inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Ijumaa, 30 Agosti 2013

MUDA WA KUIPIGIA KURA BLOG YETU UIPENDAYO UMEONGEZWA...PIGA KURA KADIRI UWEZAVYO

HUU NI UTHIBITISHO WA E-MAIL KUHUSU ONGEZEKO LA MUDA WA KUPIGIA KURA BLOG YETU UIPENDAYO KAMA ULIVYOTOLEWA NA SHABIKI ALIYEIPIGIA KURA BLOG YETU
_________________________________________________________________________________
We wish to express our gratitude for taking your time to nominate this blog. We are pleased to acknowledge that your nomination file is compete. Don't forget to vote for your favorite blogs.
Voting is open to everyone from September 8th to 14th, 2013.

Sincerely,

Tanzanian Blog Awards Admin
_________________________________________________________________________________ KUENDELEA KUPIGA KURA FUATA HATUA KUPITIA:


 AU

UKURASA WETU WA FACEBOOK

Alhamisi, 29 Agosti 2013

TUZO KWA BLOG BORA 2013. TAFADHARI TUNAOMBA USHIRIKI WAKO KUIPIGIA KURA BLOG HII www.jielimishekwanza.blogspot.com



 JINSI YA KUSHIRIKI... 
HAKUNA GHARAMA YA KUSHIRIKI!

http://tanzanianblogawards.blogspot.com/

1. Unaweza kuipendekeza blog yetu www.jielimishekwanza.blogspot.com katika vipengele vingi upedavyo lakini katika kila email unayotuma ni blog moja tu utaruhusiwa kuipendekeza kwa wakati mmoja

mfano:  NENDA ENEO LA KUANDIKA E-MAIL

Kwenye subject unaandika jina la blog YETU: www.jielimishekwanza.blogspot.com

Kwenye body ya email unaandika vipengele unavyotaka blog yetu www.jielimishekwanza.blogspot.com ishirikishwe kutokana na maudhui yake:



VIPENGELE:
  • Best Newcomer Blog
  • Best Inspiration Blog
  • Best Creative Writing Blog
  • Best Educational Blog
  • Best General Blog
2. Email yako iwe ni ya ukweli, waandaaji wanaweza  kuwasiliana na wewe kuhusu link ya blog uliyopendekeza ili waweze kufanya hivyo na 

Tuma mapendekezo yako kwa hii hapa 

Email : nomination@bloggersassociationoftanzania.com 
au          tanzanianblogawards@gmail.com
3.Mwanzo wa kupokea mapendekezo hayo ni Tarehe 17/8/ 2013 saa 12:01am mpaka tarehe 30/8/2013 saa 11:59pm saa za Africa mashariki

TUNASHUKURU KWA USHIRIKIANO!

Jumatano, 28 Agosti 2013

MTAZAMO NA UCHUMI: JINSI YA KUWA NA MALI KWA KIPATO KIDOGO ULICHONACHO…

Picha  na endoftheamericandream.com
Hivi umewahi kujiuliza kwa nini matajiri wanaendelea kuwa matajiri wakati huo huo masikini wanaendelea kuwa masikini?
Tofauti kati ya makundi haya mawili ni kwamba, matajiri wanawekeza zaidi kwa kutumia pesa zao wakati huo huo masikini wanatumia ovyo kwa kile wanachokipata.
Nikilinganisha hali hii kihistoria, hasa maisha ya zamani ya babu na bibi zetu kutegemea uwindaji, ilikuwa ni hali iliyozoeleka kwa wanaume kuaga familia zao asubuhi na mapema kwenda kutafuta kitoweo.Hii ilikuwa ni hali ya kila siku ili kuweza kukidhi haja ya siku husika.
Kwa jamii za wale waliogundua siri ya kujilimbikizia mali waliamua kutengeneza boma la kuhifadhia wanyama waliowategemea kwa mlo…hapa ufugaji ukaanza, kwa lengo la kujiepusha na usumbufu wa kwenda kuwinda mara kwa mara pia uhaba wa wanyama kwa msimu fulani.Baada ya muda fulani wanyama waliowafuga walizaliana na hatimaye kukidhi hitaji la kitoweo pia kuuza kwa wengine wasiokuwa na maono ya kujilimbikizia kwa ajili ya baadaye.
Historia inatufundisha kujiwekea akiba ya baadaye na si kuangalia maisha ya leo.
Kuna hatua mbili (2) muhimu wanazotumia watu wenye mali nyingi na kuendelea kuwa jinsi walivyo:
1.KUWA NA MAAMUZI SAHIHI YA KUTUMIA PESA KATIKA NJIA SAHIHI... mfano kununua kitu kwa kusudi maalumu na si kwa sababu imetokea tu au kwa sababu mtu mwingine anacho au tu kwa mashindano..la hasha!
2.KUJENGA “BOMA”
Kama nilivyotoa mfano wa kihistoria kuhusu maisha ya watu wenye mali waliowahi kuishi, kwa maisha ya leo kuna mifumo mbali mbali ya kuwa na boma nayo ni;
·  KUJENGA BIASHARA
· KUTUNZA PESA (AU KUTUNZA VITU VINAVYOWEZA KUTHAMANISHWA NA PESA WAKATI PESA IKIHITAJIKA)
· KUJIHUSISHA NA KUNUNUA VIWANJA, NYUMBA NA KUKODIAHA/KUPANGISHA AU KUUZA KWA FAIDA
·    KUWEKEZA KWENYE SOKO LA HISA

Makala hii imeandaliwa na Jielimishe Kwanza! kwa kushirikiana na kitabu alichoandika mjasiriamali maarufu nchini Marekani Robert Kiyosaki-“Be Rich & Happy”  Sura ya 19 ukurasa wa 195.  

Ikiwa unahitaji kitabu hicho tuwasiliane kupitia 0754 572 143.Ikiwa unaona uvivu kusoma kitabu, fuatilia mbinu za kuanza kusoma kitabu kwa mafanikio kupitia http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/elimu-na-mtazamo-mbinu-10-za-kuanza.html
Usipuuze ushauri huu, kumbuka maneno ya tajiri mkubwa -Henry Ford, mwanzilishi wa kampuni ya magari aina ya Ford alisema; 

"PAYING ATTENTION TO SIMPLE LITTLE THINGS THAT MOST MEN NEGLECT MAKES A FEW MEN RICH " -Henry Ford



Jumanne, 27 Agosti 2013

VIJANA KATIKA VIKUNDI: KIKUNDI KINACHOUNDWA NA WAHITIMU WA SHULE YA SEKONDARI LUGALO IRINGA 2001 TANZANIA CHATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA “CHAKUWAMA”

-->
Katika kuadhimisha sherehe ya kutumiza mwaka 1 siku ya Jumapili 25 Agosti 2013 kikundi hicho kijulikanacho kwa jina la “LUGALO GRADUATES’ NETWORK ASSOCIATION -2001” kilichoundwa na vijana waliosoma Shule ya sekondari Lugalo Iringa- Tanzania kilionelea ni vyema kuwajibika katika kutoa mchango kwa jamii ikiwa ni sehemu mojawapo ya malengo ya kikundi.
Kikundi hicho chenye wanachama hai 18 chini ya uongozi wa Mwenyekiti-
Henry Kazula kiliweza kutimiza adhma hiyo kwa kuwatembelea na kutoa msaada wa vifaa vya matumizi ya kawaida vyenye thamani (shilingi laki moja) sh.100,000 kwa watoto yatima wa kituo kiijulikanacho kwa jina la CHAKUWAMA kilichopo Sinza-Meeda jijini Dar es salaam.
Wakiongea na Jielimishe Kwanza! wanakikundi hao walieleza kuwa lengo kuu la msaada huo ni kushiriki kwa pamoja na kikamilifu kwa mali na hali katika shughuli za kijamii kwa kile wanachokikusanya kutokana na michango yao ya kila mwezi.
Pia walisema wamefanya hivyo kuweza kutoa changamoto kwa wanajamii wengine kujitoa kwa hali na mali kusaidia watoto yatima na si kusubiri hadi watu watoke nje ya nchi kutoa misaada.
Hii ni kutokana na matatizo kadha wa kadha ndani ya vituo vya kulea watoto yatima ikiwa ni huduma mbovu za afya,ufinyu wa malazi na ukosefu wa wataalamu wa kuwafundisha watoto hao malezi bora na stadi za maisha.
Wakiungana kwa pamoja na Jielimishe Kwanza! wanatoa rai kwa jamii kulivalia suala hili njuga ili kuijenga jamii ijayo yenye maadili na tija kwa Taifa.
Walitoa angalizo kuwa kutowajali na kuwapuuza watoto na vijana waishio katika mazingira magumu kunaandaa jamii/kundi hatari sana kwa Taifa hapo baadaye.
Wasiliana na kikundi hicho kupitia 0785 175 157 au andika kupitia jielimishekwanza@gmail.com
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!

Jumatatu, 26 Agosti 2013

BIASHARA: UKITAKA KUJENGA BIASHARA IMARA NA YENYE MAFANIKIO FANYA HIVI…



Kumekuwepo na changamoto nyingi kwa wafanyabiashara wadogo pia hata wale wanaolekea kuwa na biashara kubwa.Moja ya changamoto kubwa kwa biashara ndogo na zilizoanza ni kushindwa kukuza soko la biashara na faida ndogo iliyo tofauti na malengo ya mmliki/wamiliki wa biashara fulani.Pia mitaji midogo ni changamoto nyingine inayodidimiza kupanuka kwa biashara ndogo.
Tukitambua na kuzitumia changamoto zilizopo kama sehemu ya kusimamia ni vyema tukashirikishana kwa pamoja mbinu 10 mbadala za kuboresha biashara zetu kwa mafanikio tarajiwa kwa muda tuliojipangia.

1.ANDIKA NA UFUATE MPANGO WA BIASHARA “Business plan”
Ukiwa na wazo la biashara ni vyema ukafanya upembuzi yakinifu kupitia mpango wako wa biashara.Kupitia mpango huo wa biashara uliouandika utaweza kupunguza hatari zilizopo katika biashara yako,pia utaona ni kwa njia ipi utapata faida na utajua muelekeo wa biashara yako kuliko kuingia kichwa kichwa katika biashara.
2.PENDA KILE UNACHOKIFANYA, utakifanya kwa bidii…Kama Steve Jobs- mjasiriamali, mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya "Apple Computers na Pixar Animation" alivyosema; “huna sababu ya kutofuata ukipendacho” Hii ni muhimu sana kwa biashara changa.
3.IFANYE BIASHARA YAKO KUWA NA HUDUMA AU BIDHAA ZA KIPEKEE
Kufanikisha hili fanya utafiti wa soko la bidhaa na huduma za washindani wako, BORESHA! ukijitofautisha nao ila ukihakikisha unakidhi mahitaji ya wateja wako.
4.HAKIKISHA UNAWASHIKA WATEJA WAKO…fanya hivi ukichukulia kama wamekuja ofisini kwako kwa mara ya kwanza…usiwachukulie kimazoea na kuwapuuza.Hili ni muhimu sana kwa wateja wa mwanzo kwa sababu wanakwenda kukufanyia matangazo bila gharama yeyote.
5.TENGENEZA WIGO WA SOKO LAKO
Hakikisha unalenga wahusika wa aina fulani.Mfano.Kama unauza nguo za jaribu kujitofautisha na wengine kwa kuzingatia rika na jinsia.Hii itakusaidia kuitofautisha biashara yako na wengine hivyo kuwa na wigo wa uhakika wa soko lako kibiashara.
6.JITENGENEZEE MTANDAO MZURI…zingatia ushirikiano wa kibiashara wenye kufaidiana kibidhaa au kihuduma.Mfano kampuni moja haiwezi kuwa na kila kitu, ni lazima itahitaji huduma au bidhaa kutoka kampuni nyingine…hii nisehemu nzuri ya kutenga mtandao mzuri ukiwa makini kuangalia fursa.
7.WEKA LENGO LA KUIFANYA BIASHARA YAKO KUKUA IKIWA NA FAIDA ENDELEVU…
Tukizingatia ushauri wa wafanyabiashara…inatambulika kuwabiashara imara na yenye tija ya faida endelevu ni ile inayokuwa kulingana na muda na malengo ya kukua.Inatarajiwa kuwa biashara iliyokuwa inahusisha kutembeza bidhaa inaweza kuonyesha hali ya kukua hasa kwa kumiliki duka la bidhaa.
8.SOMA ALAMA ZA NYAKATI
Ni vyema kujua aina na wakati wanapopatika wateja wako kulingana na aina ya bidhaa au huduma yako. Usifanye biashara kimazoea ukiwa na lengo la kukuza biashara yako.Hakikisha unabadilika kulingana na mazingira…na hii ni sifa mojawapo ya mjasiriamali.
9.THAMINI NGUVU YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO
10.USIKATE TAMAA PALE UNAPOPATA HASARA...tumia mapungufu yako kujiboresha zaidi.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!

Jumamosi, 24 Agosti 2013

VIJANA NA MTAZAMO: MTAZAMO HUU UTAKUFANYA UFE MASIKINI…BADILI MTAZAMO!

-->
Picha na http://madonnarobinson.com
Bila shaka umewahi kusikia vijana wengi wakisema hivi “umri bado unaruhusu” au “mimi bado mdogo” kuhusiana na suala zima la maisha ya kujitegemea na hata uthubutu wa kuelekea kwenye uwekezaji pia kuwa na mali.
Nikilinganisha mtazamo huo na misemo ya Kiswahili kama “Chelewa chelewa utakuta mwana si wako” na “ujana maji ya moto” yenye mantiki ya kuchukua hatua mapema bila kujali hali ya umri ulionao au maisha yaliyopo naona kuna haja ya kubadilisha mtazamo.
Sanjali na hilo pia kuna msemo huu wa Kiingereza uliozoeleka sana midomoni mwa watu- “Life is not a rehearsal, is a performance” ni ukweli usiopingika kuwa tunatakiwa kuonyesha kiuhalisia jinsi tunavyoishi na si kujaribu au kuigiza.Natumaini umejua namaanisha nini? 
Hivyo basi tunatakiwa kuchukua hatua ya uthubutu wenye tija-SOMA HII http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/06/vijana-na-maisha.html ili kujinasua hapo tulipo na si kunung'unika huku tukisubiri tuzeeke na kutumainia malipo ya uzeeni…wakati wa kuwekeza ni sasa kwa sababu tuna nguvu, ari na akili inafanya kazi kwa haraka.
Fanya mabadiliko sasa kupunguza tatizo la utegemezi ndani ya familia na jamii kwa ujumla.
Vijana Taifa la Leo na Kesho!
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!

Jumapili, 18 Agosti 2013

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KATIKA UTOAJI WA TUZO KWA VIJANA CHINI YA MIAKA 30 “Under -30 Youth Awards 2013” WALIOFANYA VIZURI KATIKA NYANJA MBALIMBALI ZA KUTOA MCHANGO KWA JAMII.

-->
Jumamosi-Agosti 17, 2013 ilikuwa ni kilele cha siku ya kutunuku tuzo kwa vijana kama ilivyokuwa imepangwa na “Youth for Africa (YOA)” ikishirikiana na wadhamini mbali mbali.Soma undani wa maandalizi hadi kuifikia siku hii kupitia http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/zoezi-la-kutunuku-tuzo-kwa-vijana-chini.html
Ilikuwa ni siku nzuri iliyogubikwa na shamra shamra, burudani zenye kuhamasisha vijana wengine na jamii kwa ujumla kuhusu kutumia vipaji na uwezo binafsi kuwa na uthubutu kugusa maisha ya wengine.Ikiwa ni sanjari na kauli mbiu ya YOA –“Born talented living to do it.” Naweza kuongezea kwa kusema…and influence other talented to do it!
Mgeni rasmi wa tukio hilo Mhe. Januari Makamba(MB) aliwaamasisha vijana kuhusu kusoma vitabu ili kujiongezea uwezo na kuboresha mtazamo wa kufikiri na kubuni mbinu mbali mbali kupambana na changamoto za maisha.Kwa kuzingatia umuhimu wa kusoma vitabu, Jielimishe Kwanza! imeliona hilo mapema na kutoa njia mbali mbali za kufanikisha kujisomea.Ukitaka kujua umuhimu na siri iliyopo ndani ya vitabu soma hii: http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/ifahamu-siri-iliyopo-ndani-ya-vitabu.html?spref=bl  na pia jinsi ya kuanza kusoma kitabu kwa mafanikio soma hii http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/elimu-na-mtazamo-mbinu-10-za-kuanza.html.
Naomba kutoa rai kwa wazazi kuanza kuwajengea uwezo watoto wao kujisomea vitabu...soma hii zaidihttp://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/elimu-na-malezi-mjengee-mtoto-wako.html
Pia Mhe.Januari Makamba(MB) alitoa pongezi kwa Asasi isiyo ya kiserikali -YOA http://www.yoa.or.tz/ ikishirikiana na wadhamini mbali mbali kwa kutambua uwepo wa vipaji na kuandaa tukio hilo kubwa.
Tuzo hizo zitakuwa zikitolewa kila mwaka kwa kuzingatia maboresho zaidi ili ziwe na tija zaidi hasa kuwahamasisha vijana wa Kitanzania na Afrika kwa ujumla kubadili mtazamo wa kufikiri kwa kuijenga Afrika huru.
MATUKIO KATIKA PICHA:


Timu nzima ya YOA wakiwa na Mhe.Januari Makamba (MB).

Jumatano, 14 Agosti 2013

VIJANA NA MAISHA:KWA SIFA HIZI, KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 18-35 NI TAJIRI!

-->
Kupitia makala kuhusu vijana na maisha-KWA HIZI SIFA 10, KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 18-35 UNAKARIBIA KUWA TAJIRI! Nilieleza sifa hizo kwa kuzingatia mifano ya matajiri vijana maarufu duniani, nilitoa mfano wa mjasiriamali pia mwanzilishi mwambata wa mtandao wa kijamii-Facebook Mark Elliot Zuckerberg. Soma http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/vijana-na-maisha-kwa-hizi-sifa-10.html
Huyu ni kijana mwenzetu, Mtanzania, mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa akiwa ni
   Patrick Ngowi, mwanzilishi na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya          Helvetic Solar Contractors (Picha na www.bongo5.com)
mwanzilishi na mkurugenz mtendaji wa kampuni ya vifaa vya nishati ya jua iitwayo "Helvetic Solar Contractors."FUATILIA MAHOJIANO NA "GEORGE MEDIA NETWORK" KUPITIAhttp://www.georgenetwork.com/feature/exclusive_interview_with_managing_director_patrick_ngowi.html


Ufuatao ni muendelezo wa sifa hizo 10 ambazo kijana yeyote anapaswa kuzifuata kwa vitendo ili kutimiza ndoto ya kuwa tajiri.
(Sifa hizi hazipo kwa mtiririko...pia si lazima uwe nazo zote, lakini unaweza ukawa nazo chache na zikakufanya uwe nazo zote.Anza sasa kubadilika kwa vitendo!)


11.HUOGOPI KUJITOA MUHANGA NA KUPAMBANA NA HATARI (RISK TAKER)-Soma http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/06/vijana-na-maisha.html
 

12.UNAJARIBU KUJISHUGHULISHA NA BIASHARA TOFAUTI TOFAUTI…UKIJIFUNZA KWA MAKOSA -soma pia sifa ya 1 kupitia http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/06/vijana-na-maisha.html


13.UNAJITAHIDI KUHUSISHA UNACHOFAHAMU(HASA KIPAJI CHAKO) NA UTENDAJI HALISI-UNAKUWA MBUNIFU


14.UNATAMBUA UWEZO WAKO WA KUTENDA NA SI KULAZIMISHWA NA MTU MWINGINE


15.UNAJIONGOZA MWENYEWE KWA KUWA UNATAMBUA HATMA YA MAISHA YAKO IPO MIKONONI MWAKO 


16.UNASIMAMIA JAMBO(wazo la biashara) HADI KIELEWEKE, HUTAKI KUYUMBISHWA, HUJALI WATU WANASEMA NINI KUHUSU UAMUZI WAKO


17.HUOGOPI KUKATISHWA TAMAA, UNAJIAMINI NA KUSONGA MBELE

18.UNA MALENGO MAKUBWA, HURIDHIKI NA VIDOGO (soma zaidi

19.UNAANDIKA MALENGO YAKO NA KUYAFANYIA KAZI KWA MUDA ULIOJIPANGIA UKIWA NA MTAZAMO CHANYA- Soma zaidi http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/06/mtazamo.html

20.UNAJITAHIDI KUJIFUNZA KUPITIA WATU WALIOFANIKIWA, PIA UNATENGENEZA MTANDAO WA MAWASILIANO NA WATU HAO

Ni mtazamo tu wa Jielimishe Kwanza! kwa kuzingatia taarifa za mafanikio ya vijana.
USIKATE TAMAA…

CHUKUA HATUA YA UJASIRI KUBADILIKA!

Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
 

Jumatatu, 12 Agosti 2013

ELIMU: JIFUNZE VITU VIPYA KWA MAFANIKIO YA KUTOKUSAHAU KWA KUHUSISHA VILE UNAVYOVIFAHAMU PIA HALI HALISI


                                   Picha na www.presstv.ir 
Kila mwanadamu ameumbwa na hali ya kukumbuka na kusahau mambo mbali mbali yanayomtokea kila siku.Katika hali zote kuna faida na hasara yake, tukiangalia upande wa faida- mfano binadamu tunajihisi vizuri pale tunapokumbuka mambo mazuri yenye kufurahisha yaliyowahi kututokea pia tunasahau mabaya, huzuni na mengine yaliyowahi kutuudhi.

Tukirudi katika mfumo wa kujifunza hakuna mtu atakataa kuwa angependa akumbuke mambo yote aliyofundishwa na kujisomea ili afaulu mitihani na kupata cheti kizuri ilihali utendaji na utumiaji wa hayo anayojifunza  katika uhalisia ni hafifu.

Wanafunzi wengi wanapata shida na kukata tamaa ya kujifunza kutokana na aduni huyu mkubwa aitwaye KUSAHAU.












Mtazamo wa Wanasaikolojia kuhusu chanzo cha kusahau ovyo.

Text Box: Mmoja wa watafiti maarufu wa hivi karibuni wa masuala ya kumbu kumbu Elizabeth Loftus, ameainisha sababu kubwa nne zinazowafanya watu kusahau: 
• “retrieval failure” kushindwa kurudisha taarifa zilizotunzwa kwenye ubongo, 
• “interference”-mkanganyiko wa taarifa za zamani na mpya  
• “failure to store” -Kushindwa kutunza taarifa  
• “motivated forgetting” -uchochezi wa  kusahau. 

Soma: http://psychology.about.com/od/cognitivepsychology/tp/explanations-for-forgetting.htm

Tunawezaje kuboresha kumbu kumbu zetu na kuepukana na tatizo la kusahau kwa kulinganisha unachokifahamu na unachotaka kukifahamu?

Ikiwa wewe ni mwanafunzi, jaribu kujihoji kwanza ninafahamu nini? kabla ya kujifunza kitu kipya, husianisha kwa pamoja ukizingatia kufanana kwa hizo taarifa au mambo hayo mawili.

Pia jaribu kuhusianisha maarifa unayojifunza na hali halisi au vitu halisi.Ukitaka kukumbuka, hasa siku ya mtihani ni rahisi sana kukumbuka vile vitu au maarifa tuliyokuwa tunayafahamu kabla…hivyo husianisha! Utaona maajabu yake…hakika utakumbuka!

Ukitaka ufafanuzi au kujifunza zaidi kuhusu mbinu hii ya kuepukana na kusahau, tuwasiliane...

Imetolewa na
Jielimishe kwanza!


Ijumaa, 9 Agosti 2013

AFYA, MAZOEA NA MTAZAMO: FANYA HIVI KUDHIBITI UZITO WAKO KUEPUKA UNENE ULIOKITHIRI!

-->
Picha na www.nydailynews.com
Kutokana na taarifa ya Shirika la  afya duniani (WHO) za hivi karibuni zimebaini kuwa 65% ya idadi ya watu duniani wana uzito uliozidi na kuwa na vitambi, hii  pia imedhihirisha kuwa kundi hilo linaongoza kwa kupoteza maisha (kutokana na magonjwa mbali mbali ya tabia kama kisukari, shinikizo la damu, na magonjwa mengine ya moyo) kuliko kundi jingine la watu lenye uzito wa chini ambalo ni sawa na 35%. (Uchunguzi huo ulijumuisha nchi zote zenye watu wenye vipato vya juu na kati).

Huu ndiyo uhalisia…je hali yako ya mazoea katika kula inakuweka kwenye kundi gani?
Kwa pamoja tutafahamishana mbinu 10 za kukufanya uwe na uzito unaotakiwa kama ilivyoshauriwa na WHO kwa kuzingatia kipimo cha usawazisho cha uzito wa mwili na urefu (BMI) kama ifuatavyo:
Text Box: Body mass index (BMI) is a simple index of weight-for-height that is commonly used to classify overweight and obesity in adults. It is defined as a person's weight in kilograms divided by the square of his height in meters (kg/m2).
The WHO definition is:
• a BMI greater than or equal to 25 is overweight
• a BMI greater than or equal to 30 is obesity.

Source: http://www.who.int/mediacentre/factsheets/fs311/en/
                     Picha na www.belfasttelegraph.co.uk
 Ukitaka kujua kama uzito wako umezidi au kupungua ungana na ukurasa wetu, tazama sehemu imeandikwa PIMA AFYA YAKO HAPA! JE, UNAHITAJI KUONGEZA AU KUPUNGUZA UZITO? WASILIANA NASI 0754 572 143.(Hakikisha unafahamu uzito wako wa sasa(Kg) na urefu wako(cm) kabla ya kuanza zoezi hili).
Tuungane kipindi kijacho kuzifahamu mbinu 10 za kuthibiti uzito wako zilizo kinyume na mfumo mbaya wa ulaji.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza! kwa kushirikiana na CoNept-Afya.

Alhamisi, 8 Agosti 2013

ELIMU NA MTAZAMO: NINI HATMA YA KIWANGO CHA ELIMU ULICHONACHO…JE, KIMEKUPA FURAHA YA MAISHA?

-->

Picha na successfulworkplace.com


Ni dhahiri na ukweli usiopingika kuwa watu wengi wanaamini kuwa ni elimu pekee ndiyo mkombozi na chanzo cha furaha maishani.Ikiwa ni sanjari na msemo wa Kiswahili usemao; “Elimu ni ufunguo wa maisha” yaani bila elimu hujafungua maisha au …! Bila shaka unakubaliana na dhana hii.

Wanafunzi kuanzia ngazi ya awali hadi chuo kikuu wanasoma sana na hatimaye wanapofika mwisho wa safari yao huanza  kulinganisha walichojifunza na maisha halisi na mwisho wa siku tunajikuta tuna makundi tofauti tofauti yenye mtazamo tofauti tofauti kwa mfumo ule ule wa elimu:
·      Wengine huona kama wamepotea njia,

·      Wengine huanza kushtuka kuanza kuchagua kitu cha kufanya wakiwa wamehitimu

·      Wengine hujitamba kuwa wana vyeti vizuri na kujitukuza…hivyo kuchagua aina ya kazi

·      Wengine huanza kutumia kile walichosomea kutatua matatizo katika jamii kiuhalisia

·   Wengine hufurahia kutumia walichosomea kupanda vyeo sambamba na ngazi za mshahara

·      Wengine hutumia elimu ndogo waliyo nayo kupewa kazi wasizoweza kuzimudu

·      Wengine, wamethubutu kuviongezea vyeti vyao uwezo kwa kuambatanisha na vya watu wengine kupata ajira zinazofahamika kuwa na maslahi

…ndiyo hivyo, utaamua mwenyewe kujiweka kwenye kundi ulipendalo!

Swali la msingi

Naomba ujiulize, unakitumia kile ulichokisomea kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu? au ilikuwa ni kwa ajili ya kupata cheti tu au heshima isiyo na faida?

Hivi ina faida gani kusomea taaluma fulani kwa miaka 3 au 4 au 5 halafu isitumike kuboresha utendaji au kutatua matatizo katika jamii? Kwa mtazamo mwingine ni sawa na kupoteza muda na rasimali pesa ya Taifa.

Hivi tukitafakari kwa kina, nini lengo kuu la elimu? Ninaweza kuanisha malengo kadhaa ya elimu

·      Kuchochea na kukuza vipaji…elimu inapaswa kuchochea/kukuza vipaji na si kudumaza vipaji

·      Kuboresha mtazamo wa kufikiri na kutenda hasa katika kutatua matatizo ndani ya jamii

·  Kumpa mtu ujuzi wa kufanya kazi kutegemeana na kipaji chake…je unafanya kazi kulingana na kipaji chako?…au bora mkono uende kinywani?

·      Kujenga mahusiano mema, ushirikiano na watu wa jamii tofauti tofauti

·      Kumkomboa mtu na utumwa wa fikra…kumfanya mtu kuwa huru kifikra



Nini tufanye ili kuitendea haki elimu tuipatayo shuleni kwa manufaa ya jamii nzima hasa ile iliyokosa fursa adimu ya kupata elimu?

Kuna manung’uniko kila kukicha kuhusu ukosefu wa ajira…lawama zote hutupiwa serikali…hivi serikali ni nani? Bila shaka utajibu kuwa ni watu, na watu wenyewe ni kama wewe na mimi!

 Inasemekana, serikali pekee ndiyo yenye jukumu la kutengeneza ajira.Sasa umefika wakati kwa wahitimu wa vyuo vikuu na wanajamii kwa ujumla kutengeneza ajira na si kuitegemea serikali pekee…nikuahakikishie hata ungekuwa wewe madarakani usingefanikiwa kumpatia kila raia ajira anayoitaka kwa wakati anaotaka!

Tunapaswa kutumia tulichokisomea na vipaji vyetu kutatua matatizo katika jamii kwa kuongeza fursa za ajira kwa wengine.

Nikimnukuu Hayati baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere aliwahi kuweka msisitizo “Haitoshi kusema nafahamu, kufahamu kunapaswa kubadilishwa kuwa nyenzo katika kuboresha maendeleo ya jamii”

Pia unaweza kusoma makala hii muhimu inayoendana ELIMU NA UTENDAJI: KUFAHAMU BILA YA KUTENDA NI SAWA NA KUTOFAHAMU KABISA!KUJIFUNZA BILA YA KUTENDA NI SAWA NA KUTOJIFUNZA KABISA! kwa kubofya http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/05/elimu-na-utendaji.html

Education is what remains after one has forgotten what one has learned in school. Albert Einstein 
Education is not the learning of facts, but the training of mind to think -Albert Einstein

Huu ni mtazamo tu wa Jielimishe Kwanza!
Ikiwa una maoni au ushauri,

Usisite kutuandikia kupitia: