inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Alhamisi, 13 Machi 2014

KAZI NA AJIRA: NAMNA YA KUACHA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAZURI NA SALAMA

-->Na Emmanuel C. Zongwe, kwa msaada wa mitandao. Mwandishi pia ni msomi wa masuala ya Kazi, Ajira na Rasilimali WatuTop of Form.Bottom of Form
+255 717 058 045

E-mail:ezongwe@yahoo.com
 


K
atika masuala ya kazi na ajira, jambo la muajiriwa kuacha kazi ofisi moja na kuhamia ofisi nyingine au kujiajiri ni la kawaida sana. Hii inatokana na mtu kuwa na matamanio ya kuwa na kazi nzuri zaidi, kazi inayolipa zaidi au anataka kuwa bosi wake mwenyewe (kujiajiri). Pamoja na kwamba jambo hili ni la kawaida katika mazingira ya kazi,tatizo lipo kwenye namna unavyoondoka katika ajira yako hiyo. 

Picha na woman.thenest.com
Je, unaondoka ukiacha mazingira salama au unaacha chuki na hasira kwa wengine? Watu wengi hujikuta wakiwa hawana mahusiano mazuri na waajiri wao wa zamani au hata wafanyakazi wenzao wa zamani. Wataalamu wa mambo ya Kazi, Ajira na Rasilimali Watu wanashauri kuwa jambo hili si zuri hasa kama mtu anahitaji kuwa na mtandao mpana wa wanataaluma tofauti    tofauti.
Kwa kuzingatia ushauri huo, hapa nakuletea njia sahihi 6 za wewe kuacha kazi uliyonayo sasa huku ukiacha mazingira salama na yenye kuweka hali ya kutengeneza mahusiano mazuri baadae.

1. Toa taarifa kwa wafanyakazi wenzako - siku uliyotoa taarifa rasmi kwa muajiri wako au siku chache baada, kutana na wafanyakazi wenzako, angalau watatu au wanne, ambao umekuwa ukishirikiana nao vizuri. Hao ni washauri wako wazoefu, ni marafiki wako katika masuala ya kitaaluma, ni watu unaopaswa kuendelea kuwa nao karibu. Waeleze kuwa unaacha kazi hapo, hakikisha pia unawaeleza namna misaada yao kwako ilivyokuwa ya thamani na kama ikiwezekana waeleze kuwa uko tayari kusaidiana nao hata kwa kipindi ambacho hutokuwa nao tena ofisini.

2. Onesha thamani ya ofisi hiyo - kwasababu kazi yako ya sasa na ufanisi uliouonesha hapo ndio chanzo cha wewe kupata ajira nyingine, basi onesha thamani ya ofisi hiyo. Hii ni muhimu hasa kama unahamia ofisi pinzani (competitor). Fanya mawasiliano na muajiri wako wa sasa, mueleze mategemeo yako kwenye ajira yako mpya, pia eleza namna unavyo thamini msaada wake kipindi chote ulichofanya naye kazi.

3. Tafuta mbadala wako - mkufunzi mmoja wa masuala ya Mawasiliano Sehemu ya Kazi, Jodi Glickman, ambaye ni Rais wa kampuni ya Communication Training anasema, "huwa nawahimiza watu wanaoacha kazi watafute watu watakaoziba nafasi zao kabla ya kuondoka". Kama muajiri atakuwa tayari, angalia mtandao wako na chagua angalau watu watatu ambao unahakika kati yao atapatikana mtu sahihi. Mpe muajiri wako mahali pa kuanzia kuziba pengo lako kwa kumpatia orodha ya watu    sahihi      kwa nafasi    hiyo.

4. Ondoka bila kuacha kasoro - hata kama unaona uwezo wako wa kutambua mambo unaweza kuwasaidia wafanyakazi unaowaacha pale, usijaribu kueleza mambo yatakayoacha kasoro pale. Mfano; usijaribu kusema mambo mabaya yamhusuyo muajiri, hata kama ndio yanayokufanya kuacha kazi hapo kwani kufanya hivyo kutaadhiri maendeleo ya taaluma yako. Badala yake eleza mambo chanya na uoneshe thamani ya viongozi wako wa kazi (supervisors).

5. Toa ujumbe wa shukrani
- fanya jitihada za kutuma ujumbe wa shukrani kwa waliokuwa viongozi wako wa kazi ambao kiukweli ndio waliokuwezesha kupata ujuzi mpya na uzoefu wa kazi (experience). Katika ujumbe huo eleza mambo mawili matatu ambayo hakika yalikusaidia sana. Ujumbe huu ni vizuri ukautuma      wiki chache baada ya kuondoka.

6. Fanya mrejeo - hapa namaanisha 'follow up'. Tengeneza namna ya kuendelea kupata habari zozote kumhusu muajiri wako wa zamani au kampuni uliyokuwa ukifanyia kazi. Fanya mawasiliano ya mara kwa mara na wafanyakazi wenzako wa zamani. Panga kukutana nao kwenye chakula cha mchana au wakati wa jioni, baada ya muda wa kazi na jadili nao mambo kadha wa kadha yahusuyo maisha.

Mwisho, hakika hizi njia zitakusaidia sana kuimarisha ukaribu na muajiri wako wa zamani. Ni dhahiri kuwa utapata ushirikiano kwani waajiri wazuri (smart employers) wanaelewa faida za kuwa na mawasiliano mazuri na wafanyakazi wao wa zamani.
Ni muhimu sana kwani hujui kesho na kesho kutwa utamkuta nani utakapokuwa unatafuta ajira nyingine mpya.
Imetolewa na
                                                     Jielimishe Kwanza!Social Entreprises


Jumapili, 9 Machi 2014

BIASHARA: NJIA PEKEE ZA KUPAMBANA NA KUMSHINDA MSHINDANI WAKO KATIKA BIASHARA…(SEHEMU 2)
Huu ni muendelezo wa makala iliyotolewa siku a Alhamisi, 20 Februari 2014, Soma.
Picha na blog.bounzd.com
Kwa kuzingatia maombi ya wasomaji wetu, tumeonelea ni vyema tukamalizia njia nyingine 3 zilizobaki za kupambana na kumshinda mshindani katika biashara,  ikiwa wengi wamejaribu kuzitumia njia mbili zilizotolewa katika makala iliyopita kwa mafanikio ya kuboresha ushindani wa biashara zao.
Nasi bila hiyana leo tunamalizia njia hizo kama ifuatavyo;
 3.Ongeza thamani ya ubora 
Wafanyabishara wengi hufikiri kuwa wakishusha bei zaidi ya mpinzani watalishinda soko, 
La hasha! Ikiwa mfanyabiashara kafikia hatua hii ujue kasahau kuwa, wateja hununua thamani ya kitu kwa lugha ya Kiingereza “value” ikiwa na maana ya kumridhisha mteja na si gharama ya kitu.Chukulia mfano wa bidhaa na huduma za Kampuni ya Apple zilivyo na thamani ya ubora  inayoendana na gharama.
Ingekuwa wateja wanaangalia gharama, hakika watu wachache sana wangeweza kumudu.Ila kwa kuzingatia thamani ya ubora, watu wanajitahidi kumiliki bidhaa na huduma za Kampuni ya Apple.
Hivyo,ongeza thamani ya ubora ikiwa sanjari na ongezeko la bei zaidi ya mpinzani wako…Hakika utalishinda soko!

4.Thamini kila mteja
Usijaribu hata siku moja kumbeza mteja wa aina yeyote ile, huwezi kujua leo kanunua kitu cha sh.1000 kesho atanunua kitu cha sh.10,000 nakuendela.Pia ujue kuwa wateja wako wanachukua sehemu kubwa ya matangazo, tena wanakufanyia matangazo bure! kwa njia ya mdomo…ni kwa sababu umewauzia thamani ya ubora wa huduma na bidhaa. 
Hii ni njia nzuri ya kucheza na saikolojia ya wateja wako, wakati huo huo ukiendelea kumshinda mpinzani wako katika soko.

5.Weka motisha kwa mteja
Njia hii ni nzuri ikiwa unaifuata njia namba 4.Njia hizi mbili zinaendana sana.Bila kujali aina ya mteja, hakikisha unajua kwanza motisha zitolewazo na mpinzani/wapinzani wako.
Mifano tunayo mingi, hebu jaribu kuchunguza makampuni ya simu jinsi yanavyocheza na akili za wateja kwa kuweka vijimotisha kila kukicha.Lengo lao kubwa ni kuhakikisha unabaki kwenye kampuni ya simu husika.Hata kama makampuni yote yanatoa motisha, usihofu!…mteja ndiye mwenye chaguo, atahakikisha anapata motisha kutoka kila kampuni kulingana na huduma itolewayo kwa wakati husika.Nawe hutakuwa na kitu cha kupoteza.

Mwisho, ndugu msomaji na mfanyabiashara nikutakie kila la heri katika kuboresha na kuimarisha biashara yako, usije kulogwa kumchukia mpinzani wako, huyu anakusaidia sana kuboresha biashara yako na kuifanya isibaki kama ilivyo kwa miaka nenda rudi.Hivyo mjue undani wake, Soma na boresha thamani ya ubora.
Kwa ushauri na maelekezo ya biashara, usisite kuwasiliana nasi,
+255 754 572 143

Imetayarishwa na kutolewa na 
Jielimishe Kwanza!

Jumanne, 4 Machi 2014

KAZI NA AJIRA: KUFANYA KAZI KWA BIDII PEKEE HAITOSHI…FANYA KWA MOYO!
“And the only way to do great work is to love what you do”-Steve Job
Njia pekee ya kufanya kazi kwa ufanisi ni kupenda kile unachofanya-Steve Job 
Utendaji kazi na wenye tija ya mafanikio huanzia ndani ya moyo.Mtu anaweza kufanya kazi kwa bidii ila ndani ya moyo wake anasononeka na kuwaeleza wengine kuwa anapata ujira usiokidhi mahitaji yake.Hapa tunasema mtu huyu hana moyo wa kazi…
Picha:www.telegraph.co.uk
Watu wengi hufanya kazi wasizozipenda ilimradi tu wapate kipato kwa wakati husika, pia kwa sababu wamekosa kazi.Naomba nikuhakikishie ndugu msomaji, hakuna kitu kibaya kama kufanya kazi usiyoipenda! Ukifanya kazi usiyoipenda, hata kama unafanya kwa bidii vipi utajiona ni mtumwa tu.
Nikimnukuu Mama Theresa anasema; usitarajie mambo makubwa, tenda mambo madogo kwa moyo- kwa lugha ya kiingereza: “Don't look for big things, just do small things with great love.”Ukitenda mambo madogo kwa moyo ni rahisi sana kukupeleka kwenye mambo makubwa.Anasisitiza tena kuwa; Kufanya kazi pasipo upendo ni utumwa. “Work without love is slavery.”
Hapa nitatengeneza swali, moyo upi tena ikiwa natafuta kipato cha kukidhi mahitaji? Naweza kuliweka hili sawa kuwa, hupaswi kufanya kazi fulani usiyoipenda kwa minajili kuwa  ina kipato kikubwa…kama nilivyosema awali, utakuwa mtumwa wa kipato! Ndiyo maana kila siku wafanyakazi wanalalamika kuwa kipato hakitoshi, hii ni kwasababu wamejikita sana kwenye kuangalia maslahi pekee bila kuonyesha moyo wa kazi, pia hawalinganishi na ubora wa kazi wauletao kwenye soko.Kama alivyosema Jim Rohn kuwa, “watu hulipwa kutokana na uthamani wauletao kwenye soko.”Thamani kubwa zaidi kwenye soko, ujira mkubwa zaidi.Je, utawezaje kuleta uthamani kwenye soko kama huipendi kazi yako?
Ubora wa kazi hauwezi kupatikana kama watu wakitoa udenda kwanza kwenye kipato kabla ya kuonyesha moyo wa kujitoa na kuipenda kazi.Kwa lugha rahisi kabisa, onyesha moyo na nia ya kazi uifanyayo bila kutoa macho makubwa kwenye ujira.
Nimeshuhudia baadhi ya wafanyakazi wanaofanya kwa moyo- mh! Kama ukiwaona ndugu msomaji, unaweza kufikiri wanalipwa ujira mkubwa sana, lakini nilipopata fursa ya kuwahoji, wakanieleza kuwa wanafanya hivyo kwa sababu wanaipenda kazi, yaani wanajiona huru kufanya kazi.
Unaweza usinielewe kwa haraka haraka, fanya jaribio la kuipenda kazi kwanza, onyesha ubora, usinung’unike kama wengi wafanyavyo…utastaajabu kuona kipato kikiongezeka kwa njia nyingine.Utakuwa huru sana kwa sababu unajua sababu ya kufanya hivyo.
Ikiwa hujajua kazi uipendayo; jitathimini, isikilize sauti ya ndani ya moyo wako, chukua hatua ya kubadilika…simaanishi uache kazi, ila tenga muda wa ziada kuifanya kazi unayoipenda.
Kuna wakati mwingine nitakufahamisha faida za kufanya kazi unayoipenda.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Kama unataka ushauri usisite kuwasiliana nasi, 
Barua pepe: jielimishekwanza@gmail.com 
Skype: JielimisheKwanza13
Facebook: Jielimishe Kwanza!
+255 754 572 143