inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumanne, 29 Julai 2014

MTAZAMO: TUKIBADILI MTAZAMO TUNAWEZA KULETA MABADILIKO…

Nakuletea makala hii fupi ikiwa ni sehemu tu ya yale yaliyojili siku ya wiki ya maadhimisho ya kuzaliwa shujaa wa Afrika-Nelson Mandela “Madiba” kuanzia Julai,12-18,2014 katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia-Tengeru,Arusha.

Kwa wiki nzima kulikuwepo na maonyesho ya ubunifu wa Kisayansi na elimu za hadhara zikijumuisha wataalam mbali mbali wa Sayansi na Teknolojia kutoka vyuo vya hapa nchini na nje ya nchi.

Nikiwa mwanachuo, nilitembea mabanda mbali mbali ya kibunifu.Nilivutika na ubunifu wa mtaalamu, mjasiriamali Bw. Justin Mungure wa Makumira, Arusha kwa ubunifu wake wa kuibadilisha TOYO ya magurudumu matatu maarufu kwa kubeba mizigo kuwa ya magurudumu manne muonekano kama ule wa gari.
Picha:Muonekano wa pikipiki aina ya TOYO ya magurudumu matatu.
Niliweza kumhoji mtaalamu, ilikuwaje kufikia ubunifu wake? Alijibu; “mara nyingi nimeona TOYO za magurudumu matatu zikianguka kwa kukosa nguvu ya mbele ya gurudumu moja…hivyo nikaamua kuiboresha zaidi kwa kuifanya iwe na magurudumu mawili sawa na nyuma…na sijabadilisha mfumo mwingine wa mashine…”
Picha:TOYO ya magurudumu manne-Ubunifu wa Justin Mungure.

Mungure anifanya kazi hiyo katika karakana yake iliyopo eneo la Makumira-Jijini Arusha.Hubadilisha TOYO ya magurudumu matatu kwa gharama ya takribani shilingi milioni moja na nusu za kitanzania(1,500,000/=) licha ya gharama ya kununua TOYO mpya.
Picha:Justin Mungure akiwa kwenye TOYO yake.

Nilihamasika sana na ubunifu wake ndiyo maana nimependa kukushirikisha ndugu msomaji kuwa tunaweza kubadili mtazamo wa kufikiri na kuamini katika masuala mengi katika maisha yetu ikiwemo jinsi ya muonekano wa vitu mbali mbali na hata yale yahusuyo Teknolojia kwa lengo la
--> kwa lengo la kuboresha ubora na ufanisi.Tunahamasishwa kuwa na mtazamo tofauti wa kufikiri na si kutegemea mtazamo wetu tuliouzoea kila siku na kutegemea matokeo tofauti katika maisha yetu ya kila siku.

Imetayarishwa na kutolewa na 
Jielimishe Kwanza! Social Enterprise.