Picha imetolewa Jukwaa huru |
Neno “falsafa” kama lilivyoainishwa na tovuti ya Mwanahalisi Forum, ni imani aliyonayo mtu juu ya jambo au kitu fulani.Katika maana halisi ya neno "falsafa" kwa Kigiriki-"philosophy" lenye muunganiko wa maneno mawili; philo=love na sophia=wisdom (love of wisdom) lina mantiki kubwa katika kuhamasisha, kuchokoza fikra, hisia na ufahamu; kubwa zaidi ni kupenda kutenda mema.
Mtandao wa Mwanahalisi
Forum unafafanua zaidi kuwa; kila
mwanadamu aliye timamu katika maisha anaongozwa na vitu vitatu ambavyo ni
FALSAFA, MTAZAMO na MSIMAMO, vitu hivi huwa ndiyo dira ya mwanadamu katika
maisha yake. Mambo hayo matatu ndiyo hufanya wakati mwingine watu kutofautiana
au kuwa kitu kimoja.
Jicho letu linapenda
kuangazia zaidi kuhusu kuijenga “falsafa
binafsi ya maisha”-“philosophy of life” iliyo kanuni au utaratibu
anaojiwekea mtu binafsi; bila kushurutishwa na mtu mwingine ikiwa ni dira ya
maisha yenye kutoa maamuzi ya busara, yasiyo na kikwazo kwa maisha ya mtu au watu
wengine.
Tukiangazia fikra zetu zaidi
katika falsafa ya maisha iliyo dira
ya maisha ya mtu binafsi ni vyema kujua umuhimu
wa kuunda falsafa binafsi ya maisha na kujua jinsi ya kuijenga falsafa hiyo ndani ya maisha yetu kwa lengo la
kutawala maisha yetu.
Umuhimu
Wa Kuunda Falsafa Binafsi Ya Maisha
Kama ilivyoainishwa awali, falsafa
binafsi ya maisha yetu ni dira inayoongoza na kutawala upeo wa maisha yetu;
hutupatia faida mbali mbali kwa kuzingatia uwezo wetu wa ndani katika kutoa
maamuzi yaliyo sahihi na yasiyo kinzana na maadili ndani ya jamii husika.
Ndugu msomaji, natumaini
unafuatana nami ili kuepusha mkanganyiko wa kimtazamo na kifikra…hivyo basi,
nikujuze umuhimu wa kuwa au kuunda falsafa binafsi ya maisha kama hukuwa nayo,
na kama ulikuwa nayo kujifunza zaidi kuiimarisha kwa mafanikio maishani.
1.FALSAFA BINAFSI HUTUEPUSHA
NA HATARI MBALI MBALI KATIKA KUTOA MAAMUZI SAHIHI…
2.HUTOA MWONGOZO WA MAISHA
YETU...falsafa ya maisha ni dira ya maisha yetu!
3.HUTUEPUSHA KUWA WATUMWA WA
MAWAZO YA WENGINE…ikiwa tumekosa falsafa thabiti ya maisha yetu, ni rahisi kwa
watu wengine kutambua mapungufu yetu hivyo kutuingia kifikra na kutawala mawazo
na mtazamo wetu pasipo kujua.
4.HUTUJENGEA MSIMAMO THABITI
KATIKA MAAMUZI YETU…Huepusha kuyumbishwa na msimamo wa watu wengine kuhusu
sisi.Msimamo wetu ulio thabiti hudhihirisha ukweli wa vile tulivyo;
hututambulisha kwa wengine vile tulivyo.
5.HUTUEPUSHA KUWA BENDERA
FUATA UPEPO…hivyo kuongeza heshima na kuonyesha busara zetu kwa wengine katika
kutoa maamuzi sahihi.
6.HUSABABISHA KUWEPO KWA
MAHUSIANO MEMA NA WATU WENGINE…falsafa yetu iliyo na tija maishani huwavuta
wengine kwetu na kujenga mahusiano mema.
Fahamu
kwa undani jinsi ya kuijenga falsafa binafsi kwa kubofya HAPA
Tunakutakia
kila la heri katika zoezi hili muhimu la kujijengea falsafa yako.
Imetayarishwa na,
Imetolewa
na
Jielimishe
Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni