inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumanne, 25 Novemba 2014

MTAZAMO:


 USITEGEMEE KULIPWA SAWA SAWA NA WEMA ULIOTENDA…

Picha na http://www.simplemindfulness.com/2013/09/29/the-art-of-helping-others/
Watu wengi wamekuwa na mtazamo unaokinzana na ule usemi maarufu wa Kiswahili usemao; “tenda wema uende zako, usingoje shukrani”. Kupitia utafiti wa kimtazamo uliofanywa na Jielimishe Kwanza! Blog kuhusu kutenda mema kwa marafiki au ndugu umebaini kuwa 99.99% ya wanajamii nchini Tanzania hutarajia kurudishiwa wema ule ule waliomtendea mtu mwingine wakati wa shida au raha. Mfano mdogo tu ni wakati wa kutoa mchango wa harusi, watu hutoa mchango wakitarajia kuwa utamchangia vile vile kama alivyokuchangia.
Ifahamike kuwa, unapomsaidia ndugu au rafiki katika shida au raha ni sehemu mojawapo ya wewe kuonyesha ushirikiano na upendo kwa wanajamii kufanikiwa katika maswala mbali mbali.Isiwe kinyume chake kwa kumsaidia mtu na mwisho kutarajia malipo na yasipopatikana kama ulivyotarajia ni matusi na masimango-“eti fulani bwana nilimchangia na kufanikisha shughuli yake…yeye hakunichangia, watu wengine bwana! hawana shukrani!”
Pia inapaswa wanajamii kufahamu kuwa si kila anayekutendea wema umeweza kumlipa vile vile kama ulivyotendewa.Tunasaidiwa au watoto na ndugu zetu wa karibu wanasaidiwa na wengine kwa njia moja hadi nyingine kiasi kwamba tumeshindwa kurudishia wema ule ule.Ikiwa hali halisi ni hiyo, kwa nini sisi tuwe wa kwanza kudai shukrani kutoka kwa wenzetu?
Kiuhalisia ni kwamba tupo duniani ili tufaidiane, hakuna aliye mkamilifu wa kila kitu…hata hao wanasiasa na vigogo hutegemea sana wananchi wawaweke madarakani kwa kutoa ahadi kadha wa kadha, mwisho wa siku huwaacha solemba na kuwadharau kabisa hadi kipindi kingine cha kuomba na kubembeleza uongozi kifike.Sipigii makofi tabia hii hata kidogo! Namaanisha kuwa tuishi na watu vizuri tukijua maana na lengo halisi la kutegemeana na kufaidiana.Isiwe faida ya upande mmoja kila wakati, inapobidi toa shukrani kuthamini mchango wa wengine.Pia tunapotoa msaada au kutenda wema tusidai shukrani, kwa kuwa shukrani ya mtu iliyo ya dhati hugusa dhamiri ya mtu kwa kuzingatia uwezo wa wakati husika.
Nitofautiane pia na mtazamo wa wengine kuwa watendapo wema kwa mtu au watu ni kama wamewekeza; wakitarajia malipo ya shukrani vile vile kwa wema waliowatendea wengine.Ijulikane kuwa tutendapo wema kwa wengine tunajifungulia milango ya baraka kwa njia nyingine…bila kutarajia tunaweza kupata wema zaidi na usiopimika kupitia mlango mwingine kuliko kung’angana na kudai au kutegemea shukrani kutoka kwa wengine.
Hivyo basi, tusikate tamaa ya kuwasaidia wengine kwa kutotarajia malipo kutoka kwao.Tujitoe kwa raha na shida za wengine, wengine kupitia mlango usiofahamika watajitoa kutusaidia tukiwa na raha au shida.
Pia tunaposaidiwa, tuthamini sana mchango wa wengine kwetu; tukijitahidi sana kuwasaidia wengine kwa upendo tu ulio na ushirikiano wa dhati kwa wanajamii wengine na si kwa lengo la kulipiza wema ule ule kwa matarajio ya shukrani.
Imetolewa kwa udhamini wa Jielimishe Kwanza! Social Enterprise.

Jumamosi, 15 Novemba 2014

MTAZAMO:

 USIDHARAU MAMBO YANAYOONEKANA KUWA NI MADOGO…


Ni mara nyingi jamii imekuwa ikipotezea sana masula au mambo yanayoonekana kuwa ni madogo "small things" kwa wakati husika.Inafika wakati natafakari, nashawishika, pia kuchelea kukumbuka na kuikumbusha jamii misemo hii ya Kiswahili inayoonekana kupitwa na wakati kama;  “mdharau mwiba mguu huota tende” na ule wa “usipoziba ufa utajenga ukuta”.
Katika kuendana na wakati, pia uhalisia wa mambo yatokeayo kila siku; misemo hiyo tajwa ina maana kubwa na kwa hakika haijapitwa, wala haitapitwa na wakati abadani.Misemo hiyo au “methali” za Kiswahili zilikuwepo na kutumika kuweka taadhali kwa mambo yanayoonekana kupuuzwa na kuwa ni mzaha ilihali mwisho wa siku madhara yake ni makubwa sana kuliko ilivyodhaniwa awali.
Nchini Tanzania na bila shaka kungineko duniani kuna tabia na mazoea yaliyojijenga ndani ya jamii yenye kupuuza masuala au mambo yanayoonekana kuwa madogo kwa wakati husika.Kuainisha baadhi ya masuala hayo ni kama;
·      kutupa takataka ovyo kwa minajili eti ni kidogo tu ikitupwa nje ukiwa ndani ya chombo cha usafiri haitakuwa na madhara yoyote
·      pia utupaji wa taka ngumu kiholela katika mazingira yetu
·      kuchoma na kukata miti ovyo bila urejeshaji wake
·      kutiririsha maji taka ovyo kwenye bahari na vyanzo vingine vya maji,
·  kutupa taka hewa angani kwa minajili kuwa zitasafiri kwa upepo na kwenda sehemu nyingine zikipungua madhara yake.Taka  hewa hizo ni kama hewa ukaa (CO2), na gesi taka nyinginezo za viwandani na vyombo vya usafiri vitumiavyo mafuta.
Nimeainisha masuala machache yanayochukuliwa kama mzaha na madogo sana kwa wakati uliopo, ila madhara yake ni makubwa kadiri siku zinavyoyoyoma.Madhara ya mambo yanayoonekana kuwa ni madogo hujikusanya kidogo kidogo bila jamii kutambua kwa wakati husika. Chukulia mfano halisi wa tatizo la mmong’onyoko wa udongo unavyotokea; huanza taratibu kwa udogo kuondolewa katika uso wa ardhi- katika eneo moja lililo wazi kwa kukosa miti na nyasi hadi eneo lingine kidogo kidogo kwa upepo na mvua, hatimaye kupelekea kuwepo kwa mabonde na ardhi isiyofaa kwa shughuli mbali mbali.
Pia kuna madhara mengine huripuka na kuiacha jamii na wataalamu kuhaha huku na huko kutafuta tiba ya matatizo yaliyosababishwa na mkusanyiko wa mambo madogo madogo. Mfano mwingine ni huu wa “wimbo wa dunia” wa “mabadiliko ya tabia ya nchi” yapelekeayo kuongezeka kwa joto duniani-kwa lugha ya huko majuu hujulikana kama “climate change” ni matokeo ya shughuli za kila siku za binadamu zenye kupuuza masuala madogo madogo kwa miaka nenda rudi.
Katika kipindi hicho cha kuhaha, msemo mwingine ndani ya jamii wa “kinga ni bora kuliko tiba” hujitokeza kama sehemu ya kujikumbusha uzembe uliotokea awali wa kudharau masuala na mambo yaliyoonekana kuwa ni madogo. Hapa jamii hukumbuka kujikinga na madhara yaliyotokea kwa kudharau mambo madogo.Kampeni nyingi zenye pesa hujitokea ili kuhamasisha mbinu mbadala za kujikinga na madhara yaliyotokana na mambo madogo, pia kujipatia matumaini ya kurejesha hali pendwa ilikuwepo awali.
Kiuhalisia, ni rahisi sana kufanikiwa kupambana na kupata suluhisho la mambo yapelekeayo madhara makubwa katika hali ya awali kabisa-hali ya udogo wake na si kupuuza udogo wake.
Hivyo basi, ni vyema na ni wajibu wa kila mwanajamii kutopuuza hata kidogo mambo au masuala yanayoonekana madogo kwa kujiridhisha upeo wetu kwa wakati husika.
Soma zaidi kujua ni nani anawajibu wa kutunza mazingira kwa kutopuuza mambo madogo madogo yaliyoanishwa.
Imetolewa na Jielimishe Kwanza! Social Enterprise kwa udhamini wa “Ide@Spot” na “Enviro-Forum”

Ijumaa, 7 Novemba 2014

HAMASIKA NA TED VIDEOS: 3 ZILIZOHAMASISHA ZAIDI

1.How schools kill creativity
 (Viewed 25 Million times)
-->
  In this talk Sir Ken Robinson makes an entertaining and profoundly moving case for creating an education system that nurtures (rather than undermines) creativity

-->
2. How great leaders inspire action (Viewed 25 Million times)
-->

-->
Simon Sinek has a simple but powerful model for inspirational leadership all starting with a golden circle and the question “Why?” His examples include Apple, Martin Luther King, and the Wright brothers.

3. Your body language shapes who   you are (Viewed 16 Million times)
-->
 
____________
Samahani wasomaji wetu kwa lugha ya Kiswahili, najua haiwezekani kupata video hizi kwa lugha ya Kiswahili.Lakini ni muhimu sana kujua ujumbe uliopo.Ukihitaji ufafanuzi wasiliana nasi.

Imetolewa na
                                                    Jielimishe Kwanza kupitia TED.
 


Jumapili, 2 Novemba 2014

MTAZAMO:NINI HASA HUKUAMINISHA KUWA HABARI KUTOKA CHOMBO FULANI CHA HABARI NI KWELI?

Ndugu msomaji natumaini u buheri wa afya na yawezekana unaendelea kufuatilia habari kem kem ili hali uwe jirani na dunia.Sambamba na hilo naomba nikukumbushe kidogo kuhusu makala yetu ya siku chache zilizopita kuhusu “je unajuaje kama kila unachoambiwa ni kweli?”  ukizingatia kuwa tunapenda kupata habari mpya kila siku.Tuliona kuwa ni vyema kuchunguza kwa kina na kujielimisha zaidi  kwa kusoma vitabu, makala, majarida mbali mbali na pia kusikiliza hotuba mbali mbali  ili kuboresha upeo wetu katika kupambanua mambo, mwisho wa siku kuweza kujua ukweli wa mambo.Kinyume na hapo tutakuwa ni watu wa kudanganywa tu, mwisho kuchukua maamuzi yasiyo sahihi kwa wakati husika!
Picha;http://www.tmf.or.tz/
Leo nataka nikulete kwenye mandhali hiyo hiyo lakini nikijikita zaidi katika taarifa lukuki tuonazo na kusikia kupitia vyombo mbali mbali vya habari vinavyojulikana na kuheshimika kisheria.
Ama kwa hakika tumekuwa mstari wa mbele kufuatilia kwa makini na kutaka kujua zaidi undani masuala mbali mbali yanayojili na yaliyojili ndani na nje ya nchi kupitia vyanzo hivyo vya habari.Inafika wakati tunabaki njia panda, hasa kwa kupata habari zilizo na mkakanganyiko na uzushi. Wakati mwingine tunagundua kuwa vyanzo vingine vya habari hutoa na kupambisha habari  ili viuze au kuboresha umaarufu wa watu fulani.
Wengi waweza kukubaiana nami kuwa kuna wakati habari tunazosoma kupitia magazeti na majarida…(sina haja ya kuyataja) huweka"headlines" / vichwa vya habari vya kuvutia sana lakini undani wa habari hukinzana kabisaaaa!!!! na hali halisi na matarajio ya msomaji.
Pia kwa upande wa televisheni zetu, ndugu msomaji unaweza kuwa shahidi; kuna mazingira ya habari na matukio yanayoonyeshwa wakati mwingine kwa maslahi ya watu fulani ili kujiimarisha kisiasa na kiuchumi na hata kutaka kuwa maarufu.Lakini ukizingatia na kufanya utafiti wa kutosha utaujua ukweli wa mambo kwa KUJIELIMISHA.
Ndugu msomaji, sina hakika sana kuwa ni mara ngapi umewahi kujiuliza swali hili ambalo leo nauliza; “nini hasa hukuhamasisha kuwa habari kutoka chombo fulani cha habari ukipendacho ni kweli?
Katika kutoa msaada wa kuweza kujibu swali hili ni vyema ukasoma tena makala yetu kuhusu “ je unajuaje kama kila unachoambiwa ni kweli?” utaona mbinu ya kuweza kuchuja habari tupokeazo kwa kusikiliza, kutazama na kusoma.Ila, mbinu kubwa kuliko zote ni ile ya kufuatilia habari husika ukilinganisha na vyombo vingine vya habari visivyopungua kumi…je vyanzo vyote vya habari husika vinasimamia habari hiyo hiyo kama ilivyo? Hapa namaanisha tusichukulie uzito wa habari katika chombo kimoja cha habari, hata kama ni chaguo lako…linganisha habari kwa kuunganisha matukio…kwa msemo maarufu wa lugha ya Malkia wanasema “connecting dots”
Kuwa na mashaka sana kuhusu habari iliyojenga “headline” ...vijana wa mjini hupendelea kuiita “habari ya mjini” kupitia chombo kimoja tu cha habari! Wakati mwingine huwa ni uzushi tu au chombo hicho cha bahari kutaka kumchafua mtu au kikundi cha watu fulani, au kuuza habari…Ichunguze habari hiyo kwa makini sana, Jielimishe Kwanza! ili ufahamu ukweli halisi wa mambo.
Nakutakia usomaji, utazamaji na usikivu mwema wa habari ukijiridhisha kuwepo kwa ukweli ndani yake.
Makala hii imetolewa na Jielimishe Kwanza! Social Enterprise kwa udhamini wa Ide@Spot na Enviro-Forum.
Habari /maulizo:jielimishekwanza@gmail.com