Nimekuwa nikitafakari kwa kipindi kirefu kwa
kutazama mtazamo na uelewa wa jamii kuhusu usafi wa mazingira na
kinachofanyika baada ya uchafuzi wa mazingira kutokea, nikajiuliza swali hili
“nani mwenye jukumu la kutunza usafi wa mazingira?” bila shaka ukiwa mdau wa
usafi wa mazingira, utajiuliza swali hili.Ikiwa hufahamu umuhimu wa usafi wa
mazingira, utajua ni nani anahusika kutunza usafi wa mazingira ukiendelea kusoma makala hii.
Ili kuweka bayana suala hili la usafi wa mazingira,
ni vyema tukajulishana au kukumbushana maana halisi ya neno “mazingira” …kwa
uelewa wa kawaida, mazingira ni mjumuisho wa mambo yote yanayomzunguka binadamu,
ukijumuisha mimea, wanyama na viumbe visivyo hai.Kwa lugha nyepesi, mazingira humtunza mwanadamu
ukijumuisha mimea na wanyama.Hivyo, binadamu hupaswa kutunza na kuhifadhi
mazingira ili yamtunze, yatunze pia
viumbe vingine vilivyo hali.
Binadamu anatajwa kuwa mstari wa mbele katika
kutunza mazingira kwa sababu ana utashi wa kujua mema na mabaya.Pia ndiye wa
kwanza kuanzisha shughuli mbali mbali za kibiashara na kiuchumi katika
mazingira yanayomtunza.Ikiwa sanjali na shughuli hizo, mwanadamu ana jukumu la
kuhakikisha mazingira anayoishi hayaathiriwi na shughuli zake kwa hali moja au
nyingine.
Nimezungumza kwa mapana sana, sasa niguse wahusika moja kwa moja.Kutokana na mgawanyiko wa majukumu ya kila siku,tofauti za
hali kiuchumi, na fursa ya kuwepo kwa teknolojia ya viwanda kumetokea matabaka
katika jukumu letu sote la kutunza usafi wa mazingira.
Baadhi ya watu wamejitenga kabisa na jukumu hili
muhimu kwa afya zao na za wengine kwa kusimamia maslahi pekee.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nisipothamini
juhudi za watu wachache katika kuzingatia jukumu la ubinadamu la kutunza usafi
wa mazingira.Mfano: vikundi vya kijamii, serikali kwa sehemu yake, Mashirika
yasiyo ya kiserikali na watu binafsi.
Leo nitoe mfano wa shughuli zifanywazo na
Shirika lisilo la Kiserikali “VoiceGiving” katika
kusimamia usafi wa mazingira na kutoa elimu ya usafi wa mazingira jijini Dar es
salaam-Tanzania. Shirika hili limenihamasisha sana kuhamasisha wengine kuhusu kuheshimu
na kutunza mazingira yetu.
Picha na Voice Giving. Baadhi ya vijana wa Shirika la "Voice Giving" VG wakiwa kazini katika kituo cha basi jijini Dar es salaam. |
Wanatumia njia shirikishi kuwahamasisha watu na
kuwakumbusha jukumu lao la asili la kutunza usafi wa mazingira.Wameanza
utekelezaji wa adhma yao kwa kuanza na mazingira ya vituo vya basi jijini Dar
es salaam.Hutumia kauli mbiu kama “nipe fagio” na “taka nomaa.”
Mwisho, najua kila mtu anapenda kuona mazingira
yakiwa safi, najua binadamu ndiye anayetengeneza uchafu kutokana na shughuli
zake za kila siku, pia hakuna mtu anayependa kukaa na uchafu, cha kushangaza zaidi watu huukimbia uchafu…ila kuna watu wachache sana huusika kusafisha mazingira.
Naomba tukumbushane wajibu wetu
kupitia nukuu maarufu kutoka kwa mwanaharakati wa mazingira-Mahatma Gandhi
aliposema “Be the change that you wish to
see most in your world.” Kwa tafsili isiyo
rasmi-“Uwe chanzo cha mabadiliko utakayo kuyaona” hivyo ukitaka kuona mazingira
safi anza kuonyesha juhudi ya kuyaweka mazingira katika hali ya usafi, anzia
nyumbani kwako.Chukia uchafu kwa vitendo, usisubiri mtu mwingine aje kuleta
makabadiliko-wewe ni chanzo cha mabadiliko.
Imetayarishwa na kutolewa na Jielimishe Kwanza!
Barua pepe: jielimishekwanza@gmail.com
+255 754 572 143