inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumanne, 13 Desemba 2016

MTAZAMO: SHAIRI: "HATUFUNDISHWI SHULENI"


_______________________________
MTAZAMO:SHAIRI
Na Justine Kakoko
Activities: Social & Political activist I Social entrepreneur I Administrator I 
Poet & Song writer based on 
Pan-africanism  Ideology
______________________________________


SHAIRI: "Hatufundishwi Shuleni"

Hutufundishwi Kujiamini/
Hatufundishwi Kujithamini/
Hatufundishwi Kujijua,
Kujitambua Sisi Ni Wakinanani/
Hatufundishwi Tukagundua
Wapi Tulikuwa Kabla Ya
Ukoloni/ Zaidi Ya Kuchukiana
Hatufundishwi Kupendana
Darasani/ Hata Sishangai
Nikisikia, Mwafrika Kuingia
Vitani Kisa Dini/

Hatufundishwi Faida ya
Kuungana/ Hatufundishwi
Umuhimu Wa Kushirikiana/
Kuweka Nguvu Pamoja
Biashara Zilete Maana/
Tunafundishwa Ukilema
Watu Wazima Kutegemeana/
"..Aliyeanguka Sio Wenu.."
Hatufundishwi Kuinuana/

Tunafundishwa Historia
Isiyoandikwa Na Sisi/
Historia Iliyobadilishwa
Historia Isiyonauhalisi/
Tunafundishwa Matatizo
Pasipo Njia Za Kuyatatua/
Inachosha, Yanazidi Ongezeka
Hakuna Linalopungua/

Hatufundishwi Tukajua Kuwa,
Waafrika Tuna maadui/
Kila Nyakati Twawindwa
Si Usiku Mchana Hata Asubui/
Mzungu Njama Nyingi
Katu Mapigo Hayapungui/
Tumechomwa Sumu Tumeachwa
Tunatizama Alama Ya Ndui/

Tunafundishwa Kuigiza Nyendo
Za Mzungu/ Tusichojua Hayomaigizo
Yanaongeza Ukungu/

Hutufundishwi Mifumo Ya Dunia/
Jinsi Gani Inafanya Kazi Ili
Tusije Angamia/ Waongozoji
Kitu Gani Haswa Walichokipania/
Agenda Zao Wapi Zilipolalia/
Hatufundishwi Uozo Wa "Umoja
Wa Mataifa" Nyuma Ya Pazia/
Hatufundishwi Kwanini Mashujaa
Wa Afrika Tunaendelea Kuwafukia/

Tunafundishwa Nadharia Bila Vitendo/
Tunafundishwa Subira, Eti Polepole
Ndio Mwendo/ Tunafundishwa Wagunduzi
Wa Afrika Tuliyoikaa Tokea Mwanzo/
Mambo Ya Vasco Dagama, Historia Ya Kitoto
Tufanye Ukatazo/

Hatufundishwi Jinsi Ya Kujilinda/
Hatufundishwi Jinsi Ya Kuyapinga
Mazito Yanayotushinda/
Hatufundishwi Kukwepa Propaganda
Kuondoka Kwenye Runinga/
Ili Twende Kusoma Tuondoe Ujinga/

Hatufundishwi Tukajijua Kiundani/
Ili Tuwe Imara Kimwili Na Akili
Yatupasa Tule Chakula Gani/
Hatufundishwi Elimu Ya Jinsia
Wengi Tunajifunzia Uwanjani/
Hatufundishwi Mahusiano,
Usione Ajabu Ni Malumbano
Nyumbani/

Hatufundishwi Kwanini Hakuna
Ajira Nchini/ Tunafundishwa Ajira
Zipo Tunasoma Kwa Matumaini/
Hatufundishwi Kujiajiri, Tumalize
Tuishi Kimasikini/ Hatufundishwi
Kujenga Bila Hofu Ya Kuanguka Chini/
70% Ya Vijana Wapo Vijiweni
Baada Ya Kuitimu Vyuoni/
Inabidi Iwe Hivyo Maana
Hatufundishi Kipi Kipo Mtaani/

Hatufundishwi Kwanini Sisi
Ni Masikini/ Masikini Wa Hali Ya
Chini Maisha Yetu Duni/

Kipi Chashusha Kabisa Hali
Yetu Ya Uchumi/ Mbona
Tunawanyama Tele Mbugani..?/
Mafuta Na Madini Yanachimbwa Ardhini...?/
Lakini Hatufundishwi, Kuuliza Kwanini..?/

Hatufundishwi Kuijenga Afrika/
Hatufundishwi Afrika "Mpya"
Nini Inataka / Hatufundishwi
Kuichukia Misingi Iliyotuzika/
Misingi Waliyoijenga
Ili Unyonyaji Usijekatika/
Kiukweli Tunafundishwa Kulala,
Katu Hatufundishwi Kuamka/

Hatufundishwi Kuijua Siasa/
Siasa Inaendeshwa Vipi Ndani
Ya Ulimwengu Wa Sasa/
Tunachofundishwa Ni Akili
Kuzipumbaza/ Hatufundishwi
Kwa Macho Matatu Dunia Kuiangaza/
Kuangaza Marekani Na China Wanavyotuburuza/

Tunahitaji Elimu Yenye Kuiakisi Afrika/
Itakayotuhusu Sisi Na Mazingira
Yanayotuzunguka/ Itakayorekebisha Makosa
Ya Wapi Tulipoanguka/ Itakayotuonyesha Njia
Na Vipi Tutainuka/ Itakayoturudisha Kwenye
Asili Mpaka Tutapojikumbuka/
Elimu Hii Ya Sasa, Elimu Hii Nimeichoka/
Tunahitaji Tufundishwe Historia Yetu/
Tunahitaji Tufundishwe Tamaduni Zetu/
Tunahitaji Tufundishwe Thamani Na Ushujaa
Wetu/ Tunahitaji Tufundishwe Wapi Walipoishia
Babu Zetu/ Ili Juhudi Zao Ziendelezwe Visibezwe
Vizazi Vyetu/ Tunahitaji Tufundishwe Juu Ya Imani
Na Dini Zetu/

Tunahitaji Tufundishwe Kutofautisha
Kati Ya Taarifa na maarifa/
Ili Tusioshwe Ubongo, Uongo Uongo
Usilete Nyufa/
Tunahitaji Tufundishwe Chanzo
Cha Magonjwa Kama Ebola Ona
waafrika Wanavyokufa/

Tunahitaji Tufundishwe Kujiongoza
Tuondoke Utumwani/
Tuhitaji Tufundishwe Ili Tusirudishwe
Mashambani/
Tunahitaji Tufundishwe, Vipi Izalishwe
Isisafirishwe Katani/

Tunahitaji Tufundishwe Kupendana
Waafrika/ Chuki Yatutafuna, Umoja
Hatuna Twaingilika/

Tunahitaji Tufundishwe Manufaa
Ya Elimu Tuipatayo/
Elimu Tuipatayo Ituondoshe
Kwenye Hali Tulionayo/
Elimu Tuipatayo, Ikamilishe Safari
Tuijengayo/
Elimu Tuipatayo Ilishe Wengi
Isiache Wengine Wapige Mwayo/

Tunahitaji Tufundishwe Wizi
wa Warumi Na Wagiriki/
Kubeba Kila Kilichochetu Kusema
Chao Wakadiriki/
Dini, Sanaa, Sayansi, Uandishi,
Vyote Tulianzisha Sisi Hawatuandiki/
Tunafundishwa Uongo, Lakini, Ukweli
Haubadiliki/

Tunahitaji Tufundishwe Haki
Zetu Za Msingi/
Ili Uonevu Uondoshwe Maana
Manyanyaso Ya Polisi Ni Mengi/

Malcolm X Alisema,
"Hakuna Mtawala Anayemfundisha
Mtumwa Kuwa Huru"
Basi Tufundishane Kuikata Minyororo
Ikiwa Kweli Tunauhitaji Uhuru/

-GSP


KUSIKILIZA SHAIRI "Hatufundishwi Shuleni" na 
MASHAIRI MENGINE, JIPATIE CD YAKO-VOL 1- 
TZS 6,000
+255 754 572 143

Jumamosi, 26 Novemba 2016

Tangazo: GREEN TEAM BUILDING


Tangazo: GO-GREEN-EXPO


Please take our apology for extending this important event of our time to 25th-26th March 2017.This is in response to make it more appealing and involve more stakeholders as agreed with some sponsors.
Doors for Exhibition registration with bonus and Sponsorship or Involvement are open till 30th December 2016.
You are welcome to showcase your Green/Sustainable business!
Karibu sana.Dar es salaam, Tanzania
Info: +255 754 572 143
More updates, please follow:
#gogreentanzania #JielimisheKwanza #TGBN #SDGsActionTanzania

Ijumaa, 12 Agosti 2016

SIKU YA VIJANA DUNIANI 2016

“Activista Tanzania” Yawakutanisha Vijana Jjijini Dar es salaam Kujadili Jinsi Ya Kuondokana Na Umasikini Na Jinsi Ya Kuwa Na “Uzalishaji Endelevu Na Matumizi Yenye Tija, hii ikiwa ni kauli mbiu ya mwaka 2016 kwa siku ya vijana Duniani.Ndugu Hatibu Kilenga, Mwenyekiti wa Activista Tanzania akifafanua jambo kuhusu ushiriki wa vijana katika maendeleo.(Picha na Activista Tanzania)Vijana wakifuatilia mada. (Picha: Activista Tanzania)

Kipekee, kwa kuzingatia mchango kwa vijana na nguvu yao katika jamii, Henry Kazula- Mkurugenzi wa kampuni ya “Jielimishe Kwanza” alipata fursa ya kuhudhulia tukio hilo na kuwa miongoni mwa wawezeshaji kwa kutoa mada kuhusu lengo namba 12 kati ya 17 la Maendeleo Endelevu: “Matumizi Endelevu na Uzalishaji wenye tija” (Sustainable Consumption and Production).


Henry Kazula- Mkurugenzi wa kampuni ya “Jielimishe Kwanza” akitoa mada kuhusu “Matumizi Endelevu na Uzalishaji wenye tija”-lengo namba 12/17 Maendeleo endelevu ya dunia 2030.(Picha: Activista Tanzania)


Washiriki wote wakiwa katika picha ya pamoja.(Picha na Activista Tanzania).

Imetolewa na Jielimishe Kwanza Blog

Ijumaa, 24 Juni 2016

MTAZAMO: NUKUU 10 MUHIMU ZA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE KUTOKA KATIKA KITABU CHAKE “TUJISAHIHISHE- MAY 1962”


1.         “Kujielimisha ni kutafuta ukweli wa mambo.”

2.          Ukiondoa matatizo wayapatayo binadamu kwa sababu ya mambo kama mafuriko,nzige,kiangazi,n.k., matatizo yao mengi hutokana na unafsi.

3.         Nitasema kweli daima.Fitina kwangu ni mwiko.

4.         Wengine humwona mwenzao anafanya kosa.Badala ya kumwambia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya.Lakini hawanyamazi kimya kabisa! Watakwenda kumteta katika vikundi vya siri siri.

5.         “Wengine hugawa watu katika mafungu.”Fulani” japo akifanya kosa kubwa sana hasemwi.Lakini “Fulani” wa pili akifanya kosa japo dogo, kosa lile hukuzwa likawa kama mlima Kilimanjaro.”

6.         “Ukweli una tabia moja nzuri sana.Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki.Kwake watu wote ni sawa.”

7.         “Makosa yetu mengine hutokana na woga; woga unaotuzuia kumlaumu mkubwa japo tunajua kuwa kakosa, au kumtetea mdogo anayelaumiwa na wakubwa japo tunajua kuwa hana makosa.”

8.         “Kosa jingine ni kutojielimisha.Kanuni yetu moja inasema: Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu wote na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.Wengine hufikiri kuwa kujielimisha ni kujua kusoma na kuandika.Hilo ni kosa, lakini si kubwa kama la pili.Wengi wetu, hasa baadhi ya viongozi, hufikiri kuwa tunajua kila kitu na hatuna haja kujifunza jambo lo lote zaidi.”

9.         “Watu walio hatari sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu, wala hawana haja kujifunza zaidi.Hii ni tabia mbaya ambayo huzuia kabisa maendeleo.”


10.   “Uvivu wa kutumia akili unaweza kutufanya tutumie dawa kuondoa matatizo ambayo si ya dawa hata kidogo.Daktari asipojua ugonjwa wangu na sababu zake hawezi kujua dawa yake.Akinipa dawa nikapona, atakuwa kaniponya kwa bahati tu, kwa desturi daktari wa namna hiyo hawezi kumponya mgonjwa, na ni daktari wa hatari sana.”Imetolewa na 
Jielimishe Kwanza