Picha na www.narconon.co |
Habari!
Naomba niwakaribishe tena katika ukumbi huu
kuhusu “MTAZAMO”.Wiki iliyopita niliandika makala kuhusu MADHARA YA KUWA NA MTAZAMO
HASI…
ISOME HAPA: http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/06/epuka-kuwa-na-mtazamohasi-picha-na.html
Mwishoni niliahidi kukuletea mbinu za kumfanya mtu kuwa na mtazamo chanya. Karibu tena leo kuzifahamu mbinu hizo.
Awali ya yote ni vyema tukafahamu faida za
kuwa na mtazamo chanya;
· Ni njia nzuri kiafya ya kuepukana na hatari ya
kupatawa na magonjwa ya moyo, pia huchochea kinga ya mwili
· kujiongezea uwezo wa kutatua matatizo
·
ni rahisi kwa watu wenye mtazamo chanya
kupambana na msongo wa mawazo
· mtazamo chanya huvuta vitu chanya-hii ni
sambamba na kufungua milango ya mafanikio katika maisha
· Katika hali ya muonekano wa kwanza, mtazamo
chanya utakufanya ukubalike na watu
Zifuatazo ni mbinu zinazoweza kumjengea mtu
uwezo wa kuwa na mtazamo chanya na wenye tija;
1.TUMIA LUGHA ILIYO CHANYA- USISEME “SIWEZI
KUPATA”…SEMA “NITAPATAJE?”…
Mjasiriamali maarufu na mwandishi wa vitabu
aliyebobea nchini Marekani-Robert Kiyosaki anatoa mtazamo huo katika hali ya
swali “NITAPATAJE?” akimaanisha kuwa swali hili litaubidisha ubongo kufikiri
njia mbadala za kupata suluhisho la tatizo.
Anapingana na usemi wa kwanza ulio
katika sentensi kamili “SIWEZI KUPATA” akimaanisha kuwa mtazamo huu hasi
unamfanya mtu kuwa mvivu wa kufikiri.
Anasisitiza kwa kusema kujiuliza maswali ni
njia moja wapo ya kuupa ubongo mazoezi na kuuongezea uwezo wa kufikiri, na
mwisho wa yote ni kupata mafanikio tarajiwa.
2.EPUKA KUELEZA MALENGO YAKO KWA KILA
MTU…UTAKATISHWA TAMAA!
Jifunze kuchagua mrafiki wa kuwaeleza malengo
yako…kuwa makini sana! Wapo wengine kazi yao ni kukukatisha tamaa.Ukitaka
kuwajua mtazamo wao, sikiliza maneno yao.
Angalizo: wapo watu watakaotaka kuboresha wazo/lengo lako kwa lugha ya kuonyesha ufanye marekebisho au maboresho, usiwabeze...chukulia hiyo kama changamoto kusonga mbele na kufanya vizuri zaidi.
3.JIFUNZE NA UFANYIE KAZI ULIYOJIFUNZA UKIWA
NA MTAZAMO CHANYA
Katika maisha ya kila siku tunajifunza kwa
njia moja au nyingine…jukumu letu ni kuchagua kujifunza mema au mabaya.Nikizungumizia
kuhusu kujifunza mema na yote yanayojenga ni vyema kuyafanyia kazi kwa vitendo
tukitegemea majibu chanya.Kadri utavyokuwa ukipima mafanikio ya utendaji ndivyo
unavyozidi kujiimarisha zaidi katika kuwa na mtazamo chanya.
4. JIWEKEE MALENGO KWA MAANDISHI
Ni kitu cha muhimu kuweka malengo-yanaweza
kuwa ya muda mfupi au mrefu.Mara nyingi malengo ya muda mfupi hutupa ari ya kuyakaribia malengo ya muda mrefu, pia ni sehemu ya kutuepusha kukata tamaa tukiwa katika safari ya kuelekea kwenye malengo ya muda mrefu.Kipimo cha mafanikio ya malengo yako kitaweza
kuboresha uwezo wako wa kuwa na mtazamo chanya.
5.JIHUSISHE NA WATU WENYE MATEGEMEO CHANYA
Kujihusisha na watu wenye mtazamo chanya
kutakuongezea uwezo wako wa mategemeo chanya katika mambo unayofanya.Pia
watakupa ari ya kusonga mbele kimawazo na kiutendaji.
6.FAHAMU FAIDA ZA KUWA NA MTAZAMO CHANYA
Ukifahamu faida za kuwa na mtazamo chanya
utajibidisha kufikia lengo la kuwa na mategemeo chanya.
7.JIWEKEE MPANGO WA KUEPUKA KUWA NA MTAZAMO
HASI
Panga utaratibu ulio kwa vitendo kuepukana na
mtazamo hasi.Kwa kufanya hivyo, mtazamo chanya utazidi kujijenga siku hadi siku.
8.TAMBUA NA UPAMBANE NA MAWAZO HASI
Kuna msemo unasema, kulijua tatizo ni njia
mojawapo ya kuoambana na tatizo au kumfahamu adui ni njia nzuri ya kuanza
kupambana naye.Jaribu kujichunguza utagundua ni kwa kiasi gani au mara ngapi
umekuwa na mtazamo hasi hata kwa vitu vilivyo kwenye uwezo wako?
9.JARIBU KUFANYA VITU VIPYA
Unapokuwa na uthubutu wa kutenda vitu vipya
ni njia ya kujiongezea ujasiri na kuimarisha mtazamo chanya wa kufikiri.Usiogope
kufanya makosa, hayo yanakuwa ni ishara ya kukuboreshea utendaji wako kwa kujifunza.
10.JISOMEE VITABU NA MAJARIDA
Kupitia vitabu na majarida utajifunza mambo
mengi kuhusu kujiimarisha katika mtazamo wa kufikiri hasa ukilinganisha na
wako.Ukitendea kazi mbinu mbali mbali zilizotolewa zitakuongezea uwezo wa kuwa
na mtazamo chanya siku hadi siku.
11.SIKILIZA HOTUBA NA MAFUNDISHO YENYE
KUIMARISHA
Kusikiza hotuba na mafundisho yenye
kuimarisha ukiwa kwenye gari au nyumbani ni njia nzuri kujiongezea uwezo wa
kuwa na mtazamo chanya.Kupitia hao utajifunza mbinu walizopitia kufikia malengo
yao.
Tuma maoni kupitia:jielimishekwanza@gmail.com
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni