inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumapili, 21 Aprili 2013

NYUMBANI


Uwanja huu ni kwa kila mtu anayependa kuziishi ndoto zake.Kujielimisha kwanza ni suala muhimu katika maisha yetu ya kila siku.

Kama ule usemi wa wahenga usemao "Elimu ni bahari" au "Elimu haina mwisho", pia kujielimisha hakuna mwisho.

Ningependa kujikita kwa suala zima la kutoa ushauri wa elimu,maisha,kazi,afya,sanaa na mazingira na mfumo wa maisha nikitumia uzoefu na ufahamu wangu nikiambatanisha na tafiti mbalimbali za kitaalamu.

Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikisoma vitabu na majarida mbalimbali na kusikiliza masuala yanayojenga na kuelimisha, kwa hakika sipo vile nilivyokuwa mwanzoni, nimebadilika kifikra, kimtazamo na kiutendaji.

Kuna kitabu ambacho kila mtu anatakiwa kukisoma-"Think and Grow Rich"(Fikiri Uwe Tajiri) cha Napoleon Hill, utatambua siri kwanini si "Work Hard and Grow Rich"(Jitumikishe sana uwe tajiri).Kwanza fikiri, jitumikishe sana mwenyewe kuliko unavyojitumikisha kazini. 

Inaweza ikawa vigumu kunielewa,lakini namaanisha kuwa jiongezee uwezo wako wa utendaji kwa kujielimisha zaidi kuliko unavyojitumikisha kwa mwajiri wako.

Ukiielewa falsafa hii utajikuta unafanya kazi kwa ubora unaohitajika na kipato chako kinaongezeka.

Nikizingatia makundi ya rika zote tutashirikiana kujifunza jinsi ya kuweka malengo,kutunza muda,kutunza pesa,kujiendeleza kusoma kwa bidii na kufahamu vitabu muhimu vya kusoma ili kuboresha ufaulu na utendaji wa kazi.

Nikilinganisha na mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia, kuna tatizo kubwa sana la kuendana na mabadiliko haya.

Mara nyingi mabadiliko huja na fursa.Je,umejipangaje kuzitumia fursa hizo? Kwa pamoja tutaweza kupeana ujuzi na ufahamu jinsi ya kuzitumia fursa na kuziishi ndoto zetu.

Nikimnukuhu mtaalam wa masuala ya Komputa na mvumbuzi wa Kampuni ya "Apple"-Steve Jobs alisema "...There is no reason not to follow your heart" akimaanisha kuwa-"...Huna sababu yoyote ya kutofuata ukipendacho."  



Nakukaribisha uungane nami kuweza kuziishi ndoto zako na si kugombania ndoto ya mwenzio.Kuna ushahidi wa kutosha kuwa Mungu alimuumba kila mtu tofauti na kipawa chenye faida kwa wengine ndani yake.


Karibu!

 
Jielimishe Kwanza!

"It's all about Inspiration"

Utaziishi ndoto zako.

Na Henry Kazula