Kufuatia mapinduzi
makubwa ya Sayansi na Teknolojia nchini na duniani kwa ujumla mambo mengi
yamerahisishwa sana.
Wakati huo huo, uzuri wa Teknolojia unaweza
kuleta hasara endapo hakutakuwa na uelewa sahihi wa matumizi.Mfano halisi ni
matumizi ya Intaneti kupitia simu za viganjani.Nilitegemea, hii ingekuwa ni
fursa kwetu watanzania kuwasaidia watoto wetu kujifunza kwa kupata maarifa
kupitia njia hiyo…kinyume chake wanajamii wanatumia intaneti “kuchat” na masuala yanayowahusu, pia kupitia
mitandao ya kijamii kwa mambo yasiyojenga.
Wakati huo huo wanasema walimu hawatoshi na
hawafundishi…je umewahi kuchukua jitihada kutafuta njia mbadala? au tunasubiri
majibu ya mwisho ya mtihani yatolewe ndiyo tushike vichwa na kutoa lawama kwa
Serikali na walimu wake?
Hapa inatakiwa ieleweke kuwa mafanikio ya
watoto wetu yanaanzia na sisi wazazi/walezi ikiwa sambamba na watoto wenyewe
kujitambua na kutii.
Naomba niwathibitishie kuwa kwa hatua
tuliyofikia kimawasiliano na teknolojia ya intaneti kupitia simu zetu, hakuna
kitu kisichokosekana mtandaoni kuhusiana na masomo ya watoto wetu. Kuna mwalimu
anaitwa Google, You tube…tuanze
kuwatumia.
Cha msingi ni kumnunulia mwanafunzi muongozo
wa kila somo”syllabus” na kusimamia kujifunza.Shule inakuwa ni sehemu ya kwenda
kuuliza maeneo asiyoelewa na kufanya mazoezi kujifua na kile alichojifunza.
Inafika hatua nashangaa sana kuona teknolojia
inabadilika kwa kasi na watu wanaipokea kwa kasi kinyume na matumizi hasa
kwenye nyanja hii nyeti ya kujielimisha.
Si kitu cha ajabu kumuona kijana/mwanafunzi
anatumia tabiti “tablet” kusikilizia
muziki, kuchati na marafiki na kutazama sinema…ukimuuliza maswali kuhusu
masomo ya shuleni anakujibu mwalimu hajafundisha bado.Hivi, tutamtegea mwalimu
kwa asilimia 100% hadi lini?
Hili linachangia
kwa asilimia nyingi idadi kubwa ya wanafunzi wa sekondari kufeli na wale
walio vyuo vikuu kukosa mbinu za utendaji katika soko la ajira. Bila shaka unauona
mwelekeo wa jahazi la elimu ya Tanzania…huna haja ya kuwa na Shahada ya
uzamili(Masters) au ile ya uzamivu(PhD) ili kujua hatima yake.
Nikiendelea sana, watu watasema nawapangia
matumizi ya simu na tabiti au komputa zao.Lakini uhalisia ndiyo huo.Tunatakiwa
kubadilika ili kulikomboa jahazi la elimu ya Tanzania.
Ukiwa ni mzazi/mlezi mwenye mapenzi mema na unataka
kumuandaa mwanao kusoma kuendana na teknolojia ya habari na
mawasialino, pia usiyetaka mizigo isiyo ya lazima hapo baadaye, chukua hatua sasa kumsaidia mwanao kielimu na kujitambua kabla maji hayajamwagika!
Unaweza kuwasiliana Jielimishe Kwanza! kwa ushauri zaidi.
Simu ya kiganjani: +255 754 572 143
Barua pepe:
jielimishekwanza@gmail.com
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni