inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumamosi, 25 Januari 2014

MTAZAMO: MAMBO TUNAYOSOMA, KUSIKILIZA NA KUTAZAMA YANATUJENGA KITABIA



K
atika maisha yetu ya kila siku tunakutana na mambo mbali mbali, mambo hayo tunayoyaona,kusoma na kusikiliza yana mchango mkubwa katika kujenga tabia zetu kwa njia moja au nyingine.
Mambo yote hayo yanaweza kutujenga na kuonyesha tabia hasi au chanya mbele ya jamii kulingana na mazingira.
Nikimnukuu msanii wa muziki wa kufoka foka nchini Tanzania, Farid Kubanga almaalufu kama 
Fid Q katika wimbo wake wa Propaganda kuna mstari anaimba-“tunajenga tabia kisha tabia zinatujenga” …hii ni kweli kabisa, tabia tunazozijenga kutokana na mazoea mbali mbali kwa kujua au kutokujua, zinatujenga kitabia.
Ijulikane kuwa,tabia ikijijenga ni vigumu kuibadili, ukweli huu ni sawa alivyoimba msanii wa muziki wa mashairi ya kughani Mrisho Mpoto katika wimbo wake wa “Nikipata nauli” kuwa, tabia ni kama ngozi ya mwili hauwezi kuibadili…ni afadhali iwe njema, ikiwa mbaya ni hatari kwa mtu binafsi na Taifa kwa ujumla.
Ikiwa unasikiliza,kusoma au kutazama masuala yenye mtazamo hasi na yenye hali ya hofu ya kutothubutu, ni hakika kabisa kuwa utakuwa ni mtu wa mashaka katika maisha yako.
Pia kuna masuala yanayovuta hisia na faida yake ni kitambo kidogo, haya yote kwa namna moja au nyingine yanajenga tabia ya msomaji,mtazamaji au msikilizaji na hatimaye kupelekea kuonyesha tabia hizo kwa vitendo mbele ya jamii.
Kwa hakika, tabia zetu na matendo yetu ni mazao ya masuala mbali mbali tunayoyasoma,kuyasikia na kuyaona.Hii hutokea pale tu tunapoamua kujifunza na kuyaweka katika utekelezaji kwa mazoea na hatimaye kuwa tabia.Unaweza usiamini haya niyasemayo, kwa sababu yanatokea kwetu bila kujijua…hadi mtu mwingine mwenye kujua tabia za watu atueleze.
Nikitoa mfano mdogo tu wa tabia ya ukatili kwa binadamu wenzetu, hii hutokea kwa mtu kuwa na mazoea ya kusoma,kusikiliza,kutazama sinema/video za watu makatili.Utaniuliza inawezekanaje mazoea yakasababisha mtu kuwa katili kwa wengine? Hii hutokea kwa sababu ya kuchukulia matendo ya watu makatili tunaowaona,kuwasikiliza na kusoma taarifa zao kimazoea katika maisha ya kawaida.Filamu mbali mbali za kikatili huwaaminisha watu kuwa matendo yaonekanayo ni ya kawaida tu ilhali si kweli.
Mfano mwingine ni ule wenye kuchochea tabia njema na yenye maendeleo na kupelekea mtu kubadilika kitabia kutokana na kusoma vitabu vyenye kuonyesha mbinu za mafanikio pia kuangalia filamu zenye kuchochea maarifa na utendaji bora wa kazi, hivyo kuleta maendeleo kwa mtu husika na taifa kwa ujumla.Fuatilia historia ya mafanikio ya watu mashuhuri duniani utagundua ukweli wa jambo hili.
Kufikia hapa unaweza kujichunguza mwenyewe, unapendelea kusoma,kusikiliza,kutazama mambo gani? Je, yana tija ya kukukomboa kiuchumi au yanakufanya uwe msindikizaji ya mafanikio ya wengine? Au yanakupa hofu ya kuchukua hatua ya kuthubutu kuelekea katika safari ya mafanikio? Sambamba na hilo, je unatumia muda katika njia ya kuzalisha faida au hasara? Majibu unayo mwenyewe…Tumia muda huu kuchagua kusoma,kusikiliza au kutazama mambo yanayojenga tabia njema, amini usiamini hutakuwa vile ulivyo sasa.
Nakutakia kila la heri  katika kujiepusha na mambo yasiyojenga tabia njema na kukutisha na kukukatisha tama ya kusonga mbele kimaendeleo…soma,angalia,sikiliza mambo yenye kuchochea mtazamo chanya…utapata ujasiri wa kuleta mabadiliko yenye tija ya maendeleo binafsi na  nchi yako kwa ujumla.
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza! 

Kwa udhamini wa ………………………………..(bofya hapa kuwa mdhamini na ujitangaze zaidi).



Jumanne, 14 Januari 2014

MTAZAMO 2: HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUTUMIA MTAZAMO WA WENGINE KUKUHUSU WEWE NA KUJIONGEZEA UTHAMANI…

-->

It’s what we learn about ourselves from our response that really matters-Marissa Walter
________________________________________________________________________________________

N
dugu msomaji, najua unaambatana nami kuhusiana na makala iliyopita kuhusu unavyojiona, unavyowaona na vile wanavyokuona wengine.http://jielimishekwanza.blogspot.com/2014/01/mtazamo-unavyojiona-unavyowaona-na-vile.html
Kama nilivyoeleza katika makala hiyo kuwa, kuna utofauti wa kimtazamo kwa sisi tunavyojiona ukilinganisha na ule wa wengine.
Moja kwa moja nikulete kwenye jinsi unavyoweza kutumia mtazamo wa wengine kukuhusu wewe na kujiongezea uthamani katika utendaji kazi na maisha ya kila siku.
Zipo njia mbali mbali zitakazokufanya uweze kutumia mtazamo wa wengine kujiongezea uthamani, nitainisha njia tano (5) zinazobeba nyingine;
1.Jitambue uwezo wako wa asili kabla ya wengine hawajakueleza.Hii ni njia muhimu sana…inatengeneza sehemu ya kuanzia kupima mtazamo wako kiutendaji.(Hili huanza na shauku au hamasa iliyo sanjali na uwezo wako wa ndani).
2.Kuwa mwepesi kupokea mawazo kutoka kwa wengine kutokana na mitazamo yao kukuhusu(uwe makini kulinganisha mawazo yako na yao ukisimamia sifa zinazoendana na wewe).
3.Usichukulie kama unadharaulika kutokana na mitazamo ya wengine kuhusu uwezo wako wa ndani…chukulia changamoto wanazozileta kama njia ya kuboresha mapungufu uliyonayo katika utendaji wako.(Tambua kuwa kuna watu wengine wapo kukukatisha tamaa, hawakutakii mema…utawajua kwa kusikiliza mawazo yao ukilinganisha na uwezo wako na mawazo ya wengi kukuhusu wewe).
4.Watumie vizuri watu unaofanana nao mtazamo…hawa watakuimarisha zaidi.
5.Usishawishike kubadisha mtazamo wako kuhusu ulivyo na utendaji kila wakati…hii itakufanya usiwe na msimamo, mwisho wa siku hautakuwa na kitu cha kusimamia na kutambulisha uwezo wako wa asili.Mfano:Ukiwa na shauku ya kuwa mwana mageuzi,kiongozi halafu mtu mwingine akakueleza kuwa huna sifa/karba hiyo na una sifa nyingine tofauti ilihali wengi wanathamini uwezo wako.
Picha na
--> ferociousstrength.com

Lakini mwisho wa siku, cha muhimu zaidi ni vile unavyojiona mbele ya watu wengine.Maoni yao kukuhusu wewe yanaongezea na kujenga uwezo wako kwa njia moja au nyingine kama utayachukulia kwa mtazamo chanya.
Nakutakia kila la heri katika kutumia mtazamo wako na wa wengine katika kuboresha uthamani wako.
Imetayarishwa na kutolewa na 
Henry Kazula
Jielimishe Kwanza!

Ijumaa, 10 Januari 2014

MTAZAMO: UNAVYOJIONA, UNAVYOWAONA NA VILE WANAVYOKUONA WENGINE…

-->
-->
“Person perception refers to the different mental processes that we use to form impressions of other people.” Michal Zacharzewski

W
atu wengi kwa maeneo tofauti wamekuwa wakiamini sana vile wanavyojiona na kujichukulia hasa katika uwezo wa asili wa kupambanua mambo na utendaji. Kujiaminisha huko kunatokana na hisia zao za ndani zinazoendeshwa na dhamiri zao.
Picha na www.elements2lead.com
Mtazamo wa kisaikolojia unadhihirisha kuwa tunavyojiona kwa nje kwa kulinganisha na utendaji wetu wa kila siku ni tofauti na wengine wanavyotuona na kutuchukulia.
Pia tunavyowaona wengine na kujiaminisha kuwa ni uhalisia wao  unakuwa uhalisia wetu kuwahusu wao.Soma hii kujua zaidi kupitia http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/12/mtazamo-taswira-unayowajengea-watu.html
Mwanasaikolojia Kendra Cherry, kupitia http://psychology.about.com/od/socialpsychology/a/person perception.htm anaeleza kuwa kuna hali tatu za kimuonekano zinazopelekea kuwachukulia wengine; tabia ya mtu unayemtazama, mazingira ya tukio na tabia yako mwenyewe.
Tunaweza kujiona tuna kipaji au uwezo fulani na kulizika, lakini kwa upande mwingine bila kujijua tuna uwezo mwingine mkubwa uliojificha ambao hatuuoni ila wengine wanauona.
Tufanye nini sasa ili kujua mtazamo wa wengine kuhusu tulivyo na uhalisia wetu?
Fuatana nasi katika makala ijayo ili ujue upande wa pili unatuchukuliaje ili utumie fursa hiyo kutambua uwezo wako mwingine na kujiongezea uthamani mbele za watu.

Imetayarishwa na kutolewa
Jielimishe Kwanza!


Alhamisi, 2 Januari 2014

MAFUNZO NA AJIRA:FURSA ZA KUJITOLEA NA KUPATA FURSA YA AJIRA

Opportunity to your door, Get this opportunity,Learn to become a skilled Volunteer.Get exposed to employment opportunity.

Volunteers selected to join with Jielimishe Kwanza!
(
Social Enterprises) will get training fee discount of 50% to attend a training on Volunteerism and Professional soft skills for 1st week(full course) and 2nd week (hidden qualities required by employers from volunteers+connection to other working place). Other volunteers will be required to pay 100% of training fee.

Training fee will cover training materials+venue+refreshments.
Apply or Register Now!

Read http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/10/vijana-kujitolea-njia-kuelekea-kupata.html to get some tips on volunteering.