T
|
ukikumbushana moja ya makala zetu kuhusu viashiria
vya kutekwa kwa uhuru wa fikra,mtazamo, uchumi wa mtu binafsi http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/12/mtazamo-hivi-ndivyo-uhuru-wako.html
Picha na stepontoliquid.wordpress.com |
naomba nikulete kwenye makala ya leo kuhusu makosa yanayoweza kuinyima akili
uhuru wa kufanya kazi yake barabara-(mbele ya kila kosa kuna suluhisho);
1.
Kutojielimisha-kujielimisha ni njia ya kujua ukweli wa mambo
2. Kupuuza usomaji wa makala na vitabu- ukweli wa mambo
hufahamika kupitia kulinganisha mawazo ya watu tofauti tofauti…Unasoma mawazo
yao kupitia vitabu au makala zao au kuongea nao.
3.
Kupuuza mawazo ya wengine-kuwa msikivu zaidi na si muongeaji
zaidi bila kupuuza wazo la mwingine
4.
Kujifanya mjuaji wa yote-tambua kuwa siku zote tunajifunza
vitu vipya, huwezi kujua kila kitu
5. Kuwa na majibu rahisi kwa maswali magumu(huu ni uvivu wa
kufikiri)-tuepuke kubashiri kwa hisia na kutoa majibu rahisi ya
matatizo/maswali magumu…tuiruhusu akili yetu itafakari kwa kujiuliza maswali ya
msingi na kutoa majibu ya matatizo.
6. Kuchagua viongozi wasio na sifa…hawa hukunyima fursa ya
kutoa mawazo yako na kukufanya uwe mtumwa wa fikra zao-tuwapime viongozi kwa
uwezo wao wa kuongoza wenye kujua wameteuliwa kwa manufaa ya wananchi na si
unafsi.Tuwaepuke viongozi wanaoamini zaidi mawazo yao binafsi kwa manufaa yao
na kuyafanya ya wengi.
7.
Kutumia pombe na madawa ya kulevya kupindukia-punguza au
acha matumizi ya pombe na madawa ya kulevya.
8. Kutopata muda wa kukaa mwenyewe na kutafakari maisha
yako-jiwekee utaratibu wa kukaa mwenyewe na kutafakari kuhusu changamoto za
maisha.
9. Kutegemea wengine wakuamulie kila kitu au wakuthibitishie
maamuzi yako-jiamini, tambua kuwa wazo lako ni wewe unayejua hatma yake.Ujue
kuwa katika dunia hii kuwa wakatisha tama wengi.Wakati mwingine ni vyema
kufanya mambo yatokee…ukikosea, jifunze tena kwa kupitia makosa hayo.
10. Hofu ya kukosea-Wavumbuzi wengi duniani walifanya makosa
mengi sana…wakajifunza kupitia makosa.(Ungana nasi kwenye makala ijayo yenye kichwa:TUJIELIMISHE!
TUJIFUNZE! TUJIPANGE UPYA KUPITIA MAKOSA…
Mfano wa Thomas Edison katika kuvumbua taa ya umeme
alifanya makosa 1,000.Edison alichulia makosa haya kama ni njia 1,000 za
kutengeneza taa ya umeme.Jifunze kwa watu mashuhuri duniani waliofanya makosa
kupitia http://www.uky.edu/~eushe2/Pajares/OnFailingG.html
Ikiwa hujanielewa na unahitaji ufafanuzi zaidi, tafadhali usisite kuwasiliana nasi.
Imetayarishwa na kutolewa na,
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni