Ikiwa ni siku chache kabla ya Mkutano mkuu Wa jinsia Wa Baraza kuu la Umoja wa Afrika (AUC) unaotarajiwa kuanza tarehe 22-25 Januari 2017 jijini Addis Ababa-Ethiopia, Shirika la “Action Aid Tanzania” kwa kushirikiana na Mtandao Wa Jinsia- “Tanzania Gender Networking Programme” (TGNP)-Mtandao wamekutana kwa pamoja kujadili mafanikio makubwa ya kuundwa kwa Baraza la Wanawake Vijijini-The Rural Women Council (RWC) lililoundwa mwaka 2012.
Moja
ya mafanikio, na kubwa kuliko yote ni lile la Baraza la Wanawake Vijijini (RWC)
kutambuliwa na Baraza kuu la Umoja wa
Afrika (AUC) hadi kufikia hatua ya kutoa mwaliko kwa Bi. Flora Mathias Mlowezi
ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la hilo kwa Afrika Mashariki, pia ni mwanaharakati
wa masuala ya Jinsia kutoka “TGNP’s
Tigushe Knowledge Center in Mbeya rural district” ili kuwakilisha sauti za
vilio vya wanawake wengi vijijini kuhusu Haki yao ya msingi kumiliki Ardhi nchini
Tanzania na Afrika ya Mashariki kwa ujumla.
Picha: Bi. Flora Mathias Mlowezi: Mwenyekiti-Baraza
Afrika ya Mashariki na
Mwanaharakati- “TGNP’s Tigushe Knowledge Center
in Mbeya rural district" kutoka Tanzania.
Licha
ya kutetea maslahi za wanawake wengi waliopo vijijini katika haki yao ya
kumiliki Ardhi; Bi Flora anakuwa ni miongoni mwa wanawake shupavu walioweza
kushiriki Kampeni maalumu ya kupanda mlima mrefu Afrika-Kilimanjaro kupitia
kampeni “Kilimanjaro Initiative”
iliyoasisiwa na
Baraza la Wanawake Vijijini-The Rural Women Council (RWC) mnamo Octoba 2016 chini ya uangalizi wa TGNP-Mtandao wa Jinsia na Action Aid Tanzania jijini Arusha-Tanzania.
Kupitia
mkutano mdogo wa wadau wa kutetea masuala ya haki ya mwanamke kumiliki Ardhi
kutoka TGNP- Mtandao wa Jinsia na Action
Aid Tanzania uliofanyika jijini Dar es salaam tarehe 21/01/2017, washiriki
walilenga kumjengea uwezo na kumpa ujasiri Bi.Flora ili kuwa na uelewa wa
kutosha katika kuwawakilisha wanawake wote wa vijijini nchini Tanzania na
Afrika Mashariki kwa ujumla wake.
Picha: Wajumbe katika Mkutano mdogo wafuatilia jambo kutoka kwa Mwenyekiti wa kikao.
Suala
la msingi linalomfanya Bi.Flora kwenda kuwakilisha sauti za wanawake wengine
kuhusu haki ya kumiliki Ardhi, ni lile la kutoa ufafanuzi wa kina wa tamko la
madai ya wanawake wote wa vijijini lililowasilishwa Octoba 2016 kwa Mwenyekiti
wa AUC. Hivyo, itakuwa na wasaa mzuri kwa jitihada hizo za Wanawake waishio
vijijini kuweza kusikilizwa katika masikio ya viongozi, watunga sera na
wasimamiaji sera kutoka mataifa mbali mbali barani Afrika na jumuiya nyingine
za Kimataifa.
Picha: Mwenyekiti wa kikao akiwasilisha Tamko la Madai lililotokana na Kilimanjaro Initiative ya Octoba 2016.
Dhana
ya kutoa kipaumbele kwa wanawake waishio vijijini ilikuja kutokana na kuwepo
kwa 70% ya wanawake wanaoishi vijijini ukilinganisha na mjini, pia idadi hiyo
kubwa inawahusisha wanawake walio wengi wanaotegemea Ardhi kama rasilimali ya
kuendesha maisha yao ya kila siku kama vile kilimo na ufugaji.
Imetolewa na Jielimishe
Kwanza kwa niaba ya Action
Aid Tanzania jijini Dar es salaam.