Raisi,(1994-1999), Mwanamapinduzi,Mpigania haki kuhusu ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini-Nelson Mandela. (Picha na www.newstimeafrica.com). Picha hii imewekwa kwa kuthamini mchango wake, ni mfano wa kiongozi bora wa kuigwa, pia kumtakia heri. |
Wataalam wa masuala ya uongozi wamekuwa
wakijiuliza swali lifuatalo mara nyingi; viongozi huzaliwa au hutengenezwa?
Ikimaanisha-ni mtu tu anajikuta kazaliwa ana uwezo wa kuongoza au anafundishwa
kuwa kiongozi?
Mtazamo wa wengi ni kuwa viongozi
wanazaliwa…ni kipaji tu cha mtu cha kuzaliwa nacho.Yaani, wakichukulia kuwa
tangu kipindi cha utoto utaiona tabia ya mtoto akiwaongoza wenzake katika
michezo ya kitoto.
Pia, kiasilia kunapokuwa na watu zaidi ya
wawili na wanahitaji kutoa maamuzi ya pamoja utaona kuwa mmoja hujiweka
kipaumbele katika kutoa maamuzi na anakubalika.
Mwandishi maarufu, Stephen R.Covey katika
kitabu chake cha “The 8th
Habit- From Effectiveness to Greatness” anapingana na mawazo ya wengi kwa
kuweka msimamo hasi…akimaanisha kuwa viongozi hawazaliwi wala hawatengenezwi ila
mazingira huwafundisha na kuwalea.
Akiunganisha na wazo la uwezo wa asili wa
mwanadamu…Stephen anasema; "kikawaida mwanadamu ana nguvu ya asili ya kufanya
chaguo."
Hivyo
basi, akasiliba kwa kusema "viongozi hujitengeneza
kwa kuchagua wenyewe", na endapo watafuata kanuni na kujiongezea nidhamu
dhabiti, uhuru wao wa kuchagua huongezeka.
Akithibitisha
ukweli wa wazo lake Stephen kwa kulinganisha na wazo la Dk.Noel Tichy ambaye
alisema;viongozi hawazaliwi ila hufundishwa…Stephen anaunganisha mawazo kwa
kusema; watu hutumia nguvu yao ya kuchagua kujifunza na kufuata mafunzo.
Tukifuatilia kwa makini orodha ya viongozi wenye mafanikio duniani ni kubwa.Nikisema nianze kumjadili mmoja hadi
mwingine itachukua muda mrefu sana bila ya kumaliza.Ila viongozi wote hawa
walikuwa na tabia/wana tabia za kipekee na zinazofanana ambazo ni;
1. Kuwa na maono”vision” ya mbali yenye tija na kuyafanyia utekelezaji, ambayo
wengine (wafuasi) hawayaoni. Mtaalamu wa masuala ya uongozi na mwandishi
aliyebobea nchini Marekani Warren Bennin alisema, “uongozi ni kubadilisha maono kuwa uhalisia”
2.
Hutenda kwa kufuata dhamiri “conscience”…hutenda kwa kufuata sauti
ya moyo ya ndani inayomfanya mtu kutofautisha jema na baya. Kama Stephen Covey
anavyosema; “Sauti hii ya ndani ni tulivu
na ya amani. Pia inahusisha kujitoa mzima mzima kwa jambo jema tarajiwa…Ni hii
dhamiri inayotafsiri maono kuwa huruma kwa wengine.”
3. Huwa
na shauku”passion” kubwa ya
kutenda.Hii hutoka moyoni. Nikimnukuu
mjasiriamali mwenye mafanikio na mwandishi wa vitabu Anthony Robbins anasema;
"There is no greatness without a
passion to be great, whether it's the aspiration of an athlete or an artist, a
scientist, a parent, or a businessperson." Akimaanisha kuwa hakuna ukuu au umaarufu unaokuja bila ya shauku ya
kuwa mkuu au maarufu, si ndoto ya kuwa mwanariadha au msanii, mwanasayansi,
mzazi au mfanyabiashara.Haya yote yanaanza na kuwa na shauku.
4.
Nidhamu”discipline”
kwao ni silaha.Kama alivyosema raisi wa
26 wa Taifa la Marekani Theodore
Roosevelt alisema; “kila kitu
kinawezekana kwa kuwa na nidhamu binafsi”
5. Ukifuatilia
mafundisho au hotuba zao, huongea na hisia za watu kwa kugusa mioyo. Hupangilia
maneno yao si kwa kujifurahisha wenyewe, bali kugusa hitaji la ndani la mioyo
ya wengine. Kwa mantiki hiyo, wafuasi hupenda kuwasikiliza na kutendea kazi
mawazo na mafundisho yao.
Bila shaka umepata kujua kuwa kila mtu anaweza kuwa
kiongozi.Pia ni suala la kuchagua kujifunza na kufuata kanuni za uongozi bora
na si bora kiongozi.
Jielimishe Kwanza!
Tutumie maoni yako
Barua
pepe:jielimishekwanza@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni