inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Alhamisi, 24 Agosti 2017

Workshop Redesign Your Business Harnessing Green MarketsWorkshop Redesign Your Business Harnessing Green Markets: In a process to Resign Your Business in a Networked societyDigital Innovation...Remember Global market is shifting to Green with enormous opportunities.

You're Invited to attend this Workshop to be aware of;

1.Trending issues in a Networked society and Digital Innovation-Business perspective

2.Trending issues in Global Green Market-The future is Green with unprecedented opportunities.

3.Harnessing Green business opportunities to Green jobs creation and decent jobs

4.Networked society & Digital Innovation-Green business/Market nexus

5.Redesign your business model to Green Business Model(GBM)

Register Today:
+255 754 572 143
or Contact #TGBN Events Manager: Mr.Henry Kazula
e-mail: jielimishekwanza@gmail.com

Alhamisi, 1 Juni 2017

“AZIMIO LA KILIMANJARO” - “KILIMANJARO DECLARATION” LAIBUA HARAKATI ZA KUMKOMBOA MWAFRIKA DHIDI YA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU, UVUNJIFU WA AMANI NA KUTOJALI UTU


Picha: Activista Tanzania
Kufuatia makubaliano ya Azimio la Kilimanjaro au Azimio la Arusha lilioboreshwa-“Kilimanjaro Declaration” la tarehe 23-24 Agosti 2016, washiriki 272  kutoka ndani ya nchi takribani 45 yakiwemo mashirika binafsi, asasi za kiraia,umoja wa wafanyabiashara, wawakilishi wa vikundi vya wanawake na wanaume, Vijana, watu wenye ulemavu, Wabunge na mashirika ya habari, na vikundi vya Dini na Waafrika waishio Nje ya Afrika walikuta Arusha,Tanzania kujalidili mustakabali wa Bara la Afrika linaloaminishwa kuwa ni masikini ilihali lina utajiri wa kutosha lakini watu watu wanaishi maisha duni yenye changamoto mbali mbali zinazohusiana na uvunjivu wa amani, kutojali haki na utu wao kwa maslahi ya wachache.
Mkutano huo mkubwa ulikuja na maazimio makuu sita (6) kama ifuatavyo;
1.    Afrika ina utajiri.Kuitambua Afrika na Kuwaaminisha Waafrika na Dunia kwa ujumla wake kuwa ni Tajiri na Utajiri huo ni wa watu wote na si kwa maslahi ya wachache kisiasa na kiuchumi.Hivyo kupambana kuleta maendeleo ya kiuchumi yenye kujali na kujumuisha maslahi ya kijamii na kujali Mazingira.
2.    Afrika ina vivutio vingi na vya kila aina, vyenye utajiri, hivyo hutosha kujiponya na kurekebisha uharibifu wa kikoloni dhidi ya Waafrika na Mazingira.Pia itambulike kuwa uafrika unamaanisha kuthamini utu wa wengine kupitia falsafa ya “Ubuntu” iliyo fahali na utu wa Mwafrika.
3.    Vijana wa Kiafrika ni msingi imara wa kujenga na kuleta mafanikio katika Bara la Afrika na ni chachu ya kuamsha na kuhamasisha wengine kujua haki na wajibu wa kutenda Haki, kuleta Amani na Kuheshimu wengine.
4.    Waafrika waishio nje ya Afrika bila kujali kuwa wamehamia huko ugenini; ikiwa ni kwa ajili ya utumwa, ukoloni au mfumo wa kisasa wa kuhama ili kutafuta maisha bora wana wajibu wa kutumia mbinu na ujuzi katika taaluma zao kuchangia harakati za kuwakomboa Waafrika wengine dhidi ya umasikini
5.    Waafrika tumejitoa kwa dhati kuwa wamoja, kwa ajili ya mustakabali wa Raia wema baadaye kuwa tutashirikiana kutoa msaada wa kuanzia ngazi ya chini, kuwajengea uwezo viongozi wa Serikali za mtaa na wanaharakati wa ngazi za chini ili kujenga hamasa na msukumo kwa jamii kutoka ngazi chini hadi kuvuka mipaka.
6.    Waafrika tumejitoa kujenga harakati za Kiraia zenye kubeba jukumu la la uwakilishi na kusimamia viwango vya ubora kiutendaji na maadili mema.
Kufuatia maazimio hayo (6) washiriki, kwa niaba ya Waafrika, waliona ni vyema kuanzisha Kampeni za kiuharakati kuanzia ngazi ya Serikali za mtaa, Kitaifa, Bara na Dunia kwa ujumla ili;
a.    kutanua wigo wa kuchukua hatua kuhusiana na masuala ya kijamii na Siasa,
b.    kupigania haki za Wanawake na uhuru wao katika jamii,
c.    kuelekeza juhudi na mapambano yetu kuhusu Haki ya Usawa na kuheshimu utu wa wengine,
d.    kushinikiza watawala kuhusu utawala bora ili kupambana na rushwa na ufisadi,
e.    kushinikiza uwepo wa haki kuhusu masuala ya Tabianchi na Mazingira.
Hivyo basi, mnamo tarehe 25 Mei 2017 jijini Dar es salaam, kampeni ijulikanayo kama “Africans Raising Initiative” chini ya Actionaid Tanzania na Activista Tanzania ilizinduliwa katika kilele cha maadhimisho ya “Siku Ya Ukombozi Wa Mwafrika”-“African Liberation Day”.


Kampeni ya “Africans Raising Initiative” imekuja ikiwa na kauli mbiu “Africans Raising for Justice, Peace and Dignity” ikimaanisha “Waafrika Waamke Kutetea Haki zao, Amani na Utu wao”.
Uzinduzi wa Kampeni hiyo uliambatana na tamasha la jioni kwa Vijana lililofanyika katika kituo cha mafunzo, ubunifu na sanaa kwa watoto na vijana-Kigamboni Community Centre (KCC) kama inavyoonekana katika picha.
Picha zote: Activista-Tanzania
Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa Ripoti ya Makubaliano ya Mkutano.

Imetolewa na Jielimishe Kwanza Blog

Jumatatu, 13 Februari 2017

MTAZAMO: HAKI YA UJINSIA WILAYANI MAFIA MKOANI PWANI: ACTIONAID TANZANIA YAZINDUA MRADI WA KUPAMBANA NA UKATILI DHIDI YA MTOTO WA KIKE SHULENI

Vitendo vya kikatili kwa watoto wa kike shuleni vimeendelea kushika kasi na kushuhudiwa miongoni mwa jamii zetu na kuonekana kuwa tatizo lililokosa mwarobaini. Ukatili huo wa kijinsia dhidi ya watoto wa kike shuleni hujumuisha; kulazimishwa kuolewa katika umri mdogo, mimba za utotoni, kubebeshwa majukumu makubwa ya familia mara tu wanaporudi kutoka shuleni au; unyanyasaji wa kijinsia, kimwili na kihisia.

Ukizingatia takwimu ya Ripoti ya matukio ya ukatili kutoka Halmashauri ya Wilaya Mafia, Januari- Machi 2016 inaonyesha kuwa asilimia 47 ya watoto wa kike Tanzania wanaolewa chini ya miaka 18, sababu inayowafanya waache shule mapema na kuanza majukumu ya familia, ikifuatiwa na mimba za utotoni, Wilayani Mafia pekee, wastani wa wasichana 10 (0.2% ya wanafunzi wote wa kike) huacha shule mapema kutokana na mimba zisizopangwa/ tarajiwa.

Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani imekuwa ni moja ya Wilaya pekee nchini Tanzania kufaidika na mradi mpya unaoendeshwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali –Actionaid Tanzania wa kupambana na Ukatili wa mtoto wa kike shuleni ujulikanao kama “Stop Violence Against Girls in Schools-SVAGS”. Mradi wa SVAGS umekuja wakati muafaka ikiwa hali ya vitendo vya kikatili dhidi ya watoto shuleni ikiwa imeshamiri wilayani humo na kupelekea watoto wengi wa kike kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu.

SVAGS ni mradi wa miaka mitatu (2016-2018) uliozinduliwa rasmi Kitaifa kwa mara ya kwanza jijini Dar es salaam na kuzinduliwa mapema tena mnamo tarehe 10 Februari 2017 katika ngazi ya utekelezwaji Wilayani Mafia mkoani Pwani ukitarajia kuzifikia jumla ya shule 34 ndani ya vijiji 26. Lengo kuu la mradi ni kuhakikisha kuwa haki ya mtoto wa kike kuwa huru, usalama na kupata elimu bora inapatikana, pia ionekane ikitendeka ndani ya jamii  na kulindwa.

Shughuli za mradi-SVAGS zitajikita katika kufanya uchambuzi na uelimishaji umma na kujenga uwezo wa jamii kuhusu aina na madhara ya ukatili dhidi ya watoto wa kike. Pia kuondoa vikwazo vya kisheria vinavyorudisha nyuma juhudi za wanaharakati mbali mbali za kumuwezesha mtoto wa kike kupata haki ya elimu. Mradi upo mahsusi kuzungumizia na kushirikiana na wanajamii kuziondoa changamoto za mila, tamaduni, mitazamo na desturi potofu zinazochochea ukatili dhidi ya mtoto wa kike ndani na nje ya mazingira ya shule.

Akiongea na wadau (walimu wa shule za msingi na sekondari, viongozi wa ngazi ya Wilaya-Mafia, Mbunge wa Mafia) katika hafla ya uzinduzi wa mradi-SVAGS Wilayani Mafia, ndugu Amri Segera, mwendeshaji mradi ActionAid Mafia aliwaomba wadau kuupokea mradi na kuonyesha ushirikiano katika ngazi zote.
Picha: Amri Segera (Kushoto), mwezeshaji na msimamizi wa mradi SVAGS-ActionAid Tanzania, Mafia akiwa na meza kuu kutoka kushoto kwake; Gilbert E.Sandagira-Mgeni rasmi kutoka ofisi za Wilaya ya Mafia, Mhe.Mbunge wa Mafia-Mbaraka K.Dau na M/Mwenyekiti wa Wilaya ya Mafia ndugu Mohamedi J.Gomvu.
Ili kuvuta uelewa wa mradi-SVAGS, washiriki wa hafla ya uzinduzi walipata wasaa wa kujadiliana mara tu mwezeshaji kutoka ActionAid Tanzania ndugu Samwel Mesiak alipotoa utangulizi na kuboresha uelewa wa mradi.
Picha: Samwel Mesiak, mwezeshaji kutoka ActionAid Tanzania-Dar es salam akiwasilisha mada kuhusu historia na malengo ya mradi mpya-SVAGS.
Picha: Mzazi, pia mwakilishi wa kikundi cha akina mama Jojo Wilayani Mafia akieleza changamoto ya kulea watoto wa kike nyumbani na shuleni inayopaswa kuzingatiwa ili kufanikisha utekelezaji mradi mpya wa SVAGS.
Picha: Mzazi na Mwalimu katika Wilaya ya Mafia akiongea kwa msisitizo kuhusu kukabiliana na changamoto zilizopo ndani ya jamii ili kuhakikisha mradi mpya wa SVAGS unakuwa jumuishi na kufanikiwa kwa ushirikiano wa wadau wote Mafia.
Ilikuwa ni wasaa wa mbunge wa Mafia kuchangia na kujibu hoja mbali mbali zilizoletwa mezani kwa ufafanuzi zaidi.
Picha: Mhe. Mbunge wa Mafia Mbaraka K.Dau akifafanua jambo kuhusu maoni ya baadhi ya washiriki kuhusu utekelezwaji wa mradi mpya-SVAGS wa kupambana na ukatili dhidi ya watoto wa kike wilayani Mafia. 
Ulifika wakati muafaka wa kuashiria kuzinduliwa kwa mradi wa SVAGS ambapo Samwel Mesiak kwa niaba ya ActionAid Tanzania alikabidhi nakala ya mradi-SVAGS kwa mgeni rasmi ndugu Gilbert E. Sandagira kutoka ofisi ya Wilaya Mafia mkoani Pwani.
Picha: Samwel Mesiak wa ActionAid Tanzania akimkabishi mgeni rasmi-Gilbert E.Sandagira nakala maalum ya mradi SVAGS kuashiria uzinduzi rasmi na ukuanza kwa utekelezwaji wa mradi-SVAGS wilayani Mafia.
Picha: Mgeni rasmi kutoka ofisi za Wilaya Mafia ndugu Gilbert E.Sandagira akisoma kwa makini nakala ya mradi SVAGS utakaotekelezwa Wilayani Mafia.

Picha: Mgeni rasmi kutoka ofisi za Wilaya Mafia ndugu Gilbert E.Sandagira akishangiliwa na wajumbe pamoja na washiriki wa hafla ya uzinduzi kuashiria kukubalika kwa mradi SVAGS wilayani Mafia.
Mwisho wa yote ilikuwa ni furaha kwa washiriki wote kupata picha ya pamoja kabla ya kwenda kupata chakula cha mchana kwa pamoja.
Picha: Washiriki wote wa hafla ya uzinduzi wa mradi SVAGS wilayani Mafia katika nyuzo za furaha kuhakikisha kuwa wameupokea mradi-SVAGS na kuutekeleza kwa vitendo.

Imetolewa na "Jielimishe Kwanza" kwa niaba ya ActionAid Tanzania-Mafia

Jumanne, 24 Januari 2017

MTAZAMO: HAKI YA MWANAMKE KUMILIKI ARDHI- BARAZA LA WANAWAKE VIJIJINI (RWC) LATEKA HISIA ZA BARAZA KUU LA UMOJA WA AFRIKA (AUC)


Ikiwa ni siku chache kabla ya Mkutano mkuu Wa jinsia Wa Baraza kuu la Umoja wa Afrika (AUC) unaotarajiwa kuanza tarehe 22-25 Januari 2017 jijini Addis Ababa-Ethiopia, Shirika la “Action Aid Tanzania” kwa kushirikiana na Mtandao Wa Jinsia- “Tanzania Gender Networking Programme” (TGNP)-Mtandao wamekutana kwa pamoja kujadili mafanikio makubwa ya kuundwa kwa Baraza la Wanawake Vijijini-The Rural Women Council (RWC) lililoundwa mwaka 2012.


Moja ya mafanikio, na kubwa kuliko yote ni lile la Baraza la Wanawake Vijijini (RWC) kutambuliwa na  Baraza kuu la Umoja wa Afrika (AUC) hadi kufikia hatua ya kutoa mwaliko kwa Bi. Flora Mathias Mlowezi ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la hilo kwa Afrika Mashariki, pia ni mwanaharakati wa masuala ya Jinsia kutoka “TGNP’s Tigushe Knowledge Center in Mbeya rural district” ili kuwakilisha sauti za vilio vya wanawake wengi vijijini kuhusu Haki yao ya msingi kumiliki Ardhi nchini Tanzania na Afrika ya Mashariki kwa ujumla.

  
Picha: Bi. Flora Mathias Mlowezi: Mwenyekiti-Baraza Afrika ya Mashariki na
Mwanaharakati- “TGNP’s Tigushe Knowledge Center in Mbeya rural district" kutoka Tanzania.

Licha ya kutetea maslahi za wanawake wengi waliopo vijijini katika haki yao ya kumiliki Ardhi; Bi Flora anakuwa ni miongoni mwa wanawake shupavu walioweza kushiriki Kampeni maalumu ya kupanda mlima mrefu Afrika-Kilimanjaro kupitia kampeni “Kilimanjaro Initiative” iliyoasisiwa na 

Baraza la Wanawake Vijijini-The Rural Women Council (RWC) mnamo Octoba 2016 chini ya uangalizi wa TGNP-Mtandao wa Jinsia na Action Aid Tanzania jijini Arusha-Tanzania.


Kupitia mkutano mdogo wa wadau wa kutetea masuala ya haki ya mwanamke kumiliki Ardhi kutoka TGNP- Mtandao wa Jinsia na Action Aid Tanzania uliofanyika jijini Dar es salaam tarehe 21/01/2017, washiriki walilenga kumjengea uwezo na kumpa ujasiri Bi.Flora ili kuwa na uelewa wa kutosha katika kuwawakilisha wanawake wote wa vijijini nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla wake.


Picha: Wajumbe katika Mkutano mdogo wafuatilia jambo kutoka kwa Mwenyekiti wa kikao.
  
Suala la msingi linalomfanya Bi.Flora kwenda kuwakilisha sauti za wanawake wengine kuhusu haki ya kumiliki Ardhi, ni lile la kutoa ufafanuzi wa kina wa tamko la madai ya wanawake wote wa vijijini lililowasilishwa Octoba 2016 kwa Mwenyekiti wa AUC. Hivyo, itakuwa na wasaa mzuri kwa jitihada hizo za Wanawake waishio vijijini kuweza kusikilizwa katika masikio ya viongozi, watunga sera na wasimamiaji sera kutoka mataifa mbali mbali barani Afrika na jumuiya nyingine za Kimataifa.

 
Picha: Mwenyekiti wa kikao akiwasilisha Tamko la Madai lililotokana na Kilimanjaro Initiative ya Octoba 2016.

Dhana ya kutoa kipaumbele kwa wanawake waishio vijijini ilikuja kutokana na kuwepo kwa 70% ya wanawake wanaoishi vijijini ukilinganisha na mjini, pia idadi hiyo kubwa inawahusisha wanawake walio wengi wanaotegemea Ardhi kama rasilimali ya kuendesha maisha yao ya kila siku kama vile kilimo na ufugaji.

Imetolewa na Jielimishe Kwanza kwa niaba ya Action Aid Tanzania jijini Dar es salaam.