Nikizingatia makala iliyoandikwa kuhusu
kuijua siri iliyopo ndani ya vitabu http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/ifahamu-siri-iliyopo-ndani-ya-vitabu.html unaweza kujua umuhimu au faida mbali mbali unazoweza kupata.
Imekuwa ni utamaduni wa Watanzania wengi na
Waafrika wengi kupuuzia suala la usomaji vitabu hasa vyenye kujenga,kuongeza
uwezo wa utendaji,kuamsha hisia za utendaji, na vingine vyenye maudhui chanya.
Kupitia makala tajwa nilieleza faida mbali
mbali tunazoweza kuzipata moja kwa moja kwa kusoma vitabu.Tuondoe visingizio mbali mbali kuhusu suala
zima la usomaji wa vitabu mfano suala la uvivu.
Picha na www.praesa.org.za |
Napenda nikupe mbinu na hatua za kufuata
ukitaka kusoma kitabu ukipendacho kuhusu maendeleo, ni vyema ukaanza kuzifanyia kazi hatua kwa hatua kama mtoto mdogo anavyojifunza (kama ilijulikanavyo na wasomi wengi kuwa ukitaka kujifunza vizuri ni vyema kujiweka kwenye nafasi ya mtoto):
1.Anza kusoma kitabu chenye kurasa chache
2.Chagua kitabu kinachoeleza wazo moja kwa
kurasa moja au mbili
3.Una uhuru kuanza kusoma wazo lolote
unalolipenda…si lazima uanze mwanzo wa kitabu
4.Jiwekee malengo ya kusoma kurasa moja au
mbili kwa siku…unaweza kuongeza kutegemeana na uhitaji na shauku ya kusoma
zaidi
5.Tumia kalamu ya kuweka kivuli kwa sehemu
muhimu sana-zitakusaidia baadaye kuweka utekelezaji
6.Mara zote usiache kutembea na kitabu ukipendacho…unaweza
kusoma muda wowote ukihitaji kusoma
7.Ukifanikiwa kutimiza mbinu 1,2,3,4,5,na
kumaliza kusoma kitabu ulichokichagua, vuka hatua nyingine kubwa kuanza kusoma
kitabu kingine ukiongeza idadi ya kurasa-hasa kile kinachotoa maelezo marefu
kuhusu wazo moja kwa kurasa zaidi ya kumi.
8.Jichunguze uwezo na mapungufu yako
kulingana na ujuzi uliopata kupitia kitabu ulichosoma.Chunguza fursa zilizopo katika nchi yako ukilinganisha na ujuzi ulioupata kwa kusoma kitabu.
9.Jipongeze unapomaliza kusoma kitabu kimoja
na kujifunza mbinu mpya ya kuboresha maisha yako na ya wengine.
10.Chagua wazo moja au ujuzi uliopata kwa
majaribio katika maisha halisi(weka katika utendaji).
Pia unaweza kutumia ipad yako kusoma kitabu ukitakacho.
Picha na app-of-ipad.blogspot.com |
Ikiwa wewe ni mzazi au mlezi zifanyie kazi hizo mbinu 10, pia tuungane
wakati mwingine na makala “Mjengee mtoto wako tabia ya kusoma vitabu”.Makala ijayo itakuwa ya msaada mkubwa endapo utakuwa kioo
kwa mtoto kwa kutimiza hizo mbinu 10 kwa ukamilifu.
Usiposoma kitabu chochote, utapitwa na maarifa, utakosa fursa mbali mbali pia utaamini sana ufahamu wako(si kweli kuwa unafahamu vitu vyote zaidi ya wengine)...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni