomboa taifa"...
Ukiwa kama mdau, unaweza kunitumia maoni na ushauri ili taarifa hii mbaya isijitokeze tena mwakani.
Maoni:
Barua pepe: jielimishekwanza@gmail.com
Ukurasa wetu wa facebook: jielimishe.kwanza@facebook.com
Madhara (8) ya kumzuia mtoto wa umri(Miaka 3-12)kushiriki michezo na watoto wa rika lake:
Ijumaa, 3 Mei 2013 Saa 5.55usiku
Wazazi wengi nchini na jamii nyingine wanapenda kuwaona watoto wao
wakiwa kama wao
Kwa maana nyingine wanataka kuwaona
watoto wao wakiwa kama nakala zao.
Watoto wa umri kati ya miaka 3-12(ni umri kabla ya kuanza shule na
kuanza shule) huonyesha tabia za kutaka kufanya vitu wenyewe bila kuzuiliwa na
mtu yeyote. Hupenda kujifunza lugha, na ishara mbalimbali kwa kasi isiyo ya
kawaida. Hapa wazazi wengi huwachukulia watoto wao kuwa ni watundu na
wasumbufu,la hasha! Ni umri wao kutaka kujifunza kuhusu mambo yanayowazunguka.
Kama mwanasaikolojia, Maria Montessori alivyoainisha kuhusu makuzi ya
watoto, anasema kuwa watoto wa rika hili
hupenda kuwa na urafiki na watoto wa rika lao. Pia kuhusu kuwaruhusu watoto
wafanye vitu wanavyoweza kufanya na si kulazimisha kuwasaidia.Alisema, "Never help a child with a task at which he
feels he can succeed." Yaani “Usimsaidie
mtoto kufanya kazi iliyo kwenye uwezo wake.”
Kiuhalisia makuzi ya watoto hutegemea sana mazingira, mfano mtoto
aliyekulia mazingira ya shida na duni kiuchumi anatofautiana sana kiutendaji na
yule aliyetokea mazingira ya raha na furaha na uchumi mzuri.Tofauti hii ambayo
inahusisha saikolojia ya makuzi ya mtoto, ina uwezo mkubwa sana wa kushusha au
kuongeza/kuimarisha utendaji wa mtoto afikiapo utu uzima.
Nitazungumzia tofauti za watoto katika mazingira hayo mawili katika
makala nyingine.Leo napenda uungane nami katika kuyajua madhara (8) ya kumzuia
mtoto wako kushiriki michezo ya kawaida na wenzake...
Mwanasaikolojia maarufu duniani Erick Erickson 1956 aliainisha hatua
nane(8) za maendeleo ya makuzi ya binadamu kijamii na kihisia kuanzia kuzaliwa
hadi utu uzima.Alisisitiza kuwa kila hatua ina vipingamizi vyake ni muhimu
kupitia kila hatua na kuondoa vipingamizi hivyo kabla ya kwenda hatua nyingine.
Nitapenda kujikita hasa kwenye makuzi ya watoto ambayo yana mchango
mkubwa kwa utu uzima wa mtu.Nikizingatia hatua mbili za makuzi ya mtoto yaani hatua ya 2 na hatua ya 3 za
maendeleo ya ukuaji wa mtoto kama alivyozielezea Erickson;
Katika hatua ya pili (2) umri wa mtoto kabla ya kuanza shule
(chekechea), aliangalia mambo mawili yanayopingana yaani “Kujifunza mwenyewe Vs Aibu (miaka 3-4)”.Akimaanisha kuwa mtoto wa
umri huu hupenda kufanya mambo mwenyewe na hujisikia aibu pale anapokatazwa kwa
kuambiwa “Usi…” Mtoto aliyekuzwa vizuri hujisikia vizuri bila kuwa na aibu
yoyote.
Pia katika hatua ya tatu (3) umri wa kuanza shule (baada ya chekechea),
umri wa michezo, mtoto hupambana na vitu viwili yanayopingana yaani Kujianzishia kujifunza Vs Kujilaumu/Hatia.(miaka
4-12). Akimaanisha kuwa mtoto
aliyekuzwa vizuri kwa kupewa uhuru wa kujifunza (1) hujiona fahari kuwa na
wenzake,(2) hupenda kushirikiana na wenzake, (3) hupenda kuongoza pia
kuongozwa.
Kwa upande mwingine, mtoto aliyekuzwa mazingira ya kubanwa hujihisi
kuwa na hatia hivyo (1) huwa muoga (2) hujitenga na wenzake (3) anakuwa
tegemezi sana kwa wazazi (4) anakuwa amekosa mbinu za michezo na uwezo wa
ubunifu.
Nitayajumuisha madhara (8) ayapatayo mtoto wako kwa kukosa kushiriki
michezo ya kitoto na wenzake kama ifuatavyo;
___________________
1.Mtoto kukosa uwezo wa kujiamini mbele ya hadhara
Ukifuatilia michezo ya watoto kama mpira,kukimbizana, na mingine mingi utagundua kuwa watoto ni waongeaji na watendaji hasa wakiwa na watoto wa rika lao.Endapo mtoto wako atakosa fursa ya kukutana na wenzake, kwanza atakuwa na hofu-kwasababu hajawazoea, pili atajihisi mnyonge mbele ya wenzake.Hivyo kuanza kuijenga tabia ya kutokujiamini tangu utotoni.
2.Kukosa uwezo wa kuongoza
Kutokana
na hofu aliyojingea tangu utotoni, ni dhahiri kuwa atakuwa hana mbinu za
kuwasiliana kama kiongozi, pia atakuwa na aibu iliyopitiliza mbele ya watu
anaotakiwa kuwaongoza.
3.Kuwa mtegemezi wa maamuzi mbali mbali kwa wazazi hata yaliyo kwenye uwezo wake
Tatizo
hili ni kubwa, limepelekea vijana wengi kushindwa kuamua mambo yao wenyewe, eti
“labla nimuulize baba na mama”, kazi lazima achaguliwe na wazazi/walezi.
Hili ni
tatizo lililokuwa tangu utotoni, yaani kukosa uwezo wa kuamua kufanya hasa
baada ya kuambiwa “Usi…” na kutopata nafasi ya kuona watoto wengine wakijaribu
kufanya jambo fulani.
4.Mtoto hujitenga na jamii
Kwa
kuwa mzazi au mlezi ulimtenga mtoto na jamii kwa kumfungia ndani wakati wote,
na kumwachia mtoto wako awe na urafiki mkubwa na Televisheni na michezo yake
pekee, usitegemee kuona mtoto wako akiwa mbali na jamii hasa afikapo ujana na
hata utu uzima.
5.Kukosa uwezo na mbinu za kuwasiliana
Kama
nilivyoeleza awali, watoto wa umri huu hupenda kujifunza lugha na ishara mbali
mbali za mawasiliano wakiwa na watoto wa rika lao.
Hivyo basi, kama utamfungia mtoto wakati wote asikutane na wenzake, tambua kuwa unamwandaa mtoto ambaye atakuwa hana uwezo mzuri kimawasiliano.Ujuzi huu ni muhimu sana katika shughuli mbali mbali za kijamii.
Hivyo basi, kama utamfungia mtoto wakati wote asikutane na wenzake, tambua kuwa unamwandaa mtoto ambaye atakuwa hana uwezo mzuri kimawasiliano.Ujuzi huu ni muhimu sana katika shughuli mbali mbali za kijamii.
6. Kuwa na viungo dhaifu na kukosa uchangamfu wa mwili
Itafahamika
kuwa uimara wa viungo vya mtoto haujengwi na vyakula pekee, bali mazoezi ya
viungo hasa kwa michezo ya kitoto ya kukimbizana hapa na pale.
Kisaikolojia, mtoto huathirika sana anapoona watoto wengine wakicheza kwa furaha wakati yeye anazuiliwa ama kwa kupigwa na kukaripiwa.Hii humfanya mtoto kunyongea na kukosa uchangamfu.
Kisaikolojia, mtoto huathirika sana anapoona watoto wengine wakicheza kwa furaha wakati yeye anazuiliwa ama kwa kupigwa na kukaripiwa.Hii humfanya mtoto kunyongea na kukosa uchangamfu.
7. Humpelekea mtoto kujitengenezea tabia ya kutoroka ili atimize hisia zake
Hapa
ndipo utukutu na tabia mbaya zinapoanzia.Mtoto anaamua kujitengenezea mbinu ili
aweze kushiriki kwenye michezo ya kitoto.
Mtoto anapofikia hatua hii, wazazi wengi hulaumu sana kuwa watoto wa siku hizi hawatulii, wakiwa wamesahau kuwa wenyewe ndiyo chanzo cha kuwafanya watoto watoroke kwasababu ya ulinzi mkali nyumbani.
Mtoto hawezi kutoroka nyumbani kama anapata upendo na kueleweshwa mema na mabaya kwa vitendo, pia kwa kumpa na kukubaliana utaratibu wa michezo.
Mtoto anapofikia hatua hii, wazazi wengi hulaumu sana kuwa watoto wa siku hizi hawatulii, wakiwa wamesahau kuwa wenyewe ndiyo chanzo cha kuwafanya watoto watoroke kwasababu ya ulinzi mkali nyumbani.
Mtoto hawezi kutoroka nyumbani kama anapata upendo na kueleweshwa mema na mabaya kwa vitendo, pia kwa kumpa na kukubaliana utaratibu wa michezo.
8.Mtoto kukosa ubunifu wenye tija
ya kupambana na changamoto za maisha
Ubunifu
wa mtoto unachangiwa na kuwepo kwa ushirikiano wake na watoto wenzake.Ni hapo
kipaji cha mtoto kinapojidhirisha. Kutokana na mabadiliko makubwa ya sayansi na
teknolojia, wazazi wengi wamewaachia watoto wao kutazama televisheni na komputa
na si kwenda kucheza na watoto wengine.
RAI YANGU:
RAI YANGU:
Naomba
nitoe rai kwa wazazi wa karne hii ambao mnakumbana na changamoto mbali
mbali za mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia kiasi kwamba mnakuwa hamna
muda wa kukaa na watoto, ila ni kutoa amri kuwa hairuhusiwi mtoto kutoka
nje.
Ni vizuri kufuatilia kila hatua ya ukuaji wa mtoto na kuhakikisha yale mahitaji ya hatua husika yanafikiwa, kinyume na hapo tusishangae kuona watoto wetu wamekuwa vile tusivyotarajia.
Ni vizuri kufuatilia kila hatua ya ukuaji wa mtoto na kuhakikisha yale mahitaji ya hatua husika yanafikiwa, kinyume na hapo tusishangae kuona watoto wetu wamekuwa vile tusivyotarajia.
Ungana na mkala yangu nyingine kuhusu "Sababu zinazoweza kumfanya mtoto wako kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya akiwa katika umri mdogo."
Makala hii imeandikwa na Henry Kazula, ikiwa ni utafiti wake binafsi ukisaidiwa na nadharia kutoka tovuti zifuatazo:
Je ni sawa kwa watoto kutumia tabiti ?
23 Aprili, 2013 - Saa 13:56 GMT
Chanzo:BBC SWAHILI
Watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, wana kiu kikubwa kutaka kujua mambo ya teknoplojia mpya.
Kutoka kwa Smart phone hadi kwa tabiti na
michezo ya komputa sio nadra kuwaona watoto wakishika skrini za vifaa
hivyo na kubonyeza kwenye simu.
Hata kama wazazi wanafurahia kimya
kinachojiri wakati anapompa mtoto wake kifaa chochote cha teknolojia
kuchezea, wazazi huwa na wasiwasi kuwa skirini hizi zinaathiri akili za
watoto.
Lakini inaonekana kama skrini zinaweza kuwa na manufaa kwa watoto hasa kwa kusoma na hata kuweza kujua mambo tofauti.
Utafiti wa chuo kikuu cha Wisconsin
uliowasilishwa katika mkutano kuhusu ukuwaji wa watoto, ulionyesha kuwa
watoto walio na umri kati ya miaka miwili na mitatu, wana uwezo wa
kugusa skirini ambazo ni za kuteleza na kuelekeza kuliko zile ambazo
hazina hilo.
Watoto wenye kutumia simu za Smartphones na
Tabiti, wanakuwa bora zaidi ikilinganishwa na wenzao kwani wanafanya
makosa machache na kujifunza haraka pia ikilinganishwa na wenzao.
Hii bila shaka ni afueni kwa wazazi , watoto wenu wanafanya kile kinachokuja chenyewe na kutangamana na dunia.
Hata hivyo teknolojia kwa mfumo wa simu na
tabiti , itasalia kukuwa. Shule nyingi za msingi na shule za chekechea
zimeanza kutumia tabiti katika madarasa ili kuendeleza masomo.
Teknolojia na kuelewa ambavyo vifaa vinafanya kazi pamoja na teknolojia ya mawasiliano ni sehemu ya mitaala ya shule.
"Mimi sio mmoja wa watu walio na dhana kuwa
hatupaswi kuwaruhusu watoto wetu kutumia simu za mkononi na
tabiti,''anasema Helen Moylett, wa shirika linalolenga kuinua viwango
vya elimu miongoni mwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
"vinaweza kuwa vifaa vizuri sana kwa masomo ya watoto kuwasaidia lakini sio wakati wote.''
Lakini wasiwasi wake mkubwa ni kuwa wazazi huwa sio mfano mzuri ambao watoto wanaweza kuwaiga.
''Huwa naona wazazi wakituma ujumbe wa simu ya mkononi wakitembea. Wakati mwingi, wanatumia sana kupita kiasi hadi kutokuwa na muda na watoto wao.''
Mwanasaikolojia mmoja Daktari Aric Sigman,
amekuwa akisema kuwa watoto huja kuzoea vifaa hivyo sana hali ambayo
inaweza kusababisha shinikizo la mawazo kwa watoto wanapopokonywa.
Anasema kuwa watoto watakuwa wametumia mwaka mmoja wakitumia simu au tabiti wakati wanapofika umri wa miaka saba.
Ikiwa ni kweli watu wachache wanaweza kupinga kuwa hoja hii inaogofya.
Inaarifiwa kuwa watoto walio chini ya umri wa
miaka sita kwenda chini, wanapaswa kutumia saa mbili kwenye vifaa hivyo
na hiyo inatosha kwa siku nzima.
Ingawa kuna wachache wanaoonelea kuwa skrini sio nzuri kwa afya ya watoto, hakuna ushahidi kuonyesha kuwa zina athari kubwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni