Mafanikio ya mtu yapo mikononi mwake, pia ni
jinsi anavyojitazama kwa mtazamo wa wengine na kujichukulia bila kuangalia
wengine wanasemaje kuhusu maamuzi yake.
Mwanadamu ana nguvu ya asili ya kufanya
machaguo.Nikimnukuu Hayati Baba wa Taifa la Tanzania- Mwalimu Julius K.Nyerere aliwahi kusema-Maisha ni kuchagua.Inategemea unaamua kuchagua nini kwa vile
unavyotaka uwe. Jinsi ulivyo sasa kimaisha ni kutokana na maamuzi/machaguo
yaliyofanyika siku zilizopita.
Tunaweza pia kuchagua marafiki ili tushirikiane katika kupambana na changamoto za maisha.Marafiki hao wanaweza kuchangia au kudidimiza
mafanikio yako kama umakini hautachukua nafasi yake.Inategemea ni aina gani ya rafiki unachangamana naye.Leo naomba
nikujuze aina ya marafiki unaopaswa kujiepusha nao.Utawatambua kwa maneno yao
na mazoea yao/tabia zao.
1.MARAFIKI WASIOTAKA KUELEZA YAO…ILA WANA UCHU
WA KUJUA YAKO
Aina hii ya marafiki ni hatari sana…mara nyingi
hukudodosa kujua mipango yako, mwisho kukukatisha tamaa, wakati huo huo
wanatumia mawazo yako waliyoyabeza!
2.RAFIKI ANAYEJIJALI YEYE TU…HAJALI MUDA, MCHANGO
WAKO
Hii ni hali ya ubinafsi inayoweza kuufanya
urafiki uwe wa upande mmoja.Pia kupelekea mmoja kujiona ni zaidi kuliko mwingine.(Itambulike
kuwa urafiki ni kufaidiana na kusaidiana…kila mmoja ana mtegemea mwenzake).
3. MARAFIKI WAENDEKEZA STAREHE KULIKO KAZI
Waepuke marafiki wavivu wasiopenda kufanya kazi
na mwisho wa siku wanataka mtoke mkatumie ulizozichuma.Kundi hili litakurudisha
nyuma kimaendeleo.Na kundi hili linalokuwa la kwanza kukukimbia
ukiishiwa.Hakuna urafiki wa kweli kwenye kundi hili!
4. RAFIKI ANAYESEMA YAKO YA SIRINI KWA WENGINE
Muogope rafiki ikiwa umembaini! Huyu aweza kuwa
mchonganishi.Unajua kuwa watu wengine wakielezwa siri huwa inawawasha miyoni
mwao…hivyo huileza kwa wengine kirahisi sana.Mtambue rafiki wa aina hii…epuka
kumueleza siri zako!
5.RAFIKI ANAYEPENDA KUKUKOPA HALAFU
HAKULIPI…UKIMDAI UGOMVI MKUBWA!
Kundi hili hupenda kutumia njia ya urafiki
kujineemesha kirahisi wakati huo huo likileta ugomvi ndani ya urafiki.Ukiiona
umemkopesha rafiki yako pesa halafu amekaa kimya hadi siku aliyoahidi kukulipa
ujue…………..ukitaka msigombane usidai! Ila ujue kuwa anakurudisha nyuma
kimaendeleo, si unajua tena pesa haitoshi!
SOMA MBINU ZA KUJENGA URAFIKI IMARA KUPITIA: http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/urafiki-siku-ya-kimataifa-ya-urafiki.html NA
Picha na thechive.com Imetayarishwa na kutolewa na |
Huu ni mtazamo wa Jielimishe Kwanza! Ukiiona
kuna tabia nyingine waliyo nayo marafiki wa kuepukwa usisite kutuandikia na
tutaiongezea kama kawaida…
Nashukuru kulijua hili, kwa kweli inabidi kuwa na rafiki atakayekutia moyo kujikwamua kimaisha...marafiki wengi wana sifa kama ulizotaja
JibuFutaKaribu sana Ernest.Ahsante kwa kujifunza.
Futajielimishe kwanza mpo vizuri....makala zenu zinatuelimisha sana
JibuFutaAhsante Aisha,endelea kufuatilia blog hii.Wajulishe wengine
FutaNice
JibuFutaThanks Frank
Futa