Uwanja
huu ni kwa kila mtu anayependa kuziishi ndoto zake.Kujielimisha kwanza
ni suala muhimu katika maisha yetu ya kila siku.
Kama ule usemi wa
wahenga usemao "Elimu ni bahari" au "Elimu haina mwisho", pia
kujielimisha hakuna mwisho.
Ningependa kujikita kwa suala zima la kutoa ushauri wa elimu,maisha,kazi,afya,sanaa na mazingira na mfumo wa maisha nikitumia uzoefu na ufahamu wangu nikiambatanisha na tafiti mbalimbali za kitaalamu.
Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikisoma
vitabu na majarida
mbalimbali na
kusikiliza masuala yanayojenga na kuelimisha, kwa hakika sipo vile
nilivyokuwa mwanzoni, nimebadilika kifikra, kimtazamo na kiutendaji.
Kuna
kitabu ambacho kila mtu anatakiwa kukisoma-"Think and Grow Rich"(Fikiri
Uwe Tajiri) cha Napoleon Hill, utatambua siri kwanini si "Work Hard and
Grow Rich"(Jitumikishe sana uwe tajiri).Kwanza fikiri, jitumikishe sana mwenyewe kuliko unavyojitumikisha kazini.
Inaweza ikawa vigumu kunielewa,lakini namaanisha kuwa jiongezee uwezo wako wa utendaji kwa kujielimisha zaidi kuliko unavyojitumikisha kwa mwajiri wako.
Ukiielewa falsafa hii utajikuta unafanya kazi kwa ubora unaohitajika na kipato chako kinaongezeka.
Nikizingatia makundi ya rika zote tutashirikiana kujifunza jinsi ya kuweka malengo,kutunza muda,kutunza pesa,kujiendeleza kusoma kwa bidii na kufahamu vitabu muhimu vya kusoma ili kuboresha ufaulu na utendaji wa kazi.
Nikilinganisha na mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia, kuna
tatizo kubwa sana la kuendana na mabadiliko haya.
Mara nyingi mabadiliko
huja na fursa.Je,umejipangaje kuzitumia fursa hizo? Kwa pamoja tutaweza
kupeana ujuzi na ufahamu jinsi ya kuzitumia fursa na kuziishi ndoto
zetu.
Nikimnukuhu mtaalam wa masuala ya Komputa na mvumbuzi wa Kampuni ya "Apple"-Steve Jobs alisema "...There is no reason not to follow your heart" akimaanisha kuwa-"...Huna sababu yoyote ya kutofuata ukipendacho."
Nakukaribisha uungane nami kuweza kuziishi ndoto zako na si kugombania ndoto ya mwenzio.Kuna ushahidi wa kutosha kuwa Mungu alimuumba kila mtu tofauti na kipawa chenye faida kwa wengine ndani yake.
Karibu!
Jielimishe Kwanza!
"It's all about Inspiration"
Utaziishi ndoto zako.