inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumanne, 13 Desemba 2016

MTAZAMO: SHAIRI: "HATUFUNDISHWI SHULENI"


_______________________________
MTAZAMO:SHAIRI
Na Justine Kakoko
Activities: Social & Political activist I Social entrepreneur I Administrator I 
Poet & Song writer based on 
Pan-africanism  Ideology
______________________________________


SHAIRI: "Hatufundishwi Shuleni"

Hutufundishwi Kujiamini/
Hatufundishwi Kujithamini/
Hatufundishwi Kujijua,
Kujitambua Sisi Ni Wakinanani/
Hatufundishwi Tukagundua
Wapi Tulikuwa Kabla Ya
Ukoloni/ Zaidi Ya Kuchukiana
Hatufundishwi Kupendana
Darasani/ Hata Sishangai
Nikisikia, Mwafrika Kuingia
Vitani Kisa Dini/

Hatufundishwi Faida ya
Kuungana/ Hatufundishwi
Umuhimu Wa Kushirikiana/
Kuweka Nguvu Pamoja
Biashara Zilete Maana/
Tunafundishwa Ukilema
Watu Wazima Kutegemeana/
"..Aliyeanguka Sio Wenu.."
Hatufundishwi Kuinuana/

Tunafundishwa Historia
Isiyoandikwa Na Sisi/
Historia Iliyobadilishwa
Historia Isiyonauhalisi/
Tunafundishwa Matatizo
Pasipo Njia Za Kuyatatua/
Inachosha, Yanazidi Ongezeka
Hakuna Linalopungua/

Hatufundishwi Tukajua Kuwa,
Waafrika Tuna maadui/
Kila Nyakati Twawindwa
Si Usiku Mchana Hata Asubui/
Mzungu Njama Nyingi
Katu Mapigo Hayapungui/
Tumechomwa Sumu Tumeachwa
Tunatizama Alama Ya Ndui/

Tunafundishwa Kuigiza Nyendo
Za Mzungu/ Tusichojua Hayomaigizo
Yanaongeza Ukungu/

Hutufundishwi Mifumo Ya Dunia/
Jinsi Gani Inafanya Kazi Ili
Tusije Angamia/ Waongozoji
Kitu Gani Haswa Walichokipania/
Agenda Zao Wapi Zilipolalia/
Hatufundishwi Uozo Wa "Umoja
Wa Mataifa" Nyuma Ya Pazia/
Hatufundishwi Kwanini Mashujaa
Wa Afrika Tunaendelea Kuwafukia/

Tunafundishwa Nadharia Bila Vitendo/
Tunafundishwa Subira, Eti Polepole
Ndio Mwendo/ Tunafundishwa Wagunduzi
Wa Afrika Tuliyoikaa Tokea Mwanzo/
Mambo Ya Vasco Dagama, Historia Ya Kitoto
Tufanye Ukatazo/

Hatufundishwi Jinsi Ya Kujilinda/
Hatufundishwi Jinsi Ya Kuyapinga
Mazito Yanayotushinda/
Hatufundishwi Kukwepa Propaganda
Kuondoka Kwenye Runinga/
Ili Twende Kusoma Tuondoe Ujinga/

Hatufundishwi Tukajijua Kiundani/
Ili Tuwe Imara Kimwili Na Akili
Yatupasa Tule Chakula Gani/
Hatufundishwi Elimu Ya Jinsia
Wengi Tunajifunzia Uwanjani/
Hatufundishwi Mahusiano,
Usione Ajabu Ni Malumbano
Nyumbani/

Hatufundishwi Kwanini Hakuna
Ajira Nchini/ Tunafundishwa Ajira
Zipo Tunasoma Kwa Matumaini/
Hatufundishwi Kujiajiri, Tumalize
Tuishi Kimasikini/ Hatufundishwi
Kujenga Bila Hofu Ya Kuanguka Chini/
70% Ya Vijana Wapo Vijiweni
Baada Ya Kuitimu Vyuoni/
Inabidi Iwe Hivyo Maana
Hatufundishi Kipi Kipo Mtaani/

Hatufundishwi Kwanini Sisi
Ni Masikini/ Masikini Wa Hali Ya
Chini Maisha Yetu Duni/

Kipi Chashusha Kabisa Hali
Yetu Ya Uchumi/ Mbona
Tunawanyama Tele Mbugani..?/
Mafuta Na Madini Yanachimbwa Ardhini...?/
Lakini Hatufundishwi, Kuuliza Kwanini..?/

Hatufundishwi Kuijenga Afrika/
Hatufundishwi Afrika "Mpya"
Nini Inataka / Hatufundishwi
Kuichukia Misingi Iliyotuzika/
Misingi Waliyoijenga
Ili Unyonyaji Usijekatika/
Kiukweli Tunafundishwa Kulala,
Katu Hatufundishwi Kuamka/

Hatufundishwi Kuijua Siasa/
Siasa Inaendeshwa Vipi Ndani
Ya Ulimwengu Wa Sasa/
Tunachofundishwa Ni Akili
Kuzipumbaza/ Hatufundishwi
Kwa Macho Matatu Dunia Kuiangaza/
Kuangaza Marekani Na China Wanavyotuburuza/

Tunahitaji Elimu Yenye Kuiakisi Afrika/
Itakayotuhusu Sisi Na Mazingira
Yanayotuzunguka/ Itakayorekebisha Makosa
Ya Wapi Tulipoanguka/ Itakayotuonyesha Njia
Na Vipi Tutainuka/ Itakayoturudisha Kwenye
Asili Mpaka Tutapojikumbuka/
Elimu Hii Ya Sasa, Elimu Hii Nimeichoka/
Tunahitaji Tufundishwe Historia Yetu/
Tunahitaji Tufundishwe Tamaduni Zetu/
Tunahitaji Tufundishwe Thamani Na Ushujaa
Wetu/ Tunahitaji Tufundishwe Wapi Walipoishia
Babu Zetu/ Ili Juhudi Zao Ziendelezwe Visibezwe
Vizazi Vyetu/ Tunahitaji Tufundishwe Juu Ya Imani
Na Dini Zetu/

Tunahitaji Tufundishwe Kutofautisha
Kati Ya Taarifa na maarifa/
Ili Tusioshwe Ubongo, Uongo Uongo
Usilete Nyufa/
Tunahitaji Tufundishwe Chanzo
Cha Magonjwa Kama Ebola Ona
waafrika Wanavyokufa/

Tunahitaji Tufundishwe Kujiongoza
Tuondoke Utumwani/
Tuhitaji Tufundishwe Ili Tusirudishwe
Mashambani/
Tunahitaji Tufundishwe, Vipi Izalishwe
Isisafirishwe Katani/

Tunahitaji Tufundishwe Kupendana
Waafrika/ Chuki Yatutafuna, Umoja
Hatuna Twaingilika/

Tunahitaji Tufundishwe Manufaa
Ya Elimu Tuipatayo/
Elimu Tuipatayo Ituondoshe
Kwenye Hali Tulionayo/
Elimu Tuipatayo, Ikamilishe Safari
Tuijengayo/
Elimu Tuipatayo Ilishe Wengi
Isiache Wengine Wapige Mwayo/

Tunahitaji Tufundishwe Wizi
wa Warumi Na Wagiriki/
Kubeba Kila Kilichochetu Kusema
Chao Wakadiriki/
Dini, Sanaa, Sayansi, Uandishi,
Vyote Tulianzisha Sisi Hawatuandiki/
Tunafundishwa Uongo, Lakini, Ukweli
Haubadiliki/

Tunahitaji Tufundishwe Haki
Zetu Za Msingi/
Ili Uonevu Uondoshwe Maana
Manyanyaso Ya Polisi Ni Mengi/

Malcolm X Alisema,
"Hakuna Mtawala Anayemfundisha
Mtumwa Kuwa Huru"
Basi Tufundishane Kuikata Minyororo
Ikiwa Kweli Tunauhitaji Uhuru/

-GSP


KUSIKILIZA SHAIRI "Hatufundishwi Shuleni" na 
MASHAIRI MENGINE, JIPATIE CD YAKO-VOL 1- 
TZS 6,000
+255 754 572 143