inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumanne, 23 Julai 2013

ELIMU: PATA UJASIRI WA KUONGEA MBELE YA HADHIRA!

Picha na images.businessweek.co
Tunapolitazama suala zima la kujieleza mbele ya hadhira si suala rahisi kama hofu itakutawala.Itawale hofu!

Watu wengi ni waoga sana kusimama mbele ya hadhira.Mfano: utamwona mtu anatetemeka mara tu anaposimama mbele ya hadhira au kuongea maneno nusu nusu na hatimaye kushindwa kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira.Je, tatizo ni nini? Tatizo limeanzia wapi?


Awali ya yote kabla ya kueleza MBINU 5 za kukufanya ufanikiwe kujieleza mbele ya hadhira bila hofu, ni vyema tukajua chanzo cha tatizo kupitia maswali  hayo mawili yaliyotajwa.

Tatizo la kuogopa kuongea mbele za watu au hadhira linanzia tangu shuleni, pale mwanafunzi anapochekwa hasa akiwa anaongea mbele ya darasa hivyo kujikuta akikosa ujasiri wa kuendelea kuongea.Hili linawafanya wanafunzi wengine kuogopa kusimama mbele ya hadhira na mwisho hubaki kutupiana mpira wa kujieleza inapofika hatua ya majadiliano na uwasilishaji darasani.

Pia, mfumo wa elimu- mfano nchini Tanzania haujaweka msisitizo wa kutosha kwa wanafunzi kuhusiana na suala zima la kujieleza mbele ya hadhira.Wanafunzi wamekosa ujasiri wa kuelezea vitu walivyoviandika kwa ufasaha katika hali ya kawaida.Hili linatokana na kuwa na mtazamo wa moja kwa moja wa kuandika kwa lengo la kufaulu mitihani na si kuwa ujasiri wa kukielezea walichokiandika kimatendo mbele ya wengine na kupambana na changamoto za maisha ya kila siku.

Athari hii kwa mwanafunzi haishii hapo bali huathiri maisha ya ukubwani.Ndiyo maana utaona watu wengi hushindwa kujieleza kwa ufasaha kwa sababu ya hofu.
Tuje moja kwa moja kwenye MBINU 5 za kuwa na ujasiri wa kuongea mbele ya hadhira:
1. JIANDAE VYA KUTOSHA! FANYA ZOEZI UKIWA MWENYEWE...
Ni vyema kujiandaa kuhusiana na kile unachataiwa kukieleza mbele ya hadhira.Ifahamu hadhira utakayokwenda kuielezea jambo fulani. Usiende kuongea mbele ya hadhira ukifikiria kuwa maneno yatapatikana ukiwa mbele yao.
Unashauriwa kufanya zoezi la kujieleza ukibashiri kama unaongea na hadhira.Kipekee zaidi ukimtazama mtu mmoja akiwakilisha hadhira yote.Hili ni la muhimu sana katika maandalizi, unapaswa kujua kuwa huwezi kukidhi matakwa ya kila mtu.
Inashauriwa uongee ukiwa unajitazama kwenye kioo au ukamwomba rafiki yako akurekodi.Hii itakusaidia kuondoa mapungufu uliyonayo na itakujengea ujasiri zaidi hata utakapokuwa ukiongea na hadhira halisia. 
MUHIMU: Hakikisha unaifahamu hadhira utakayokwenda kuongea nayo, itakusaidia kupanga mbinu za kuwasilisha hoja zako.

2. EPUKA KUKARIRI HOTUBA YAKO KWA KILA NENO…ELEWA!
Si jambo baya kuandika hotuba yako kwenye karatasi au kijitabu, lakini kuwa makini sana wakati wa kutumia ukiwa mbele ya hadhira. Ni vyema kuelewa kile unachotaka kukiwasilisha mbele ya hadhira.
3. EPUKA KUSOMA HOTUBA YAKO NENO KWA NENO
Ukizingatia mbinu namba 2, itumie hotuba yako uliyoandika kwa kujikumbusha sehemu zenye utata.Usiisome hotuba yako…utawachosha wasikilizaji watasema; “ ni vyema angetupatia hotuba yake tukajisomee nyumbani…”
4.  USIOGOPE KUHUSU WOGA WAKO
Itambulike kuwa kila binadamu ana chembe ya woga. Ni vyema kuitambua hofu yako na kujaribu kupambana nayo bila kujulikana na hadhira pia bila kuharibu uwasilishaji wako.
5. USIJIWEKE KUWA MKAMILIFU WAKATI WOTE
Unapaswa kujua kuwa hata waongeaji maarufu wa hadhara hufanya makosa.Hivyo usifikiri kuwa hutakuwa na makosa katika uwasilishaji wako.Ni vizuri ukuamua kurekodiwa kwenye video ili ujitazame baada ya hotuba yako.Itakusaidia kujua makosa uliyoyafanya wakati wa uwasilishaji hivyo kuboresha utendaji wako siku hadi siku.
Sambamba na mbinu hizi, ni vyema pia kuboresha muonekano wako-mfano mavazi nadhifu, uongeaji wako na uhusiano mzuri na hadhira (kuwatazama moja kwa moja).Pia matendo yako yaendane na kile unachotaka watu waelewe.

Nakutakia kila la heri katika kutumia mbinu hizi na kuboresha ujasiri wako wa kuongea mbele ya hadhira. Ukifanikiwa, ni sehemu mojawapo ya kupata ajira na kuwa mahiri katika fani yako...Itambulike kuwa suala la kuongea mbele ya hadhira HUWEZI KULIKWEPA, ipo siku tu utatakiwa kusimama mbele ya hadhira na kutoa neno.

BOFYA HAPA KUTAZAMA VIDEO UONE JINSI UNAVYOTAKIWA KUONGEA MBELE YA HADHIRA...