-->
-->
ferociousstrength.com
It’s
what we learn about ourselves from our response that really matters-Marissa Walter
________________________________________________________________________________________
N
|
dugu
msomaji, najua unaambatana nami kuhusiana na makala iliyopita kuhusu unavyojiona,
unavyowaona na vile wanavyokuona wengine.http://jielimishekwanza.blogspot.com/2014/01/mtazamo-unavyojiona-unavyowaona-na-vile.html
Kama
nilivyoeleza katika makala hiyo kuwa, kuna utofauti wa kimtazamo kwa sisi
tunavyojiona ukilinganisha na ule wa wengine.
Moja
kwa moja nikulete kwenye jinsi unavyoweza kutumia mtazamo wa wengine kukuhusu
wewe na kujiongezea uthamani katika utendaji kazi na maisha ya kila siku.
Zipo
njia mbali mbali zitakazokufanya uweze kutumia mtazamo wa wengine kujiongezea
uthamani, nitainisha njia tano (5) zinazobeba nyingine;
1.Jitambue
uwezo wako wa asili kabla ya wengine hawajakueleza.Hii ni njia muhimu
sana…inatengeneza sehemu ya kuanzia kupima mtazamo wako kiutendaji.(Hili huanza
na shauku au hamasa iliyo sanjali na uwezo wako wa ndani).
2.Kuwa
mwepesi kupokea mawazo kutoka kwa wengine kutokana na mitazamo yao kukuhusu(uwe
makini kulinganisha mawazo yako na yao ukisimamia sifa zinazoendana na wewe).
3.Usichukulie
kama unadharaulika kutokana na mitazamo ya wengine
kuhusu uwezo wako wa ndani…chukulia changamoto wanazozileta kama njia ya
kuboresha mapungufu uliyonayo katika utendaji wako.(Tambua kuwa kuna watu
wengine wapo kukukatisha tamaa, hawakutakii mema…utawajua kwa kusikiliza mawazo
yao ukilinganisha na uwezo wako na mawazo ya wengi kukuhusu wewe).
4.Watumie
vizuri watu unaofanana nao mtazamo…hawa watakuimarisha zaidi.
5.Usishawishike
kubadisha mtazamo wako kuhusu ulivyo na utendaji kila wakati…hii itakufanya
usiwe na msimamo, mwisho wa siku hautakuwa na kitu cha kusimamia na
kutambulisha uwezo wako wa asili.Mfano:Ukiwa na shauku ya kuwa mwana
mageuzi,kiongozi halafu mtu mwingine akakueleza kuwa huna sifa/karba hiyo na
una sifa nyingine tofauti ilihali wengi wanathamini uwezo wako.
Picha na |
Lakini
mwisho wa siku, cha muhimu zaidi ni vile unavyojiona mbele ya watu wengine.Maoni
yao kukuhusu wewe yanaongezea na kujenga uwezo wako kwa njia moja au nyingine
kama utayachukulia kwa mtazamo chanya.
Nakutakia
kila la heri katika kutumia mtazamo wako na wa wengine katika kuboresha
uthamani wako.
Imetayarishwa
na kutolewa na
Henry Kazula
Jielimishe
Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni