Na Henry Kazula,
Picha: Activista Tanzania |
Kufuatia
makubaliano ya Azimio la Kilimanjaro au Azimio la Arusha lilioboreshwa-“Kilimanjaro
Declaration” la tarehe 23-24 Agosti 2016, washiriki 272 kutoka ndani ya nchi takribani 45 yakiwemo
mashirika binafsi, asasi za kiraia,umoja wa wafanyabiashara, wawakilishi wa
vikundi vya wanawake na wanaume, Vijana, watu wenye ulemavu, Wabunge na
mashirika ya habari, na vikundi vya Dini na Waafrika waishio Nje ya Afrika walikuta
Arusha,Tanzania kujalidili mustakabali wa Bara la Afrika linaloaminishwa kuwa
ni masikini ilihali lina utajiri wa kutosha lakini watu watu wanaishi maisha
duni yenye changamoto mbali mbali zinazohusiana na uvunjivu wa amani, kutojali
haki na utu wao kwa maslahi ya wachache.
Mkutano
huo mkubwa ulikuja na maazimio makuu sita (6) kama ifuatavyo;
1. Afrika
ina utajiri.Kuitambua Afrika na Kuwaaminisha Waafrika na Dunia kwa ujumla wake
kuwa ni Tajiri na Utajiri huo ni wa watu wote na si kwa maslahi ya wachache
kisiasa na kiuchumi.Hivyo kupambana kuleta maendeleo ya kiuchumi yenye kujali
na kujumuisha maslahi ya kijamii na kujali Mazingira.
2. Afrika
ina vivutio vingi na vya kila aina, vyenye utajiri, hivyo hutosha kujiponya na
kurekebisha uharibifu wa kikoloni dhidi ya Waafrika na Mazingira.Pia itambulike
kuwa uafrika unamaanisha kuthamini utu wa wengine kupitia falsafa ya “Ubuntu”
iliyo fahali na utu wa Mwafrika.
3. Vijana
wa Kiafrika ni msingi imara wa kujenga na kuleta mafanikio katika Bara la
Afrika na ni chachu ya kuamsha na kuhamasisha wengine kujua haki na wajibu wa
kutenda Haki, kuleta Amani na Kuheshimu wengine.
4. Waafrika
waishio nje ya Afrika bila kujali kuwa wamehamia huko ugenini; ikiwa ni kwa
ajili ya utumwa, ukoloni au mfumo wa kisasa wa kuhama ili kutafuta maisha bora
wana wajibu wa kutumia mbinu na ujuzi katika taaluma zao kuchangia harakati za
kuwakomboa Waafrika wengine dhidi ya umasikini
5. Waafrika
tumejitoa kwa dhati kuwa wamoja, kwa ajili ya mustakabali wa Raia wema baadaye
kuwa tutashirikiana kutoa msaada wa kuanzia ngazi ya chini, kuwajengea uwezo
viongozi wa Serikali za mtaa na wanaharakati wa ngazi za chini ili kujenga
hamasa na msukumo kwa jamii kutoka ngazi chini hadi kuvuka mipaka.
6. Waafrika
tumejitoa kujenga harakati za Kiraia zenye kubeba jukumu la la uwakilishi na
kusimamia viwango vya ubora kiutendaji na maadili mema.
Kufuatia
maazimio hayo (6) washiriki, kwa niaba ya Waafrika, waliona ni vyema kuanzisha
Kampeni za kiuharakati kuanzia ngazi ya Serikali za mtaa, Kitaifa, Bara na
Dunia kwa ujumla ili;
a. kutanua
wigo wa kuchukua hatua kuhusiana na masuala ya kijamii na Siasa,
b. kupigania
haki za Wanawake na uhuru wao katika jamii,
c. kuelekeza
juhudi na mapambano yetu kuhusu Haki ya Usawa na kuheshimu utu wa wengine,
d. kushinikiza
watawala kuhusu utawala bora ili kupambana na rushwa na ufisadi,
e. kushinikiza
uwepo wa haki kuhusu masuala ya Tabianchi na Mazingira.
Hivyo
basi, mnamo tarehe 25 Mei 2017 jijini Dar es salaam, kampeni ijulikanayo kama
“Africans Raising Initiative” chini ya Actionaid Tanzania na Activista Tanzania ilizinduliwa
katika kilele cha maadhimisho ya “Siku Ya Ukombozi Wa Mwafrika”-“African Liberation Day”.
Kampeni
ya “Africans Raising Initiative” imekuja ikiwa na kauli mbiu “Africans Raising for Justice, Peace and
Dignity” ikimaanisha “Waafrika Waamke
Kutetea Haki zao, Amani na Utu wao”.
Uzinduzi
wa Kampeni hiyo uliambatana na tamasha la jioni kwa Vijana lililofanyika katika
kituo cha mafunzo, ubunifu na sanaa kwa watoto na vijana-Kigamboni Community
Centre (KCC) kama inavyoonekana katika picha.
Picha zote: Activista-Tanzania
Makala
hii imeandaliwa kwa msaada wa Ripoti ya
Makubaliano ya Mkutano.
Imetolewa
na Jielimishe Kwanza Blog