1.
“Kujielimisha ni kutafuta ukweli wa mambo.”
2.
“Ukiondoa matatizo wayapatayo binadamu kwa sababu
ya mambo kama mafuriko,nzige,kiangazi,n.k., matatizo yao mengi hutokana na
unafsi.”
3.
“Nitasema kweli
daima.Fitina kwangu ni mwiko.”
4.
“Wengine humwona mwenzao
anafanya kosa.Badala ya kumwambia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa,
watanyamaza kimya.Lakini hawanyamazi kimya kabisa! Watakwenda kumteta katika
vikundi vya siri siri.”
5.
“Wengine hugawa watu katika mafungu.”Fulani” japo akifanya
kosa kubwa sana hasemwi.Lakini “Fulani” wa pili akifanya kosa japo dogo, kosa
lile hukuzwa likawa kama mlima Kilimanjaro.”
6.
“Ukweli una tabia moja nzuri sana.Haujali mkubwa wala mdogo;
haujali adui wala rafiki.Kwake watu wote ni sawa.”
7.
“Makosa yetu mengine hutokana na woga; woga unaotuzuia
kumlaumu mkubwa japo tunajua kuwa kakosa, au kumtetea mdogo anayelaumiwa na
wakubwa japo tunajua kuwa hana makosa.”
8.
“Kosa jingine ni kutojielimisha.Kanuni yetu moja inasema: Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu
wote na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.Wengine hufikiri kuwa
kujielimisha ni kujua kusoma na kuandika.Hilo ni kosa, lakini si kubwa kama la
pili.Wengi wetu, hasa baadhi ya viongozi, hufikiri kuwa tunajua kila kitu na
hatuna haja kujifunza jambo lo lote zaidi.”
9.
“Watu walio hatari sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua
kila kitu, wala hawana haja kujifunza zaidi.Hii ni tabia mbaya ambayo huzuia
kabisa maendeleo.”
10. “Uvivu wa kutumia akili
unaweza kutufanya tutumie dawa kuondoa matatizo ambayo si ya dawa hata kidogo.Daktari
asipojua ugonjwa wangu na sababu zake hawezi kujua dawa yake.Akinipa dawa
nikapona, atakuwa kaniponya kwa bahati tu, kwa desturi daktari wa namna hiyo
hawezi kumponya mgonjwa, na ni daktari wa hatari sana.”
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza