_______________________________
MTAZAMO:SHAIRI
Na Justine Kakoko
Activities: Social & Political activist I Social entrepreneur
I Administrator I
Poet & Song writer based on
Pan-africanism Ideology
Poet & Song writer based on
Pan-africanism Ideology
E-mail: justinekakoko@gmail.com.
______________________________________
SHAIRI: "Hatufundishwi
Shuleni"
Hutufundishwi Kujiamini/
Hatufundishwi Kujithamini/
Hatufundishwi Kujijua,
Kujitambua Sisi Ni
Wakinanani/
Hatufundishwi Tukagundua
Wapi Tulikuwa Kabla Ya
Ukoloni/ Zaidi Ya
Kuchukiana
Hatufundishwi Kupendana
Darasani/ Hata Sishangai
Nikisikia, Mwafrika Kuingia
Vitani Kisa Dini/
Hatufundishwi Faida ya
Kuungana/ Hatufundishwi
Umuhimu Wa Kushirikiana/
Kuweka Nguvu Pamoja
Biashara Zilete Maana/
Tunafundishwa Ukilema
Watu Wazima Kutegemeana/
"..Aliyeanguka Sio
Wenu.."
Hatufundishwi Kuinuana/
Tunafundishwa Historia
Isiyoandikwa Na Sisi/
Historia Iliyobadilishwa
Historia Isiyonauhalisi/
Tunafundishwa Matatizo
Pasipo Njia Za Kuyatatua/
Inachosha, Yanazidi
Ongezeka
Hakuna Linalopungua/
Hatufundishwi Tukajua Kuwa,
Waafrika Tuna maadui/
Kila Nyakati Twawindwa
Si Usiku Mchana Hata
Asubui/
Mzungu Njama Nyingi
Katu Mapigo Hayapungui/
Tumechomwa Sumu Tumeachwa
Tunatizama Alama Ya Ndui/
Tunafundishwa Kuigiza
Nyendo
Za Mzungu/ Tusichojua
Hayomaigizo
Yanaongeza Ukungu/
Hutufundishwi Mifumo Ya
Dunia/
Jinsi Gani Inafanya Kazi
Ili
Tusije Angamia/ Waongozoji
Kitu Gani Haswa
Walichokipania/
Agenda Zao Wapi
Zilipolalia/
Hatufundishwi Uozo Wa
"Umoja
Wa Mataifa" Nyuma Ya
Pazia/
Hatufundishwi Kwanini
Mashujaa
Wa Afrika Tunaendelea
Kuwafukia/
Tunafundishwa Nadharia Bila
Vitendo/
Tunafundishwa Subira, Eti
Polepole
Ndio Mwendo/ Tunafundishwa
Wagunduzi
Wa Afrika Tuliyoikaa Tokea
Mwanzo/
Mambo Ya Vasco Dagama,
Historia Ya Kitoto
Tufanye Ukatazo/
Hatufundishwi Jinsi Ya
Kujilinda/
Hatufundishwi Jinsi Ya Kuyapinga
Mazito Yanayotushinda/
Hatufundishwi Kukwepa
Propaganda
Kuondoka Kwenye Runinga/
Ili Twende Kusoma Tuondoe
Ujinga/
Hatufundishwi Tukajijua
Kiundani/
Ili Tuwe Imara Kimwili Na
Akili
Yatupasa Tule Chakula Gani/
Hatufundishwi Elimu Ya
Jinsia
Wengi Tunajifunzia
Uwanjani/
Hatufundishwi Mahusiano,
Usione Ajabu Ni Malumbano
Nyumbani/
Hatufundishwi Kwanini
Hakuna
Ajira Nchini/ Tunafundishwa
Ajira
Zipo Tunasoma Kwa
Matumaini/
Hatufundishwi Kujiajiri,
Tumalize
Tuishi Kimasikini/
Hatufundishwi
Kujenga Bila Hofu Ya
Kuanguka Chini/
70% Ya Vijana Wapo Vijiweni
Baada Ya Kuitimu Vyuoni/
Inabidi Iwe Hivyo Maana
Hatufundishi Kipi Kipo
Mtaani/
Hatufundishwi Kwanini Sisi
Ni Masikini/ Masikini Wa
Hali Ya
Chini Maisha Yetu Duni/
Kipi Chashusha Kabisa Hali
Yetu Ya Uchumi/ Mbona
Tunawanyama Tele
Mbugani..?/
Mafuta Na Madini
Yanachimbwa Ardhini...?/
Lakini Hatufundishwi,
Kuuliza Kwanini..?/
Hatufundishwi Kuijenga
Afrika/
Hatufundishwi Afrika
"Mpya"
Nini Inataka /
Hatufundishwi
Kuichukia Misingi
Iliyotuzika/
Misingi Waliyoijenga
Ili Unyonyaji Usijekatika/
Kiukweli Tunafundishwa
Kulala,
Katu Hatufundishwi Kuamka/
Hatufundishwi Kuijua Siasa/
Siasa Inaendeshwa Vipi
Ndani
Ya Ulimwengu Wa Sasa/
Tunachofundishwa Ni Akili
Kuzipumbaza/ Hatufundishwi
Kwa Macho Matatu Dunia
Kuiangaza/
Kuangaza Marekani Na China
Wanavyotuburuza/
Tunahitaji Elimu Yenye
Kuiakisi Afrika/
Itakayotuhusu Sisi Na
Mazingira
Yanayotuzunguka/
Itakayorekebisha Makosa
Ya Wapi Tulipoanguka/
Itakayotuonyesha Njia
Na Vipi Tutainuka/
Itakayoturudisha Kwenye
Asili Mpaka
Tutapojikumbuka/
Elimu Hii Ya Sasa, Elimu
Hii Nimeichoka/
Tunahitaji Tufundishwe
Historia Yetu/
Tunahitaji Tufundishwe
Tamaduni Zetu/
Tunahitaji Tufundishwe
Thamani Na Ushujaa
Wetu/ Tunahitaji
Tufundishwe Wapi Walipoishia
Babu Zetu/ Ili Juhudi Zao
Ziendelezwe Visibezwe
Vizazi Vyetu/ Tunahitaji
Tufundishwe Juu Ya Imani
Na Dini Zetu/
Tunahitaji Tufundishwe
Kutofautisha
Kati Ya Taarifa na maarifa/
Ili Tusioshwe Ubongo, Uongo
Uongo
Usilete Nyufa/
Tunahitaji Tufundishwe
Chanzo
Cha Magonjwa Kama Ebola Ona
waafrika Wanavyokufa/
Tunahitaji Tufundishwe
Kujiongoza
Tuondoke Utumwani/
Tuhitaji Tufundishwe Ili
Tusirudishwe
Mashambani/
Tunahitaji Tufundishwe,
Vipi Izalishwe
Isisafirishwe Katani/
Tunahitaji Tufundishwe
Kupendana
Waafrika/ Chuki Yatutafuna,
Umoja
Hatuna Twaingilika/
Tunahitaji Tufundishwe
Manufaa
Ya Elimu Tuipatayo/
Elimu Tuipatayo Ituondoshe
Kwenye Hali Tulionayo/
Elimu Tuipatayo, Ikamilishe
Safari
Tuijengayo/
Elimu Tuipatayo Ilishe
Wengi
Isiache Wengine Wapige
Mwayo/
Tunahitaji Tufundishwe Wizi
wa Warumi Na Wagiriki/
Kubeba Kila Kilichochetu
Kusema
Chao Wakadiriki/
Dini, Sanaa, Sayansi,
Uandishi,
Vyote Tulianzisha Sisi
Hawatuandiki/
Tunafundishwa Uongo,
Lakini, Ukweli
Haubadiliki/
Tunahitaji Tufundishwe Haki
Zetu Za Msingi/
Ili Uonevu Uondoshwe Maana
Manyanyaso Ya Polisi Ni
Mengi/
Malcolm X Alisema,
"Hakuna Mtawala
Anayemfundisha
Mtumwa Kuwa Huru"
Basi Tufundishane Kuikata
Minyororo
Ikiwa Kweli Tunauhitaji
Uhuru/
-GSP
KUSIKILIZA SHAIRI "Hatufundishwi Shuleni" na
MASHAIRI MENGINE, JIPATIE CD YAKO-VOL 1-
TZS 6,000
+255 754 572 143
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni