+255 717 058 045
E-mail:ezongwe@yahoo.com
K
|
atika masuala ya kazi na ajira, jambo la muajiriwa
kuacha kazi ofisi moja na kuhamia ofisi nyingine au kujiajiri ni la kawaida
sana. Hii inatokana na mtu kuwa na matamanio ya kuwa na kazi nzuri zaidi, kazi
inayolipa zaidi au anataka kuwa bosi wake mwenyewe (kujiajiri). Pamoja na kwamba
jambo hili ni la kawaida katika mazingira ya kazi,tatizo lipo kwenye namna
unavyoondoka katika ajira yako hiyo.
Picha na woman.thenest.com |
Je, unaondoka ukiacha
mazingira salama au unaacha chuki na hasira kwa wengine? Watu wengi hujikuta
wakiwa hawana mahusiano mazuri na waajiri wao wa zamani au hata wafanyakazi
wenzao wa zamani. Wataalamu wa mambo ya Kazi, Ajira na Rasilimali Watu
wanashauri kuwa jambo hili si zuri hasa kama mtu anahitaji kuwa na mtandao
mpana wa wanataaluma tofauti tofauti.
Kwa kuzingatia ushauri huo,
hapa nakuletea njia sahihi 6 za wewe kuacha kazi uliyonayo sasa huku ukiacha
mazingira salama na yenye kuweka hali ya kutengeneza mahusiano mazuri baadae.
1. Toa taarifa kwa wafanyakazi wenzako - siku uliyotoa taarifa rasmi kwa muajiri wako au siku chache baada, kutana na wafanyakazi wenzako, angalau watatu au wanne, ambao umekuwa ukishirikiana nao vizuri. Hao ni washauri wako wazoefu, ni marafiki wako katika masuala ya kitaaluma, ni watu unaopaswa kuendelea kuwa nao karibu. Waeleze kuwa unaacha kazi hapo, hakikisha pia unawaeleza namna misaada yao kwako ilivyokuwa ya thamani na kama ikiwezekana waeleze kuwa uko tayari kusaidiana nao hata kwa kipindi ambacho hutokuwa nao tena ofisini.
2. Onesha thamani ya ofisi hiyo - kwasababu kazi yako ya sasa na ufanisi uliouonesha hapo ndio chanzo cha wewe kupata ajira nyingine, basi onesha thamani ya ofisi hiyo. Hii ni muhimu hasa kama unahamia ofisi pinzani (competitor). Fanya mawasiliano na muajiri wako wa sasa, mueleze mategemeo yako kwenye ajira yako mpya, pia eleza namna unavyo thamini msaada wake kipindi chote ulichofanya naye kazi.

3. Tafuta mbadala wako - mkufunzi
mmoja wa masuala ya Mawasiliano Sehemu ya Kazi, Jodi Glickman, ambaye ni Rais
wa kampuni ya Communication Training anasema, "huwa nawahimiza watu
wanaoacha kazi watafute watu watakaoziba nafasi zao kabla ya kuondoka".
Kama muajiri atakuwa tayari, angalia mtandao wako na chagua angalau watu watatu
ambao unahakika kati yao atapatikana mtu sahihi. Mpe muajiri wako mahali pa
kuanzia kuziba pengo lako kwa kumpatia orodha ya watu sahihi
kwa nafasi hiyo.
4. Ondoka bila kuacha kasoro - hata kama unaona uwezo wako wa kutambua mambo unaweza kuwasaidia wafanyakazi unaowaacha pale, usijaribu kueleza mambo yatakayoacha kasoro pale. Mfano; usijaribu kusema mambo mabaya yamhusuyo muajiri, hata kama ndio yanayokufanya kuacha kazi hapo kwani kufanya hivyo kutaadhiri maendeleo ya taaluma yako. Badala yake eleza mambo chanya na uoneshe thamani ya viongozi wako wa kazi (supervisors).
5. Toa ujumbe wa shukrani - fanya jitihada za kutuma ujumbe wa shukrani kwa waliokuwa viongozi wako wa kazi ambao kiukweli ndio waliokuwezesha kupata ujuzi mpya na uzoefu wa kazi (experience). Katika ujumbe huo eleza mambo mawili matatu ambayo hakika yalikusaidia sana. Ujumbe huu ni vizuri ukautuma wiki chache baada ya kuondoka.
6. Fanya mrejeo - hapa namaanisha 'follow up'. Tengeneza namna ya kuendelea kupata habari zozote kumhusu muajiri wako wa zamani au kampuni uliyokuwa ukifanyia kazi. Fanya mawasiliano ya mara kwa mara na wafanyakazi wenzako wa zamani. Panga kukutana nao kwenye chakula cha mchana au wakati wa jioni, baada ya muda wa kazi na jadili nao mambo kadha wa kadha yahusuyo maisha.
Mwisho, hakika hizi njia zitakusaidia sana kuimarisha ukaribu na muajiri wako wa zamani. Ni dhahiri kuwa utapata ushirikiano kwani waajiri wazuri (smart employers) wanaelewa faida za kuwa na mawasiliano mazuri na wafanyakazi wao wa zamani.

Ni muhimu sana kwani hujui kesho na kesho kutwa
utamkuta nani utakapokuwa unatafuta ajira nyingine mpya.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!Social Entreprises
wafanyakazi wengine ni wa korofi sana sijui kama unaweza kufanya nae kazi,maana wanafanyakazi kama wapo nyumbani hii ndo inaleta shida pia,
JibuFutaPia kuna waajiri ambao pia awafuati kanuni na sheria za kazi na inawapelekea wafanyakazi kuishi kwa shida,lakini kwa hali halisi ya wafanyakazi waliyowengi wanafanya kazi katika mazingira magumu,
JibuFuta