Mfumuko wa Teknolojia ya mawasiliano na
upatikanaji wa simu za viganjani kirahisi hasa zenye intaneti zimetufikisha
hapa tulipo. Si kwa lengo baya bali jema kabisa endapo tutakuwa na mipaka ya
matumizi na kuchagua vitu muhimu vya kuangalia tukizingatia kutunza wakati.
Tukiendekeza sana urafiki na simu ya mkononi
kwa kuchati…tutajikuta tupo mbali na eneo halisi tulipo.Hii ni hatari, kwa
sababu itamfanya mtu asijue kitu kinachoendelea jirani yake na wakati huo huo akiwa
makini na mambo ya mbali.
Mfano: mtu anakata mazungumzo na mtu aliye naye
jirani na kujikita na mawasiliano ya anga hivyo kushindwa kutimiza lengo la
kuwa jirani.
Hivi sasa, ndani ya familia kumekuwa na
migogoro mingi inayosababishwa na kuendekeza matumizi ya simu kupita
kiasi.Wazazi hawaongei na watoto kuhusu malezi na kumwachia mwalimu aitwae
“Teknolojia ya Habari na Mawasiliano-TEHAMA” afanye kazi yake.
Nikirejea makala yangu kuhusu umuhimu wa
TEHAMA kwa wanafunzi kujifunza ya Jumatano,19 Juni 2013-http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/06/elimu_19.html.Ni vizuri kumtumia
mwalimu huyu, lakini tujue fika kuwa anafundisha kila kitu; mema na mabaya kama
hakuna uangalizi wa kutosha na uelimishaji sahihi wa matumizi ya teknolojia
hii.
Kuthibitisha ukweli wa jambo hili, tazama video ifuatayo;
Kuthibitisha ukweli wa jambo hili, tazama video ifuatayo;
Hili ni angalizo tu, naomba nisieleweke
vibaya…hii ndiyo hali halisi inayoendelea siku hadi siku.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni