Vitendo vya kikatili kwa watoto wa kike shuleni
vimeendelea kushika kasi na kushuhudiwa miongoni mwa jamii zetu na kuonekana
kuwa tatizo lililokosa mwarobaini. Ukatili huo wa kijinsia dhidi ya watoto wa
kike shuleni hujumuisha; kulazimishwa kuolewa katika umri mdogo,
mimba za utotoni, kubebeshwa majukumu makubwa ya familia mara tu wanaporudi kutoka shuleni au; unyanyasaji wa
kijinsia, kimwili na kihisia.
Ukizingatia takwimu ya Ripoti
ya matukio ya ukatili kutoka Halmashauri ya Wilaya Mafia, Januari- Machi 2016
inaonyesha kuwa asilimia 47 ya watoto wa kike Tanzania wanaolewa chini ya miaka
18, sababu inayowafanya waache shule mapema na kuanza majukumu ya familia,
ikifuatiwa na mimba za utotoni, Wilayani Mafia pekee, wastani wa wasichana 10
(0.2% ya wanafunzi wote wa kike) huacha shule mapema kutokana na mimba
zisizopangwa/ tarajiwa.
Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani imekuwa ni moja
ya Wilaya pekee nchini Tanzania kufaidika na mradi mpya unaoendeshwa na Taasisi
isiyo ya Kiserikali –Actionaid Tanzania wa kupambana na Ukatili wa mtoto wa
kike shuleni ujulikanao kama “Stop Violence Against Girls in Schools-SVAGS”.
Mradi wa SVAGS umekuja wakati muafaka ikiwa hali ya vitendo vya kikatili dhidi ya watoto shuleni ikiwa imeshamiri wilayani humo na kupelekea watoto wengi wa kike
kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu.
SVAGS ni mradi
wa miaka mitatu (2016-2018) uliozinduliwa rasmi Kitaifa kwa mara ya kwanza jijini
Dar es salaam na kuzinduliwa mapema tena mnamo tarehe 10 Februari 2017 katika
ngazi ya utekelezwaji Wilayani Mafia mkoani Pwani ukitarajia kuzifikia jumla ya shule 34 ndani ya
vijiji 26. Lengo kuu la mradi ni kuhakikisha kuwa haki ya mtoto wa kike kuwa huru, usalama na kupata elimu bora inapatikana, pia ionekane ikitendeka ndani ya jamii na kulindwa.
Shughuli za mradi-SVAGS zitajikita katika kufanya uchambuzi na uelimishaji umma na kujenga uwezo wa jamii kuhusu aina na madhara ya ukatili dhidi ya watoto wa kike. Pia kuondoa vikwazo vya kisheria vinavyorudisha nyuma juhudi za wanaharakati mbali mbali za kumuwezesha mtoto wa kike kupata haki ya elimu. Mradi upo mahsusi kuzungumizia na kushirikiana na wanajamii kuziondoa changamoto za mila, tamaduni, mitazamo na desturi potofu zinazochochea ukatili dhidi ya mtoto wa kike ndani na nje ya mazingira ya shule.
Shughuli za mradi-SVAGS zitajikita katika kufanya uchambuzi na uelimishaji umma na kujenga uwezo wa jamii kuhusu aina na madhara ya ukatili dhidi ya watoto wa kike. Pia kuondoa vikwazo vya kisheria vinavyorudisha nyuma juhudi za wanaharakati mbali mbali za kumuwezesha mtoto wa kike kupata haki ya elimu. Mradi upo mahsusi kuzungumizia na kushirikiana na wanajamii kuziondoa changamoto za mila, tamaduni, mitazamo na desturi potofu zinazochochea ukatili dhidi ya mtoto wa kike ndani na nje ya mazingira ya shule.
Akiongea na wadau (walimu
wa shule za msingi na sekondari, viongozi wa ngazi ya Wilaya-Mafia, Mbunge wa
Mafia) katika hafla ya uzinduzi wa mradi-SVAGS Wilayani Mafia, ndugu Amri Segera, mwendeshaji mradi ActionAid
Mafia aliwaomba wadau kuupokea mradi na kuonyesha ushirikiano katika ngazi
zote.
Ili kuvuta uelewa wa
mradi-SVAGS, washiriki wa hafla ya uzinduzi walipata wasaa wa kujadiliana mara
tu mwezeshaji kutoka ActionAid Tanzania ndugu Samwel Mesiak alipotoa utangulizi na kuboresha uelewa wa mradi.
Picha: Samwel Mesiak, mwezeshaji kutoka ActionAid Tanzania-Dar es salam akiwasilisha mada kuhusu historia na malengo ya mradi mpya-SVAGS. |
Picha: Mzazi na Mwalimu katika Wilaya ya Mafia akiongea kwa msisitizo kuhusu kukabiliana na changamoto zilizopo ndani ya jamii ili kuhakikisha mradi mpya wa SVAGS unakuwa jumuishi na kufanikiwa kwa ushirikiano wa wadau wote Mafia.
Ilikuwa ni wasaa wa mbunge
wa Mafia kuchangia na kujibu hoja mbali mbali zilizoletwa mezani kwa ufafanuzi
zaidi.
Picha: Mhe. Mbunge wa Mafia Mbaraka K.Dau akifafanua jambo kuhusu maoni ya baadhi ya washiriki kuhusu utekelezwaji wa mradi mpya-SVAGS wa kupambana na ukatili dhidi ya watoto wa kike wilayani Mafia.
|
Ulifika wakati muafaka wa
kuashiria kuzinduliwa kwa mradi wa SVAGS ambapo Samwel Mesiak kwa niaba ya ActionAid Tanzania alikabidhi nakala ya
mradi-SVAGS kwa mgeni rasmi ndugu Gilbert E. Sandagira kutoka ofisi ya Wilaya Mafia mkoani Pwani.
Picha: Samwel Mesiak wa ActionAid Tanzania akimkabishi mgeni rasmi-Gilbert E.Sandagira nakala maalum ya mradi SVAGS kuashiria uzinduzi rasmi na ukuanza kwa utekelezwaji wa mradi-SVAGS wilayani Mafia. |
Picha: Mgeni rasmi kutoka ofisi za Wilaya Mafia ndugu Gilbert E.Sandagira akisoma kwa makini nakala ya mradi SVAGS utakaotekelezwa Wilayani Mafia. |
Picha: Mgeni rasmi kutoka ofisi za Wilaya Mafia ndugu Gilbert E.Sandagira akishangiliwa na wajumbe pamoja na washiriki wa hafla ya uzinduzi kuashiria kukubalika kwa mradi SVAGS wilayani Mafia.
Mwisho
wa yote ilikuwa ni furaha kwa washiriki wote kupata picha ya pamoja kabla ya
kwenda kupata chakula cha mchana kwa pamoja.
Picha: Washiriki wote wa hafla ya uzinduzi wa mradi SVAGS wilayani Mafia katika nyuzo za furaha kuhakikisha kuwa wameupokea mradi-SVAGS na kuutekeleza kwa vitendo. Imetolewa na "Jielimishe Kwanza" kwa niaba ya ActionAid Tanzania-Mafia |