Picha imetolewa:http://www.urusecondary.sc.tz/school.htm |
Picha imetolewa:http://www.marianschool.site40.net/ |
Picha imetolewa:www.sajasemoshi.catholicweb.com/ |
Tunapozungumzia shule za sekondari bora
nchini Tanzania, tunaangalia kigezo kikubwa cha kufaulisha wanafunzi katika
mitihani ya kitaifa (NECTA). Mambo mengine ni mbwembwe tu na kupuliza upepo.
Tovuti http://serveafrica.info/tanzania/top-10-secondary-schools imeziainisha shule kumi (10) bora nchini Tanzania katika matokeo ya
kitaifa 2012 ya kidato cha (IV) kama yalivyotolewa na baraza la mitihani la
Taifa (NECTA).
Shule hizo ni;
5. TABORA
BOYS SECONDARY SCHOOL
6.
MZUMBE SECONDARY SCHOOL
8. DUNGUNYI
SEMINARY
9. PARANE
SECONDARY SCHOOL
10. ARUSHA
SECONDARY SCHOOL
Kuna suala la muhimu la kuangalia zaidi ya
ufaulu wa mitihani.Je, elimu wanayopata wanafunzi wetu ina tija ya kuwawezesha kutumia
kile walichokisomea na kujiajiri mara tu wamalizapo mfumo wa kusomea kazi-elimu
ya vyuo vikuu? AU ni ule umaridadi wa vyeti lakini hakuna uwezo wa kutumia
wanachokifahamu?
Nayasema haya kwa sababu ya ushahidi wa
kutosha uliopo katika ngazi wanazoendelea wanafunzi hao kuwa kuna jambo la
kushangaza kumuona mwanafunzi aliyepata daraja la I au la II akishindwa
kuendelea na hatua ya chuo kikuu.Hapa swali linakuja, mwanafunzi huyu aliwezaje
kupata daraja la I akiwa kidato cha IV?
Naomba nisieleweke vibaya, kuwa napinga
matokeo mazuri ya kitaaluma, ila naweka angalizo tu kwa shule zilizofanya
vizuri na zile zenye ndoto ya kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani
kitaifa.
Tuwajenge wanafunzi wetu kuendana na
changamoto za ajira na mabadiliko ya
Sayansi na Teknolojia. Tuwajengee wanafunzi uwezo wa kuwa watendaji na
si wajuaji, kwa sababu watu wengi wanajua ili watendaji wazuri ni wachache.
Tukiachana na hilo, naomba niwajulishe siri
ya mafanikio ya shule hizi bora nchini Tanzania kwa mwaka 2012;
·
Uongozi thabiti wa shule hizo
·
Usimamizi mzuri wa maadili ya wanafunzi na
walimu
·
Ushirikiano wa karibu wa walimu,wanafunzi na
wazazi
· Wanafunzi wanaochukuliwa kwenye shule hizo ni
wenye alama nzuri kutoka shule ya msingi
·
Mazingira mazuri ya kujifunzia…tembelea shule
hizo utajionea mwenyewe
·
Ubora wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia
· Naomba ufuatilie motisha wanazopewa walimu wa
shule hizo…utagundua kuwa zinawahamasisha kufanya kazi kwa bidii.
Naomba iwe funzo na changamoto kwa shule zinazochechemea ili
kuyafikia malengo ya elimu bora nchini Tanzania. Kuna njia kama mbili za
kujifunza kutoka katika shule hizo bora; moja tazama mwenendo wa shule hizo,
pili nenda uwaulize-kuhusu mbinu wanazotumia kutoa elimu bora.
Jielimishe Kwanza! , zitumie mbinu hizo kwa vitendo, utaona
mabadiliko.
Jielimishe Kwanza!
Inaalika maombi kwa shule mbali mbali nchini kwa ajili ya
kuwajengea wanafunzi uwezo wa kupambana na changamoto za ajira,
kujitambua,kuweka malengo,kuishi kwa kutimiza ndoto, kuboresha vipaji vya
wanafunzi na elimu ya jinsia.
Tuwasiliane kwa kutuandikia:
Barua pepe:jielimishekwanza@gmail.com
Au
+255 754 572 143
TUTEMBELEE OFISINI:
Sinza “B” Kitalu na 187, Shekilango road
Dar es salaam,
Tanzania.
No mzuri sana
JibuFuta