Kabla ya kukoma kwa biashara ya utumwa mnamo karne ya 18, binadamu alikuwa akiuzwa kutoka nchi moja hadi nyingine(mfano
Afrika kwenda Ulaya na Uarabuni) kwa lengo la kuwatumikia wengine kwa ujira mdogo
sana au bila ujira kabisa.
Mara tu baada ya kukoma kwa biashara hiyo ya
watumwa, wafanyabiashara na watu wa kada nyingine za ajira walikaa chini na
kutafakari…mwisho wakaweka kitu kinachoitwa ujira/mshahara kulingana na
utendaji au ubora auletao mwajiriwa katika eneo la kazi.Hapa kukatokea
ngazi/madaraja mbali mbali ya mishahara!
Nikimnukuu Jim Rohn aliyekuwa mwandishi
maarufu na msemaji wa hadhara nchini Marekani- anasema; “People get paid by bringing value to the market place”.(Watu hulipwa
kutokana na ubora wanaouweka katika soko)-Alizungumzia soko kama watu au
eneo la kazi kwa kuwatumikia watu.
Kama ulikuwa hujui hilo, funguka macho ndugu
msomaji.Hiyo ndiyo hali halisi.Hivyo basi ukiona unalipwa kidogo ujue una
mchango mdogo sana kwenye soko.Hili limepelekea watu wengi sasa kuishi katika
utumwa ulioboreshwa/Utumwa wa kisasa au kwa lugha ya Kiingereza “Modern-day Slavery”.
Picha na www.cvent.com |
______________________________________________________________________________________________________________
Utumwa huu wa kisasa unahusisha; usafirishwaji wa binadamu ndani au nje ya nchi (aina hii ni kama inaturudisha tulikotoka-Kihistoria),watumishi wa ndani, kuzidiwa na madeni,kulazimishwa kuomba omba, kushurutishwa kimapenzi, kulazimishwa kuolewa katika umri mdogo, kunyanyaswa kijinsia na manyanyaso katika sehemu za kazi(kufanyishwa kazi ngumu kwa ujira mdogo au bila ujira kabisa).
______________________________________________________________________________________________________________
Nimeamua kukujuza hili kwa kulinganisha na
taarifa ya gazeti la “The Citizen”
–Jumamosi, 19 Octoba 2013 la nchini Tanzania kuripoti kuwa zaidi ya watu
300,000 nchini Tanzania ni watumwa katika mfumo huo wa utumwa wa
kisasa!Tanzania ikiwa inaongoza kuwa na idadi kubwa ya watu walio katika utumwa
wa kisasa katika nchi za Afrika Mashariki.
Kulingana na takwimu za mwaka 2013 za “Global Slavery Index” zinaeleza kuwa
kati ya watu 310,000 hadi 350,000 wanaishi kama watumwa.Namba kubwa ya watu
ikiwa mjini.Tanzania ikiwa ya 29 katika nchi 162 zilizofanyiwa utafiti huo
duniani. Gazeti la “The Citizen”
limeripoti. Soma hii
http://www.globalslaveryindex.org/findings/?gclid=CK3ByPffp7oCFbPItAodlh0AKQ#overview
kujionea uhalisia wa takwimu hizo kwa mwaka 2013.
Utumwa huu wa kisasa una viashiria vingi
ambavyo nitavieleza siku nyingine.Pia tutafahamishana mbinu za kuepukana na
utumwa huu wa kisasa hasa katika maeneo ya rasmi ya kazi.
Hivyo endelea kuifuatilia blog yako Jielimishe Kwanza! Ujielimishe! zaidi kwa Kuhamasika!
Pia Kuhamasisha! wengine kubadili
mtazamo ili kuepuka manung’uniko na kuwa na mtazamo chanya.
Soma na hii kujua zaidi kuhusu utumwa wa kisasa http://www.antislavery.org/english/slavery_today/what_is_modern_slavery.aspx
Soma na hii kujua zaidi kuhusu utumwa wa kisasa http://www.antislavery.org/english/slavery_today/what_is_modern_slavery.aspx
Imetayarishwa na kutolewa na,
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni