-->
Picha imetolewa na www.eppgroup.eu |
Mafanikio yako katika
kuwagusa wengine kwa mawazo yako ni ule uwezo binafsi wa kuwafanya wengine wakuamini.Pia jinsi ya kuwasiliana na kufuatilia
mazungumzo na wengine hujenga uwezo na hali ya kuaminika kwa wengine.
Hata siku moja huwezi
kutimiza azma yako ya kufikisha mawazo yako kwa wengine kuhusu biadhaa, huduma au
suala lenye mustakabali kwa maendeleo ya jamii kama tu hawakuamini au
huaminiki.
Ni sawa kabisa kuwa watu
wanaweza kukusikiliza kwa makini lakini wasitendee kazi mawazo au ushauri wako;
hii ndiyo hali halisi hadi watakapopiga hatua nyingine ya ujasiri kukuamini kwa kuwaaminisha kupitia vile
ulivyo sanjali na unayoyasema.
Ukiwa muuzaji bidhaa, je watu watanuua bidhaa yako kama hawaiamini? La
hasha! Inatakiwa uweze kuwaaminisha umuhimu na ubora wa bidhaa. Katika kuweka
msisitizo wa jambo hili, Mwandishi wa kitabu “Start With Why”-Simon
Sinek anasisitiza kwa kusema kuwa; “People don't buy what you do; they buy why
you do it. And what you do simply proves what you believe”. Katika tafsiri
ya Kiswahili-“Watu hawanunui unachofanya,
hununua kwa nini unafanya unachofanya.Unachofanya hutosha kuwaaminisha
unachoamini”.
Ukiwa kama mkuu wa ofisi (Manager), unayetaka
wengine wakubaliane na matakwa yako au utaratibu fulani; utaanza kujiuliza, je
wananiamini? Hii ni kwasababu kama hujajenga hali ya kuaminiwa, ama kwa hakika
hakuna atakayetekeleza matakwa yako.
Kwa upande mwingine kama
mzazi, je watoto wako wanaamini unapowaambia, usifanye hiki mwanangu? Je,
watoto wetu wanajutia unapowaeleza kuwa umewaeleza mara nyingi kuhusu kutofanya
jambo fulani lakini wanakaidi?
Ijulikane kuwa, kazi ya
kuwaaminisha wengine si rahisi kama huna ujuzi au mbinu stahiki.Kuwaaminisha
wengine si jambo la mazoea au mzaha mzaha. Lakini kwa bahati nzuri leo napenda
kutoa zawadi hii kwako msomaji kuwa kuna njia TANO (5) rahisi sana unazoweza
kuzifuata kama nilivyozinukuu kutoka katika kitabu cha “Secrets of Power Persuasion” cha Roger Dawson ili kuijenga na kuinua hali
yako ya kuaminika kwa wengine na kujiongezea heshima, uthamani na utendaji
katika maisha yako ya kila siku. Zifuatazo ni njia TANO (5) katika dondoo, zitakusaidia
sana kama utazitumia;
DONDOO 1:
“Never assume they believe you”.
USIBASHIRI KUWA UNAAMINIWA
Watu
wenye nguvu ya kuwahamasisha na kuwaaminisha wengine kwa mawazo yao wana mambo
matatu (3) kuhusu kutobashiri;
1)
Kutobashiri hali ya umasikini wao: kutobashiri
kuwa hawawezi kulipia gharama ya bidhaa inayouzwa
2)
Kutobashiri kuwa umeeleweka
3)
Kutobashiri kuwa umeaminika. Hili jambo la
mwisho ni la msingi sana. “Kutobashiri
kuwa umeaminika”.
Hakikisha
unagusia masuala yote ya msingi kwa kuzingatia kuwa watu unaotaka wakuamini nao
wanakusikiliza kwa makini na kutafakari kwa kina kuhusu unayowaeleza na kukuamini.Tumia
kila mbinu kuhakikisha unaeleweka ili wengine wakuamini. Ni lazima uonyeshe
uwezo wa kutekeleza kile unachotaka wengine waamini na kutekeleza.
Dondoo
hii inasisitiza; narudia tena na tena-Usibashiri
kuwa umeeleweka au kuaminiwa na wengine.
DONDOO 2:
“Only tell them as much as they’ll
believe”.
WAELEZE KADIRI UWEZAVYO HADI WAKUAMINI
Dondoo
hii inamaanisha kuwa usiwaeleze watu zaidi ya vile unavyofikiri ili wakuamini.Kiuhalisia
kabisa unaweza kuwa na bidhaa au huduma inayozidi mategemeo au matarajio ya
wateja, lakini kama utashindwa kuwafanya wakuamini, hutakuwa na wakumlaumu.
DONDOO 3:
“Tell the truth, even if it hurts”.
WAELEZE UKWELI MTUPU HATA KAMA UNAUMA
Ni kweli
kabisa kueleza au kuelezwa ukweli inauma.Kama ulikuwa hufahamu maana halisi ya
kueleza ukweli ni vyema ukaanza sasa utawafanya wengi wakuamini.Haijalishi ni
ukweli mchungu kiasi gani, usisite! eleza kila kitu wazi wazi.Hakika narudia
tena, utaaminiwa kibiashara, kiutendaji na kimaisha kwa ujumla.
DONDOO 4:
“Point
out the disadvantages”
ONYESHA MAPUNGUFU YA WENGINE KIUTENDAJI
Ukiwa ni mtu wa kutoa au kuonyesha
mapungufu ya bidhaa au huduma za wengine au utendaji wa mtu fulani ni dhahiri
kuwa lolote utakalosema baada ya hapo litaaminika au kuaminiwa na wengine.Tafiti
zimeonyesha kuwa kuna faida NNE (4) nzito kwa kukosoa au kutoa mapungufu ya
upande mwingine kimtazamo;
1)
Huufanya upande unaokosolewa kuamini kuwa
huna unafiki,ubaguzi wala upendeleo.Pia ni mtu wa haki uliye na upeo mpana
katika kushauri wengine kutenda na kuenenda katika unyoofu.
2)
Humfanya msikilizaji ajione kuwa unamthamini
na kuamini uwezo wake kiakili hivyo kuweza kuyaona mapungufu yake na pia
kujiona ni mkosaji kupitia ukosoaji wako.
3)
Hukuhamasisha na kukulazimisha kutarajia
mambo halisi yasiyo na mapungufu hivyo kujitahidi kufanya mahojiano yenye
kujenga
4)
Inakuongezea
sifa ya kukubalika na kuaminika katika kila utalosema.
DONDOO 5:
“Use Precise Numbers”
ONGEA UKITUMIA
TAKWIMU KWA NAMBA HALISI
Watu huamini zaidi takwimu kwa namba halisi na si makisio au
makadirio kwa namba.Takwimu unazotoa kwa namba halisi zitakuongezea hali ya
kuaminika zaidi kwa wale wanaokusikiliza.Hii huonyesha ni jinsi gani
unavyoeleza mambo kwa uhakika na ufasaha. Hivyo basi, ukitaka kujijengea hali
ya kuaminika, tumia namba halisi.Mfano, unaweza kusema kuwa kampuni yako
inaweza kuongeza mapato yake kwa asilimia 75 kuliko kusema kampuni inatarajia
kuongeza mapato yake kwa takribani mara
mbili ya yale ya mwaka jana.
Nakutakia utekelezaji mwema katika kujijengea uwezo
wa kuaminika na kila mtu.
Makala hii imeandaliwa kwa kutumia ubunifu na uelewa
binafsi wa kisaikolojia wa mwandishi Henry Kazula kwa
kushirikiana na uzoefu kutoka katika kitabu cha “Secrets of Power Persuasion” cha Roger Dawson.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni